Na Steven Augustino,Tunduru
BIBI kizee wa Miaka 75 amefariki dunia baada ya kusombwa na maji yaliyo furika katika Mto uliopo katika Kitongoji cha Mchololo katika kijiji cha Tulieni Wilayani Tunduru.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa Bibi huyo aliyefahamika kwa jina la Laina Abdurahamani alikuwa na mkasa wakati akijaribu kuvuka mto huo wakati akitokea shambani kwake.
Taarifa hiyo iliendelea kufafanua kuwa akiwa katika harakati hizo ghafla mkondo wa maji makali yalimchukua na kuondoka.
Walisema baada ya tukio hilo wasamalia wema walipiga kelele za kuomba msaada na kwamba hadi wanafika waogeleaji katika eneo hilo walimkuta bibi huyo akiwa amekwisha fariki dunia na kufanikiwa kuuokoa mwili wake.
Mganga aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu Laina Dkt. Goerge Malawi alisema kuwa chanzo cha kifo hicho kilitokana na marehemu kunywa maji mengi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na akatumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kuacha tabia za kuishi kwa mazoea na akahimiza kudumisha utamaduni wa kuvushana.
Hili ni tukio la pili kusababisha kifo likifuatiwa na tukio la hivi karibuni ambapo hivi karibuni Mkazi waKijiji cha Kangomba said Abubakari (43) alilipotiwa kufariki dunia baada ya kupigwa na radi huku kukiwa na taarifa za 946 vyoo 35 vimebomolewa kutokana na mvua
hizo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment