MKUU WA WILAYA YA TUNDURU JUMA MADAHA
Na Augustino Chindiye,Tunduru
ZAIDI ya Nyumba 300 zimeripotiwa kubomoka katika Tarafa ya Mlingoti Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma kufuatia mvua kubwa zinazo endelea kunyesha kwa takribani siku tatu sasa na kusababisha wakazi wa kaya hizo kukosa makazi.
Sambamba na tukio hilo pia. mvua hizo zimesababisha miundombinu ya barabara za kwenda vijijini kujifunga kutokana na maji kujaa kiasi cha kutishia kubomoka huku madaraja yakiwa hayapitiki kutokana na maji kufurika na maji kupita juu ya daraja .
Taarifa kutoka kwa madereva wanaofanya safari katika barabara kuu iendayo Songea zinasema kuwa maji yamejaa sana na kupita juu ya Daraja la Mto Masonya hali ambayo imesababisha magari yao kusitisha safari za kwenda na kuingia mjini Tunduru.
Adha nao madereva wanaofanya safari za kwenda katika vijiji vya Lukumbule,Mbesa Nalasi Mchoteka nako hakufai kutokana na maji katika mto Msinjewe kujaa sana na kutishia magari ya abiria kushindwa kupita huku taarifa kutoka katika Barabara iendeyo Masasi Mkoani Mtwara na Jijini Dar es salaam zikisema kuwa kikwazo kipo katika daraja la Mto Muhuwesi ambapo pia hapapitiki hali inayo onesha kuwa mji wa Tunduru hivi sasa upo kisiwani .
Akizungumzia maafa hayo Afisa Tarafa wa tarafa ya Milingoti Manfred kahobera Hyera mbali na kukiri kuwepo kwa wimba la maafa hayo alisema kuwa hali katika mji wa Tunduru ni mbaya sana kiasi cha kutishia maisha ya wakazi wake.
Akifafanua taarifa hiyo Hyera alisema kuwa hadi sasa amepokea taarifa kutoka kwa watendaji kata tatu za miji huo Nanjoka zimeripotiwa kubomoka nyumba 50, kata ya Masonya Nyuma 52 na majengo Nyuma 32 huku taarifa kutoka katika Tarafa ya Ligoma zikidai kuwa hali ni mbaya , chanzo cha matukio hayo kikidaiwa kuwa nyumba
hizo zilijengwa kwa tofari mbichi.
Juhudi za kupata taarifa za uharibifu ulisaabishwa na Mvua hiyo katika meneo mengine ya Wilaya hiyo zilishindikana kutokana na Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo Martin Mulwafu kudaiwa kuwa yupo katika safari ya kufuatilia taarifa hizo vijjini.
Mwisho

No comments:
Post a Comment