Katibu Msaidizi wa SUFA Godfrey Mvula
Na Gideon Mwakanosya, Songea
CHAMA cha mpira wa miguu Manispaa ya Songea(SUFA) kimeanza kutoa fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa chama hicho, uchaguzi ambao umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Akizungumza mjini hapa jana Katibu Msaidizi wa SUFA, Godfrey Mvula alisema kuwa pamoja na utoaji wa fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa chama hicho, bado kamati ya utendaji wa SUFA kimepanga kuteua kamati ya kusimamia uchaguzi huo ambao utafanyika Machi 30 mwaka huu katika ukumbi ambao utakaopangwa.
Alisema wagombea wa nafasi hizo wanatakiwa wawe angalau na elimu sio chini ya kidato cha nne na awe mtu anayejihusika na soka kwa kuongoza vilabu ili kujenga ufanisi na uelewa zaidi katika kufanikisha na changamoto ya maendeleo ya soka katika Manispaa hiyo.
Alisema wagombea wote watakaojitosa kuchukua fomu na kuzirejesha watafanyiwa usaili wao wa mwisho Machi 25 kabla ya kuingia katika uchaguzi wa kuwania nafasi hizo za uchaguzi ambao watakaa madarakani kwa muda wa miaka mitatu.
Alisema SUFA kwa sasa inaongozwa na Mwenyekiti wake Gorden Sanga na ina vilabu vya soka 35 ikiwemo Majimaji ambavyo vimesajili kupitia msajili wa vyama vya michezo na vilabu nchini.
MWISHO
No comments:
Post a Comment