About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Thursday, December 29, 2011

WAKUU WA MIKOA INAYOLIMA KOROSHO KUANDAMANA KUMUONA RAIS JAKAYA KIKWETE

Na,Steven Augustino Tunduru

WAKUU wa Mikoa inayolima Korosho  nchini wameahidi kupeleka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete kero ya ubabaishaji wa bei ya soko la zao hilo ili aweze kulitafutia ufumbuzi wa kudumu zikiwa ni juhudi za kuwawezesha Wakulima kupata matunda ya jasho lao.

Hayao yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma  Saidi Mwambungu wakati akiongea na wadau wa maendeleo waliojitokeza katika kikao cha dharula cha kujadili hatima ya tukio la ubabaisshaji wa soko la Korosho ambalo msimu huu bei yake imeonesha kusuasua kilichofanyika katika ukumbi wa Boma la halmashauri ya Wilaya hiyo mjini hapa .

Sambamba na maamuzi hayo pia Mwambungu na kamati hiyo ikatoka na azimio la kutouza Korosho hizo kwa Makampuni hayo babaishaji vinginevyo wakubali kununua Korosho hizo kwa Bei itakayo kubalika na wakatumia nafasi hiyo kumuomba Meneja wa Benki ya Nmb Omari Mleche kuongeza mkopo kwa vyama vya msingi ili kuwezesha kununua Korosho zote kwa wakulima wakati juhudi za kutafuta Soko la uhakika zikiendelea.

Akifafanua taarifa hiyo Mwambungu alisema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa na Wakuu wa Mikoa ya Lindi Ruvuma na Mtwara baada ya kubaini kuwerpo kwa ubabaishaji wa Soko hilo ulio oneshwa na Wanunuzi hao wakubwa Korosho katika Msimu huu hauwezi kufumbiwa macho na Serikali na kuwaacha Wakulima wakiteseka bila msaada wa Serikali yao. 

Awali wakitoa taarifa ya ubabaishaji wa Soko la Mazao hayo Meneja wa Chama Kikuu cha Wakulima wa Korosho TAMCU Ltd  Imani Kalembo na Mwenyekiti wa  Chama hicho Mahamudu Katomondo walisema kuwa  ubabaishaji huo umeonekana katika minada mitatu iliyopita ambapo Makampuni ya Abbas Eport Treding Co.Ltd na Olam Co. Ltd awali wote waliomba kununua chini ya Bei  ya Tsh. 1500 kwa kilo moja hali iliyo onesha kuwa makampuni hayo yana ajenda ya siri ya kutaka chama hicho kishindwe kuwalipa Wakulima wake malipo yao ya awamu ya pili.

Walisema kinacho watia mashaka zaidi viongozi hao na kuwafanya wabaini uwepo wa mchezo mchafu kutoa katika Makampuni hayo ni kitendo cha Makampuni hayo pekee kati ya Makampuni 70 ambayo yalijiandikisha na kuomba kununua Korosho hizo katika Msimu huu wa Mwaka 2011/2012,

Wakizungumzia taarifa ya ununuzi Korosho hizo kutoka kwa wakulima walisema kuwa hadi sasa vyama vya msingi vya ushirika vime kwisha kusanya jumla ya Kilo 4,554334 kati ya Kilo 7,000,000 zinazotarajiwa kununuliwa katika Mismu huu na chama chao.

 Wakitoa maoni yao wabunge wa Wilaya ya Tunduru  Eng. Ramo Makani na Alhaji Mtutura Mtutura waliiomba Serikali kutumia Fedha zilizo idhinishwa katika Bajeti iliyopita kwa ajili ya Matumizi ya dhalula ili zitumike kununula Korosho hizo kutoka kwa Wakulima zikiwa ni juhudi za kuwaondolea adha hiyo.

Nao Madiwani Kazembe said  wa kata ya Ligunga na Burhani Nakanje wa Kata ya Marumba mbali na kuutuhumu uongozi wa Kiwanda cha Kubangulia Korosho kinacho milikiwa na Kampni ya Korosho Africa Ltd kuto kuwa na msaada kwa wakulima wa Wilaya yao waliiomba Serikali kuwa na macho na Wanunuzi hao vinginevyo watawaangusha na kuwafanya wananchi kukosa imani na Serikali yao.

Wakijibu tuhuma za Kiwanda hicho kuto kuwa na msaada kwa Wakulima wa zao hilo msimamizi wa Kiwanda hicho Dinesh Poojali na Enginia wa Kiwanda hicho Sivan Edayath mbali na kutoa taarifa kuwa kiwanda chao kimefungwa kutokana na kuishiwa Korosho za kubangua walisema kuwa wao hawana maamuzi yoyoyte juu ya ununuzi wa korosho hizo kutoka katika vyama vya ushirika vya msingi vya Wakulima wa Tunduru. 

Mwisho

No comments:

Post a Comment