Na Steven Chindiye,Tunduru
ZAIDI ya Wanafunzi 500 wa Shule ya Sekondari ya Kutwa Mataka wametishia kutoingia madarasani hadi uongozi wa Halmasahuri ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma watakapofanya mabadiliko ya kumrejesha Shuleni hapo aliyekuwa Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Johnes Liombo.
Msimamo huo umetolewa na wanafunzi hao wakati wakiongea na uongozi wa Halmashauri hiyo baada ya uongozi huo kupokea maandamano ya amani yaliyofanywa na wanafunzi hao kwa nia ya kupinga uhamisho wa mwalimu huyo.
Sambamba na msimamo huo wanafunzi hao, wakiwemo wanafunzi wa kidato cha Pili wanaotarajia kufanya Mtihani wa Taifa hivi karibuni walidai kuwa endapo mgogoro huo hautapatiwa ufumbuzi mapema nao hawataingia katika chumba cha mtihani huo.
Akisoma taaria ya wanafunzi hao kaka Mkuu wa shule hiyo Rajab Said alisema kuwa wanafunzi hao wamechukua hatua hiyo baada ya kubaini kuwa uhamisho wa Mwalimu Liombo ambaye amekaa miezi mitatu katika Shule yao ni wa uonevu na kwamba kitendo hicho hakiitakii mema Shule yao.
Alisema mwl. Liombo ni mwalimu wa msaada kutokana na tabia yake ya kujituma katika ufundishaji na kwamba wanafunzi wote wanaamini kuwa endapo angeendelea kubakia katika shule hiyo wanafunzi wote wangepiga hatua kitaaluma.
Akijibu kero hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mwl. Rashid Mandoa ambaye alikuwa akisaidiwa na baadhi ya wakuu wa Idara mbalimbali na kuwaomba wanafunzi hao warudi shuleni kwa ajili ya kuendelea na masomo na kuwataka waliwataka wanafunzi hao kutokubali kutumiwa ama kufanya maandamano kwa maslahi ya watu.
“kweli nimeamini kuwa wanafunzi wa Mataka Sekondari hawana nidhamu” alisema Mwl. Mandoa na kuongeza kuwa endapo wanafunzi hao wangekuwa na nidhamu walipaswa kufuata taratibu za kuonana na uongozi kwa kufuata taratibu zinazotakiwa na sio kufanya maandamano kama walivyo fanya.
Aidha Mwl.Mandoa aliwahakikishia wanafunzi hao kuwa uhamisho wa mwalimu Liyombo ni wa kawaida kama wanavyohamishwa watumishi wengine wa Halmashauri hiyo
Nae Afisa Elimu wa Shule za Sekondari wa Wilaya hiyo Mwl. Alli Mtamila katika maelezo yake pamoja na mambo mengine aliwataka wanafunzi hao kurejea Shuleni kwa madai kuwa idara yake inafuatilia tatizo hilo na kulitafutia ufumbuzi ombi ambalo lilikataliwa na wanafunzi hao na kuwafanya watawanyike kurejea majumbani mwao.
Akiongea kwa niaba ya wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo Fadhili Makanjila alisema kuwa kitendo cha uhamisho huo kimewakatisha tamaa wazazi na wanafunzi kwa katika kipindi cha Mwalimu Liombo kulikuwa na mikakati mizuli ya kuiinua kitaaluma shule hiyo.
Makanjila aliitaja miongoni mwa mikakati hiyo kuwa ni pamoja na Mkuu huyo kuwa na mipango shirikishi tofauti na walimu wengine na akatolea mfano mpango wa kuwaweka wanafunzi wa kidato cha pili katika KAMBI ambalo wanafunzi hao walikuwa wakipatiwa masomo ya ziada nyakati za usiku ikiwa ni mikakati ya kuwa andaa na mithani ijayo
No comments:
Post a Comment