About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Saturday, September 17, 2011

DIWANI WA CHADEMA AWARUSHIA KOMBORA NZITO WABUNGE WA MKOA WA RUVUMA



Na Gideon Mwakanosya,Songea
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Mkoani Ruvuma kimewashushia shutuma nzito Wabunge wa Majimbo mbalimbali Mkoani Ruvuma,pamoja na wa Viti Maalumu kuwa wamekuwa ni mzigo kwa wananchi waliowachagua kwani wamekuwa wakishindwa kuwakilisha matatizo yaliyoko katika majimbo yao kikamilifu.
Akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara kwenye Kata mpya ya Mjimwema kwenye kiwanja cha eneo la Shule ya Msingi Samora Mwenyekiti wa chama hicho Mkoani Ruvuma Joseph Fuime alisema kuwa wabunge wa Mkoani wa Ruvuma wanapokwenda kuhudhuria vikao vya bunge wanashindwa kabisa kuwakilisha matatizo yaliyoko kwenye Manispaa ya Songea ambayo kwa muda mrefu kwa nyakati za usiku kunakuwa ni giza totoro lakini Mbunge wa Jimbo hilo amekaa kimya.
Fuime ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa CCM katika Manispaa ya Songea ameeleza kuwa wabunge wa majimbo yaliyoko Mkoani Ruvuma inaonyesha wazi kuwa wanapokwenda kwenye vikao vya bunge wanakimbilia posho na sio kwenda kama wawakilishi bungeni kama wanavyofanya wabunge wengine toka majimbo ya Mikoa mbalimbali.
“Wananchi niwaambieni Songea kumekuwa na matatizo mengi yakiwemo ya vocha za pembejeo zilizo chakachuliwa na wakubwa pamoja na tatizo Kubwa la kutopatikana umeme kwa muda mrefu katika mji wa Songea lakini tangu kikao cha bajeti ya bunge kilivyoanza mpaka kimeisha Mbunge wa jimbo hilo Dkt Emmanuel Nchimbi amekaa kimya kwa kisingizio cha kudai yeye ni Waziri” alisema Fuime.
Vilevile amewataadharisha Watanzania wakiwemo wananchi wa Moka wa Ruvuma kuwaogopa viongozi wachache wa Serikali ya Ccm ambao wamekuwa ni mafisadi wakubwa na wamegeuza Watanzania kuwa ni sehemu la shamba la bibi ambalo halina mwenyewe.
Amesema kuwa viongozi hao wamekuwa wakiuchezea uchumi wa nchi bila uoga na hakuna hatua zinazochukuliwa juu yao zaidi kumekuwepo na danganya toto kwa watanzania kuwa Serikali ya Ccm imeamua kupambana na mafisadi wakati mafisadi wenyewe wanaendelea kucheza kwenye shamba la bibi bila uoga.
Kwa upande wake Katibu wa Chadema jimbo la Songea Masumbuko Paulo ameeleza kuwa kwa kitendo alichokifanya Mbunge wa Jimbo la Mbinga Kapteni John Komba cha kuamua kumsaidia Mbunge wa Songea Mjini Dkt Nchimbi kumfikishia bungeni tatizo Kubwa la miundo mbinu mibovu katika Kituo kikuu cha mabasi Songea,kinastahili pongezi kwani hali halisi ya miundo mbinu ya Kituo hicho cha Mabasi ni mbaya lakini mwakilishi wa wakazi wa Songea mjini bungeni kwa kipindi chote cha bunge la bajeti alishindwa kabisa kuliweka wazi ili Serikali ijue ni namna gani kusaidia ukarabati kwenye Kituo hicho.
 MWISHO

No comments:

Post a Comment