About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Friday, March 9, 2012

KAMATI YA KUCHUNGUZA MAUAJI MKOA WA RUVUMA KUWASILISHA RIPOTI YAKE HIVI KARIBUNI

MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU
Na Gideon Mwakanosya, Songea 
KAMATI huru ya kuchunguza vurugu zilizotokea katika Manispaa ya Songea February 22 mwaka huu ambazo zilisababisha vifo vya watu watatu vikiwemo vifo viwili vilivyotokana na kuuwawa kwa kutumia silaha za moto na Askari Polisi iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na kupewa kazi ya uchunguzi ndani ya siku saba inatarajia kukamilisha kazi hiyo ya uchunguzi mwanzoni mwa wiki ijayo badala ya jana siku ambayo ilipangwa kuikamilisha.
Akizungumza na mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com  jana ofisini kwake Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Saidi Mwambungu alisema kuwa ofisi yake mpaka sasa bado haijapokea taarifa ya kamati aliyoiunda  kufanya kazi ya uchunguzi wa kina zaidi kwa lengo la kubaini chanzo na sababu  iliyosababisha na kuwepo kwa vurugu hiyo.
Alieleza zaidi kuwa wakati kamati hiyo inaendelea kufanya kazi yake hali ya utulivu imekuwa ni nzuri na usalama umezidi kuimarishwa zaidi na kwamba kila kata imeweka mikakati ya ulinzi shirikishi ambao kila mkazi wa Manispaa ya Songea anapaswa kushiriki.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mwambungu alifafanua kuwa bado jitihada zinaendelea kufanywa kwa kukutana na viongozi mbalimbali wakiwemo wa mila na watu mashuhuri na wamedhehebu ya dini kwa lengo la kukemea uvumi na imani potofu zinazo sababisha uvunjifu wa amani katika maeneo mbalimbali kwa ustawi wa nchi na amesisitiza kila mwananchi awe na utii wa sheria badara ya kujichukulia sheria mkononi.
Amewataka wakazi wa Manispaa ya Songea kuwa makini katika shughuri zao za kila siku na badara yake waachane na uvumi ambao ndio ulio onekana umesababisha kuwepo kwa vurugu kubwa mjini Songea lakini kwa vile kamati ya uchunguzi ipo tuiachie indelee kufanya kazi.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Songea ambaye pia ni Kuu wa wilaya hiyo Thomas Ole Sabaya aliauambia mtandao huu wa www.stephanomango.blogspot.com kuwa tangu majuzi anaendelea kufanya ziara kwenye kata zote 21 kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kuweka ulinzi shirikishi kwenye maeneo wanayo ishi .
February 22 mwaka huu kulitokea mauaji ya watu wawili ambao inadaiwa waliuawa kwa kupigwa risasi na Askari Polisi na mwingine mmoja alikufa hapohapo  baada ya kutumbukia kwenye shimo wakati wananchi wenye hasara kufanya maandamano yaliyokuwa na vurugu ambayo yalilazimika yadhibitiwe na chombo cha dola.
Kufuatia kuwepo kwa hali hiyo Askari Polisi wanne walidaiwa kuhusika na mahuaji ya watu wawili walikamatwa na wanaendelea kuhojiwa na Polisi na watu 54 walitiwa mbaroni kwa kufanya maandamano bila kuwa kibali na kusababisha Manispaa ya Songea kutokuwa na amani.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment