About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Sunday, October 23, 2011

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA LEVINA ADAKWA,AKUTWA NA VITU VYA MAREHEMU

Na Gideon Mwakanosya, Songea
 
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limemtia mbaroni Thomas Jilala (22) mkazi wa Mwanza kwa tuhuma za kumuua anayedaiwa kuwa mpenzi wake Levina Kihwili (26) mkazi wa Mfaranyaki katika Manispaa ya Songea ambaye alikutwa akiwa amekufa kwa kunyongwa shingo katika nyumba ya kulala wageni ya Mikumi mjini hapa
 
Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi, Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma, Inspekta Paulo Mashimbi alisema tukio hilo lilitokea Octoba 22 mwaka huu majira ya saa 2 asubuhi huko kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni chumba namba Kumi.
 
Insekta Mashimbi alisema kuwa ililetwa taarifa katika kituo kikuu cha polisi mjini Songea kuwa katika nyumba ya kulala wageni ya Mikumi chumba namba Kumi kilichokuwa kikitumika na watu wawili alikutwa mwanamke akiwa amefariki dunia huku mwanaume aliyekuwa naye akiwa amekimbia.
 
Alisema mnamo octoba 23 mwaka huu majira ya saa Sita usiku mtuhumiwa anayedaiwa kufanya mauaji hayo Jilala ambaya anadaiwa alikuwa Mpenzi wa marehemu alikamatwa akiwa anatoroka kuelekea barabara ya Songea-Tunduru maeneo ya Namtumbo.
 
Alieleza kuwa mtuhumiwa Jilala baada ya kukamatwa alikutwa na baadhi ya vitu vya marehemu ikiwemo Saa aliyokuwa ameivaa kabla ya kuuawa pamoja na simu Mbili za mkononi vyote vikiwa ni mali ya marehemu.
 
Alifafanua kuwa mtuhumiwa pia alikutwa na vifaa vingine vilivyoibiwa kwenye ofisi aliyokuwa akifanyia kazi marehemu usiku wa kuamkia siku ya tukio hilo la mauaji.
 
Hata hivyo vyanzo vya habari vimeeleza kuwa Jilala kabla hajafanya kitendo hicho cha kinyama alikuwa akionekana mara kwa mara katika Ofisi ya marehemu ijulikanayo kwa jina la Mpenda Production kwa madai kuwa amekuja kutengeneza kadi za harusi ya kaka yake.
 
Aidha Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limesema linaendelea na uchunguzi dhidi ya tukio hilo na kwamba baada ya uchunguzi huo kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shitaka la mauaji linalomkabili.
 
Mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya mkoa mjini Songea, Dkt. Benedict Ngaiza alipohojiwa na waandishi wa habari ofisini kwake amethibitisha kuuawa kwa Levina na kwamba uchunguzi unaonesha kwamba alivunjika shingo baada kupigwa na kitu kizito.
 
Wakati huo huo Jeshi la Polisi linawatafuta watu wasiofahamika kwa tuhuma za kumuua mtu mmoja wa Kiume ambaye jina lake halijapatikana kwa kumchoma moto na mwili wake kuharibika vibaya.
 
Insekta Mashimba alisema tukio hilo lilitokea octoba 23 mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi katika eneo la shule ya Msingi ya Bombambili mjini Songea ambako inahisiwa kuwa marehemu huyo alikuwa ni kibaka.
Mwisho.  

No comments:

Post a Comment