Na Gideon Mwakanosya,Songea.
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linawashikilia watu wanne wakazi wa kijiji cha kitanda wilayani Tunduru kwa tuhuma za kumpiga na kitu chenye ncha kali sehemu mbambali za uso na kumsababishia kifo mwanamke mwenye umri wa miaka 60 mkazi wa kijiji hicho.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda akizungumza na mwandishi wa mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/, Gideon Mwakanosya kutoka mjini Songea, alisema kuwa tukio hilo limetokea septemba 10 mwaka huu mwajira ya saa 2.00 usiku huko katika kijiji cha kitanda kilichopo wilayani Tunduru.
Kamuhanda amemtaja aliyeuwawa kuwa ni Mwanahawa Landi (60) mkazi wa kijiji hicho na amewataja wanaoshikiliwa na polisi kuhusiana na tuhuma za mauaji hayo kuwa ni Mohamed Saidi (25), Kassim Said (39), Said Baina (76) na Ally Said (37) wote wakazi wa kijiji cha kitanda.
Alifafanuwa zaidi kuwa inadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio Mohamed Issa (70) alitoa taarifa kwenye kituo cha polisi cha Tunduru kuwa Mwanahawa ameuwawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali usoni na ambayo yalimsababishia sura yake kuharibika kabisa na watu wasiofahamika.
Kamanda Kamuhanda alisema kuwa chanzo cha mauaji hayo bado kinachunguzwa lakini tayari watu wanne polisi imewatia mbaroni kwa mahojiano zaidi na kwamba uchunguzi utakapokamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma za mauaji.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment