MBUNGE WA JIMBO LA NAMTUMBO VITA KAWAWA
NA, STEPHANO MANGO,NAMTUMBO
WAPIGA KURA wa Jimbo
La Namtumbo Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Wametakiwa Kumfanyia Tathimini Mbunge
wao Vita Kawawa Waliomchagua katika vipindi viwili Mfululizo Mwaka 2005 na
Mwaka 2010 kama ametekeleza vyema Ilani ya Chama chake na Ahadi alizozitoa
wakati anaomba kura katika Chaguzi mbili hizo
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini hapa Jana Afisa
Elimu Mstaafu na Mfanyabiashara Ally Mbawala Alisema kuwa Mwaka huu ni Mwaka wa
Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani hivyo ni fursa Muhimu Sana kwa
Wananchi kuchukua tafakari Stahiki ya utendaji Kazi wa Wawakilishi wao
waliowachagua vipindi vilivyopita na Kuwahukumu katika sanduku la kura
Mbawala Alisema Kuwa Kipindi hiki sio cha kufanya mchezo ni
kipindi cha kujitendea haki kwa Kuangalia utatuzi wa Changamoto zilizokuwepo
kabla ya kumchagua Kiongozi husika hadi leo ili kujiridhisha utendaji kazi wake
na kama anataka kugombea tena basi ahukumiwe kwa mujibu wa kipimo chake cha utendaji
Kazi
Alisema kuwa Jimbo la Namtumbo lina Fursa Nyingi sana za Kimaendeleo kwani kuna ardhi nzuri,
Misitu, Madini , Mbuga za Wanyama na Maliasili zingine nyingi na wananchi wake
ni wakulima wazuri wa mazao mbalimbali ya chakula , hivyo ni muhimu kupima kama
rasilimali hizo zimeweza kusimamiwa na kutumika vizuri na kama zimewezesha kuinua
maisha ya wakazi wa Jimbo hilo
Alieleza Kuwa Jimbo hilo ndilo ambalo lilikuwa Maarufu kwa
Kilimo Cha Tumbaku na Mbunge wa Jimbo hilo alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Tumbaku Tanzania hivyo ni vyema tukamtafakari
kwa kina kama ameweza kushiriki
kikamilifu kufufua vyama vya Ushirika na kukuza zao hilo ambalo ndilo zao kubwa
la kiuchumi kwa Wakazi wa Namtumbo
Alifafanua kuwa kabla ya uchaguzi ni muhimu sana Wapiga Kura
wa Jimbo hilo wakawa na vipaumbele vyao vya Kimaendeleo ili waweze kutengeneza
ajenda ya pamoja badala ya kusubiri ilani za Vyama au matakwa ya Mbunge ambayo
kimsingi hayana tija katika maisha yao
“Mimi ni Mzaliwa wa Namtumbo lakini kila Siku Maisha ya
Wakazi Wa Jimbo hili yanazidi kuwa magumu kwa sababu mbalimbali hali ambayo ina
hatarisha amani na utulivu katika jamii kwani kundi la walionacho wanaendelea
kunufaika huku kundi kubwa la wasio nacho wakiendelea kuhangaika”
Alieleza zaidi kuwa hadi leo bado kuna Wakazi wa Jimbo hilo
hawajafikiwa na huduma za Maji Safi Na Salama, Elimu, Afya, Miundombinu, huduma za kiuchumi na
Mawasiliano hali ambayo inaendelea kuwafanya wawe masikini zaidi
MWISHO
No comments:
Post a Comment