About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Thursday, March 29, 2012

MKURUGENZI WA WILAYA YA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA ATISHIWA KUUAWA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda
Na Stephano Mango, Songea
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linawasaka watu wasiofahamika wanaodaiwa kumtishia kumuua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Mussa Zungiza(56) ambaye inadaiwa kuwa alitumiwa ujumbe wa maandishi kwenye simu yake ya mkononi akitishiwa kuuawa  .
Akizungumza na www.stephanomango.blogspot.com  jana mchana ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Michael Kamhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea machi 25 mwaka huu majira ya saa za mchana huko katika wilaya ya Namtumbo .
Kamanda Kamhanda alieleza zaidi kuwa inadaiwa mnamo siku tofauti za mwezi machi mwaka huu huko katika wilaya ya Namtumbo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  ya wilaya hiyo Zungiza alipokea ujumbe wa maandishi kupitia kwenye simu yake ya mkononi akitishiwa kuuawa. 
Alibainisha zaidi kuwa kwenye simu hiyo ya mkononi ujumbe huo ulitoka  katika namba  mbalimbali za simu,ambapo ujumbe wa kwanza ulitumwa machi 14 mwaka huu  majira ya saa 1:46 asubuhi na ujumbe wa pili ulitumwa  mach 14 mwaka huu majira ya saa 4:08 usiku .
Alieleza zaidi kuwa ujumbe huo ulieleza kuwa siku yoyote Zungiza atauawa kwa njia ya aina yoyote na kutoeleza chanzo au sababu ya kutaka kumuuwa ,jambo ambalo lilimpa hofu kubwa juu ya maisha yake .
Kamanda Kamhanda alisema kuwa Mkurugenzi Mtendaji huyo Zungiza  baada ya kupokea ujumbe huo kupitia kwenye simu yake ya mkononi  hatua ya kwanza alichukua ya kuwasiliana na kamati ya ulinzi ya wilaya hiyo na kisha alitoa taarifa juu ya ujumbe huo aliotumiwa wa vitisho katika kituo cha polisi cha wilaya ya Namtumbo ambako lilifunguliwa jalada la uchunguzi .
Hata hivyo kamanda Kamhanda alisema kuwa jeshi la polisi mkoani Ruvuma  linaendelea na upelelezi zaidi wa kina kuhusiana na tukio hilo ili kuwabaini watu waliohusika kumwandikia ujumbe kupitia simu yake ya mkononi ambao ulimtishia kumuuwa Zungiza.
 MWISHO

No comments:

Post a Comment