About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Wednesday, May 16, 2012

WAMILIKI WA MASHINE WAMSHUKIA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI

Na Stephano Mango, Songea
WAMILIKI wa mashine za kukoboa na kusaga nafaka katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamemshukia Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kwa kitendo chake cha kukaa kimya wakati wananchi wanateseka kwa kukosa nishati ya umeme kwa muda mrefu
Wakizungumza na waandishi wa habari jana wamiliki hao walisema kuwa kitendo cha waziri huyo kukaa kimya kinaashiria kushindwa kwake kazi toka mapema kwani haiwezekani wananchi wanateseka bila kuwa na nishati ya umeme na kusababisha gharama za maisha kupanda
Walisema kuwa kitendo cha shirika la umeme mkoani humu kushindwa kutoa huduma hiyo kwa wakati mbali ya kusababisha usumbufu kwao pia kimekuwa kikiwakosesha mapato ambayo wanayatumia kulipa kodi kwenye mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) kutokana na hasara zinazosababishwa na ukosefu wa umeme
Mkurugenzi wa kampuni ya Mtazamo Enterpress, Julius Mlawa akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kiwanda cha kampuni hiyo kinachojishughulisha na ukoboaji nafaka, usagaji na uuzaji wa unga alisema kuwa wananchi wa Manispaa ya Songea wanapaswa kuokolewa kutokana na mgao mkubwa na usio na kikomo wa umeme unaoendelea kuwakabili
Mlawa alisema kuwa mashine za kusaga nafaka ambazo zipo katika baadhi ya maeneo ya Manispaa hiyo zimeshindwa kutoa huduma kwa muda muafaka na kusababisha wananchi walio wengi kulazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma nje ya Manispaa ambako kuna mashine za kusaga nafaka zinazotumia mafuta ya Dizeli na kusababisha bei ya huduma hiyo kupanda mara mbili ikilinganishwa na awali
Alisema kuwa bei ya unga wa mahindi ambayo hapo awali ilikuwa ni shilingi 500 kwa kilo hivi sasa kilo moja ya unga wa mahindi ni shilingi 1200 na bei ya mchele kwa miezi iliyopita kabla ya tatizo la umeme halijaanza kujitokeza kama ilivyo sasa ilikuwa ni shilingi 1000 kwa kilo lakini hivi sasa kilo moja ya mchele ni kati 1800 hadi 2000.

Alifafanua kuwa bei hizo zinaendele kupanda siku hadi siku kutokana na TANESCO  kushindwa kutoa huduma ya umeme kwenye maeneo ya manzese, Mfaranyaki , Bombambili, Majengo, Lizaboni Mjimwema na Msamala ambako ndiko kuna mashine nyingi zinazo saga nafaka  na badala yake umekuwa ukiwashwa kwa mgao ambao ratiba yake haufahamiki  kwa wamiliki wa mashine hizo.

Alisema kuwa katika kiwanda chake kuna wafanyakazi zaidi 30 ambao wanashinda kiwanda wakisubiri umeme ili waweze kufanya kazi bila mafanikio huku wakilipwa posho zao za kila siku bila kufanya kazi jambo linalosababisha hasara kubwa
Alieleza zaidi kuwa kutokana na ukosefu wa umeme ambao umekithiri katika manispaa ya Songea wafanyabiashara wengi wanashindwa kurejesha mikopo waliyokopa kwenye taasisi za fedha jambo ambalo ni hatari kwa biashara zao na jamii ambayo inanufaika na biashara hizo
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo huenda akalazimika kusitisha kwa muda kutoa huduma ya usagaji na ukoboaji wa nafaka kama hali hiyo ya ukosefu wa umeme wa uhakika haitafanyiwa kazi na shirika hilo la umeme mkoani humu kwa sababu mbali ya kukosa mapato lakini imekuwa ni usumbufu kwa wananchi ambao wanahitaji huduma hiyo.
Kwa upande wake Meneja wa shirika la umeme mkoa wa Ruvuma Mhandisi Monika Kebara alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na alisema hivi sasa huduma hiyo ya umeme inatolewa kwa mgawo kwa sababu uwezo wa ufuaji wa umeme umepungua sana kutokana na kuharibika kwa mitambo ya kuzalisha umeme iliyopo Kibulang’oma mjini hapa.
Kebara alisema kituo hicho kina mashine saba za kuzalisha umeme lakini kwa hivi sasa ni mashine tatu ndizo zinazofanya kazi hiyo kwa kutoa Megawati 2.6 wakati mahitaji ni Megawati 5 hasa ikizingatiwa kuwa katika mji wa Songea shirika hilo lina wateja elfu kumi na mbili hivyo bado umeme utaendea kutolewa kwa mgao lakini maeneo muhimu kama hospitali, ofisi za serikali na kambi za jeshi umeme utaendelea kutoleawa kama kawaida
MWISHO

No comments:

Post a Comment