MWENYEKITI WA KAMATI YA MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 38 YA CCM TAIFA DKT EMMANUEL NCHIMBI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI SONGEA
NA, STEPHANO MANGO, SONGEA
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Ruvuma Wametakiwa
kuendelea kujipanga Kikamilifu Katika Sherehe za Maadhimisho ya kutimiza miaka
38 ya kuzaliwa kwake ambayo yanatarajiwa kufanyika Katika Viwanja vya Majimaji
Mjini Songea Februari 2 mwaka huu
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jana katika Viwanja vya
Ccm Mkoa wa Ruvuma Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe hizo za Maadhimisho
ya miaka 38 Ccm Dkt Emmanuel Nchimbi alisema kuwa Maadhimisho hayo ni Muhimu
sana kwani yanalenga zaidi kukumbuka toka kuzaliwa kwake hadi hapa kilipo hivyo
wanaccm hawana budi kuhakikisha wanajipanga vizuri kufanikisha maadhimisho hayo
Dkt Nchimbi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo La Songea Mjini
alisema kuwa Wanaccm wanatakiwa kutumia fursa hiyo muhimu kujiimarisha kiuchumi
na kiutalii kwani kuwepo kwa wageni wengi wakati wa Maadhimisho hayo
kutachangia ununuzi wa bidhaa mbalimbali ambazo zinazalishwa na Wajasiliamali Mjini
hapa
Alisema kuwa Kitendo cha Viongozi Wakubwa wa Ccm Taifa katika Vikao Vyao kuridhia kuwa
Maadhimisho hayo Kufanyika Songea ni cha Busara sana hivyo Tunawajibika
kujiandaa vyema kuwapokea Wageni na kufanya mambo ambayo yanaendana na maudhui
ya Maadhimisho hayo
Alieleza kuwa Mwaka huu ni Mwaka wa Uchaguzi ni lazima
wanachama na wapenzi wa chama hicho kuelezea mafanikio yaliyopatika katika
miaka 38 ya kuzaliwa kwa chama hicho makini na kikubwa cha siasa nchini ambacho
kinaongoza nchi kwa zaidi ya miaka 50 sasa
Alifafanua kuwa Mafanikio ambayo chama hicho na kwa namana
inavyotatua changamoto za Wananchi wake ndio msingi wa Vyama vya Upinzani
Nchini kukionea wivu na hata kukieneza
vibaya katika mikutano yao ya hadhara
Hata hivyo amewataka Viongozi wote wa Jumuiya za Chama hicho
kuendelea kujipanga ili kufanikisha Maadhimisho hayo Muhimu yatahudhuriwa na wageni mbalimbali
toka nchi jirani pamoja na wegeni kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.
MWISHO
No comments:
Post a Comment