About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Monday, April 16, 2012

MBUNGE APINGA KUPITISHA BAJETI LAKINI AZIDIWA KETE NA MADIWANI

                

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA TUNDURU EPHRAIM OLE NGUYAINE
Na Augustino Chindiye, Tunduru

BARAZA la Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma limepitisha rasimu ya Mapngo wa bajeti ya mapato na matumizi ya Shilingi Bilioni 26.775 itakayotumika katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2012/2013 huku Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini Eng. Ramo makani na Diwani wa Kata ya Nakapanya  Halifa Wadari wakidai kutoiunga mkono bajeti hiyo.

Sambana na Mbunge huyo kukwamisha Bajeti hiyo isipite pia akatoa kauli ya  kushinikiza halmashauri hiyo kubadirisha matumizi ya Shilingi Milioni 300 zilizopangwa kutumika kujengea kilometa Tatu za Barabara kwa kiwango cha Lami iliyo pangwa kutekelezwa katika kipindi cha utekelezaji wa Bajeti hiyo zikiwa ni juhudi za halmashauri hiyo kuboresha mji huo akidai kuwa fedha hizo zipelekwe kujenga barabara za vumbi.

Bajeti hiyo ambayo ilipita kwa madiwani kupiga kura baada ya Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Faridu Hamisi kubaini kuwepo kwa mkanganyiko huo imebainisha  kuwa kati ya fedha hizo Shingi Bilioni 1.584 zitatokana na mapato ya ndani na shilingi Bilioni19.081zitatoka na Ruzuku kutoka serikali kuu.

Taarifa hiyo iliendelea kufafanua kuwa katika klipindi hicho pia halmashauri hiyo imepanga kutumia Jumla ya Shilingi bilioni 28,775,774,730 ambapo kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 19,0861,316,160 zitatumia katika matumizi ya kawaida, mishahara Shilingi Bilioni 16,653,115,160.

Upande wa kifungu cha matumizi mengineyo bajeti hiyo imekipangia Shilingi Bilioni 2,428,201,000, fedha kwa ajili ya maendeleo zimepangwa ni Shilingi Bilioni 8,109,726,570 huku bajeti hiyo ikielezwa kuwa na ongezeko la asilimia 37 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2012/2012.

Wakichangia kwa nyakati tofauti katika kikao hicho ambacho kilionekana wazi kumshinda kukiendesha Mwenyekiti wake kutokana na kuruhusu wajumbe kuchangia zaidi ya mara moja na kukiuka miongozo ya vikao vya mabaraza katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Klasta mjini hapa watoa pingamizi la kuto unga mkono bajeti hiyo walidai kuwa maandali zi yake hayakuzingatia uwiano wa ugawaji wa miradi katika kata zote 24/

Akifafanua kauli ya ombi lake la kubadilishwa kwa matumizi ya fedha za barabara ya Lami  Eng. Ramo alisema Mradi huo wa kujenga Kilometa Tatu ndani ya Mji wa Tunduru utakao ghalimu Shilingi Milioni 300 ni matumizi mabaya rasilimali kwani mradi huo hautakuwa na manufaa yoyote kwa madai kuwa fedha hizo zingewekwa katika mradi wa kutengeneza barabara vijjini kwa kiwango cha Changarawe halmashauri hiyo ingewawezesha wakulima wengi kusafirisha mazao yao na kuyapeleka katika masoko.

“Mimi kama mwakirishi wa wananchi wa Jimbo la Tunduru Kaskazini Siungi mkono Bajeti hii na msimamo wangu ni fedha hizo zibadilishiwe matumizi na kupelekwa kutengeneza barabara za Vijijini ziweze kuwasaidia wananchi wengi zaidi kuliko kutengeneza Barabara ya lami ambayo haitawanufaisha wengi na itajengwa katika kieneo kidogo “ alisema Eng. Ramo.

Aidha viongozi hao pia wakabainisha kuwa Bajeti hiyo imependelea na kupeleka miradi mingi zaidi upande wa Jimbo la Tunduru Kusini kutokana kupeleka miradi mingi zaidi ikilinganishwa na miradi iliyo ainishwa kutekelezwa katika Kata za Jimbo la Tunduru Kaskazini.

 Pamoja na viongozi hao kutofautia na madiwani wenzao kutokana na ushindi walioupata kutokana na kupiga kura, Diwani wa kata ya Nandembo alitolea mfano kutokana na kilichodaiwa kupangiwa miradi mindi Anitha Komba aliinuka na kueleza wazi wazi kuwa kitendo kilichofanywa na mbunge huyo ni mbaguzi na hakiitakii maendeleo ya dhati wilaya yao.

Akijibu tuhuma hizo Mkurugenzi matendaji wa halmashauri ya Wilaya hiyo Ephraim Ole Nguyaine alimtaka Mbunge huyo kuheshimu kanuni na miongozo ya uendeshaji wa mabaraza akikataa kata kata kuwa hawezi kukubaliana na maelezo ya viongozi hao waliotaka bajeti hiyo ijadiliwe upya katika ukumbi huo.

Guyainne aliendelea kueleza kuwa kabla ya kukamilika kwa mchakato huo bajeti hiyo ilipitiwa na kamati husika na kuidadavua kwa mapana na marefu hivyo kitendo cha viongozi hao kutaka bajeti hiyo ijadiliwe upya inalenga kukiuka taratibu na miongozo iliyo wekwa na mamlaka husika.

Alifunga kikao hicho Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya hiyo diwani Faridu hamisi alissitiza kuwa halmashauri yake itasimamia kwa makini na kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika kulingana na matumizi yaliyo elekezwa.

Mwisho


No comments:

Post a Comment