About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Saturday, March 10, 2012

WATU WAWILI WAMEFARIKI KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI WILAYANI TUNDURU

Na,Augustino Chindiye Tunduru

WATU wawili wamefariki dunia katika  matukio tofauti yaliyotokea wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma likiwemo tukio la kuuawa kwa kushambuliwa kwa mapanga kutoka na kilichodaiwa kuwa chanzo chake ni ugomvi wa kugombea eneo la kulima na mwingine kupigwa na radi.

Taarifa za tukio la Mauaji ya kugombea shamba lilitokea katika kijiji cha Nakawale katika Kata ya Nandembo ambapo Mtu aliyeuawa amefahamika kwa jina la Said Kaunya.

Akizungumzia tukio hilo mjomba wa marehemu Yusuph Mangalai alisema kuwa marehemu alikumbwa na maswahibu hayo usiku wa kuamkia machi 9 mwaka huu ambapo baada ya maharamia hao kutekeleza unyama huo waliuficha mwili wa marehemu kwa kuuzika pembeni mwa bwawa la maji
hali ambayo iliwapa wakati mgumu wanafamilia.

Hata hivyo Mangalai amewapongeza watu wote walioshiriki katika msako uliofanikisha kupatikana kwa mwili wa marehemu na kuuzika katika makaburi ya Njasi Mjini Tunduru.

Kwa mujibu wa taarifa hizo tukio la pili lililo husu kifo cha Mkulima kupigwa radi kilitokea katika kijiji cha Kangomba Wilayani humo ambapo aliye fariki dunia katika tukio hilo amefahamika kwa jina la Said Abubakari(43),

Akizungumzia tukio hilo Kaka wa marehemu Ally Hatibu alisema kuwa Marehemu alikumbwa na mkasa huo ulimpata wakati akipandikiza mihogo
shambani kwake.

Alisema katika tukio hilo marehemu aliunguzwa vibaya kuanzia chini ya mguu hadi kichwani upande wa kulia na kufariki papo hapo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa ruvuma Naftali Mantamba amethibitisha kuwepo kwa matukio hayo na kueleza kuwa polisi wanendelea na uchunguzi
ili sheria ifute mkondo wake.


Mwisho

No comments:

Post a Comment