About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Monday, January 19, 2015

RC MWAMBUNGU AWACHARUKIA WALIMU WAKUU RUVUMA
 MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu

NA, STEPHANO MANGO, SONGEA

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu amewataka Walimu wakuu wa Sule za Sekondari na Msingi za Serikali Mkoani Ruvuma kutomrudisha Nyumbani Mwanafunzi Yeyote Kwa Kosa la Kutokuwa na ada, michango au Sare za Shule badala yake Washirikiane na Mzazi kuweza kutatua tatizo husika

Akizungumza na www.stephanomango.blogspot.com  Ofisini Kwake alisema ni Marufuku kumfukuza Mwanafunzi Shule kwa kosa ambalo sio lake kwani anayewajibika kulipa Ada au Michango  husika ya Shule ni Mzazi na Sio Mwanafunzi

Mwambungu Alisema kuwa Mwanafunzi anasomeshwa na Mzazi au Mlezi wake kitendo cha Kumfukuza Shule kwa Kosa ambalo sio Lake ni kumnyanyasa na  kumnyima haki yake ya msingi ya kupata Elimu Bora na Kwa Wakati Stahiki

Alisema kuwa Jukumu kubwa la Walimu ni Kutoa Elimu Bora na Malezi mazuri kwa Watoto kwani wao pia ni Sehemu ya Wazazi kitendo cha kuwafukuza kinaleta picha mbaya kwani mara nyingi wanafunzi hao wanapofukuzwa  wamekuwa wakiranda randa mitaani hali inayoweza kusababisha wakapatavishawishi vya kuingia kwenye makundi mabovu ya uvutaji bangi na ngono zembe kabla ya wakati

Alifafanua kuwa Walimu wanachotakiwa kufanya ni kuwasiliana na Wazazi wa Wanafunzi husika  Kupitia Maafisa Watendaji wa Vijiji au Mitaa ili kubaini ni tatizo gani ambalo linalomfanya Asilipe Ada na Michango kwa Wakati

"Maafisa Elimu na Wakaguzi hakikisheni agizo hili linatekelezwa kikamilifu ili kuongeza kiwango cha ufaulu katika Mkoa wa Ruvuma na kwamba yeyote Atakaye bainika kuzembea kutekeleza Wajibu wake basi Sheria zitafuata juu yake", Alisema Mwambungu

Alieleza kuwa Juhudi za Ujenzi wa Maabara ikiwa ni Utekelezaji wa Agizo la Rais Jakaya Kikwete zinaendelea kwa kasi Kubwa na Ifikapo mwezi Mei Mwaka huu Zitakuwa Zimekamilika na Kuanza kutumika kadri ilivyopangwa
MWISHO


No comments:

Post a Comment