About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Wednesday, March 14, 2012

WATATU WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA MAUAJI

Na,Augustino Chindiye Tunduru

WATU watatu wamefikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma kwa  tuhuma za kumuua kwa kukusudia marehemu Said Ally Kaunya.

Walioshitakiwa kwa tuhuma hizo katika Shauri hilo la mauaji namba 3/2012 ni Rajab Kalanje Namdoa (82), Asha Rajab (44) na Yasin Mohamed (52) ambao wamedaiwa kuwa  walifanya kosa hilo kwa kukusudia,

Akiwasomea shauri hilo Mwendesha mashtaka Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Asp Alfred Kasoro alisema kuwa kwa pamoja watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Machi 8 mwaka huu katika kijiji cha Nalwale kilichopo katika Kata ya Nandembo wilayani humo.

Kutokana na Shauri hili linalowa kabiliwa watuhumiwa hao kuwa nje ya uwezo wa kusikilizwa na mahakama hiyo,  watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote.

Hata hivyo  hakimu wa mahakama hiyo  Goefre Mhini aliwaamuru kwenda Lumande hadi Machi 26 mwaka huu wakati shauri hilo litakapo somwa tena.

Kwa mujibu wa Taarifa za tukio la mauaji hayo yalitokea kwa sababu ya kugombea mashamba katika kijiji cha Nalwale katika Kata ya Nandembo ambapo Mtuhumiwa namba moja  amedaiwa kufanya tukio hilo ili kumaliza ugomvi huo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo marehemu alidaiwa kuvamia shamba la mtuhumiwa namba moja nakuanza kulilima miaka 8 iliyopita ambapo katika kipindi chote hicho kesi ilikuwa ikiendelea katika hatua mbalimbali na kwamba kabla ya kifo hicho marehemu alikuwa ametoka kushinda kesi hiyo katika mahakama ya Ardhi ya Mkoa iliyopo katika manispaa ya Songea.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment