Mzee Samwel Mapunda akimpongeza Mgeni Rasmi Juma Nyumayo mara baada ya kumaliza kuwahutubia katika sherehe za mahafali katika shule ya Msingi Mkombozi na kuwapatia msaada wa mifuko kumi ya Saruji(Cement) na wazazi kuahidi kubebelea mchanga kwa ajili ya kusakafia darasa la Awali shuleni hapo
Kushoto Padre Chinguku akiwaonyesha,Gideon Mwakanosya,Mwandishi Mkongwe wa Magazeti ya Nipashe na guardian na Mjumbe wa Bodi ya Swacco(katikati)kulia ni mzee Samwel Mapunda namna watoto walivyopendeza katika mahafali hiyo
Kulia ni Gideon Mwakanosya akisalimiana na Mjapani ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja kutokana na pilikapilika za kufanikisha mahafali hiyo,pembeni ni wanafunzi wakiwa na hamu ya kuendelea kusherehekea mahafali hayo
Viongozi mbalimbali wakiwa na Mgeni Rasmi Nyumayo katika darasa linalodaiwa kuwa ni la Awali ambalo halijasakafiwa na mgeni Rasmi kutoa mifuko kumi ya Saruji na wazazi kuahidi kutoa mchanga wa kusakafia darasa hilo kwa lengo la kutaka watoto wao wakombolewe na elimu itolewayo Shuleni hapo
Watoto wakitafakari kwa umakini hatima ya elimu yao mara baada ya kupewa Saruji na mchanga utakaotumika kuondoa vumbi katika darasa lao
Watoto wakitamani kucheza kiduku kutokana na furaha kubwa waliyonayo baada ya kusikia kuwa darasa lao litakuwa katika hali stahiki kwa kuendelea kupatiwa elimu kusudiwa
Viongozi wa Serikali ya Kata ya Bombambili wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni rasmi nje ya darasa la Awali ambalo linatarajiwa kukarabatiwa hivi punde
Wa kwanza kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mkombozi Imelda Mbawala akiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni Rasmi na familia ya Kazimguru
Sherehe ikifunguliwa kwa mbwembwe zote kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu Mkoa wa Ruvuma,ikiongozwa na Mgeni Rasmi Nyumayo,kushoto ni Diwani wa kata ya Bombambili Kenny Moto akisaidiwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mjimwema Twalik Mpakasini wa kwanza kushoto
Mwalimu Mstaafu Agnes Nkoma aliyeanza kazi mwaka 1972 na kustaafu utumishi wa UMMA,mei mwaka huu 2011 akipokea zawadi ya utumishi uliotukuka kutoka kwa Mgeni Rasmi Nyumayo katika Mahafali ya Shule ya Mkombozi ambapo amestaafu akiwa Mwalimu Mkuu katika Shule hiyo
Mwalimu Bibi(Notbuluga Mapunda)akimshukuru kwa utumishi wake Mwalimu Agnes Nkoma na kumtakia maisha mema ya kustaafu utumishi wa UMMA
Sherehe yoyote duniani haiwezi kufanikiwa bila kuwepo mziki au burudani,sasa kazi ipo Dj MKongwe ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Bombambili akionyesha umahiri wake wa kusugua Cd na kuchezesha pini za uhakika kwa wazee na vijana(Masharobaro)
Wahitimu wa darasa la Saba katika Shule ya Msingi Mkombozi wakimng'ang'ania Mgeni Rasmi Nyumayo kucheza muziki wa kisasa bila kufahamu kuwa mwenzao alikuwa kijana wa zamani na sasa akitaka kutikisa kichwa na kisigino chini lazima achezewe nyimbo za zamani kama vile Ottu Jazz Band,Sikinde na zingine za aina hiyo bila kusahau TWISTI
Hapo sasa Mgeni Rasmi akiwa na Wazee wenzake akisakata rumba katika mahafali ya aina yake huku akitamani kuvua koti la suti ili aweze kumudu vizuri rumba hilo
Ukosikia kipindi maalumu ndio hicho cha kuongeza vocha ya tumbo ili uweze kupata nguvu za kufanya jambo na uwezo kamilifu wa kufikiri,kwa kweli sherehe hiyo ilikuwa ni ya aina yake kufanyika mjini hapa,tuwashukuru wote waliowezesha mtandao huu wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ kufika shuleni hapo na ukumbi ili kuweza kuwaletea wasomaji na wadau wa mtandao huo taarifa na burudani
No comments:
Post a Comment