Na Stephano Mango,Songea
WATENDAJI na viongozi wa Jumuiya ya Wanawake ya Chama cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma wametakiwa kuwahamasisha na kuwashirikisha kikamilifu wanachama wa Jumuiya hiyo iliwaweze kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama
Wito huo umetolewa jana na Katibu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania(Uwt) Mkoa wa Ruvuma Mariam Yussuf wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusu mchakato wa uchaguzi wa Jumuiya za Chama cha Mapinduzi
Yussuf alisema kuwa viongozi wa Uwt kupitia vikao halali vya Jumuiya wanapaswa kuwahamasisha wanachama kushiriki katika uchaguzi kwa kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwani wanawake wanaweza hata bila kuwezeshwa
Alisema kuwa wanachama wanatakiwa waendelee kuhudhuria vikao na mikutano inayowahusu ili kuweza kutumia haki stahiki ya kidemokrasia kwa kuomba kuchaguliwa au kuchagua viongozi bora watakaotuvusha wakati huu mgumu
Alieleza kuwa Jumuiya ya Uwt tayari imeshawatangazia wanachama wake utaratibu wa uchukuaji wa fomu za kugombea nafasi za uongozi kuanzia ngazi za matawi,kata,wilaya,mkoa na Taifa ili wale wenye sifa za uongozi waweze kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi
Alieleza zaidi kuwa wanaotaka uongozi ni vema wasifanye kampeni kabla ya wakati kwa kuanza kurushiana maneno machafu,kwa kutoa rushwa kwani kwa kufanya hivyo kutasababisha kuleta uadui na ustawi wa jamii na jumuiya ya Uwt na Ccm kwa ujumla hivyo tuepukane na vitendo hivyo
MWISHO
No comments:
Post a Comment