About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Saturday, September 17, 2011

MAHAFARI YA KIDATO CHA NNE SHULE ZA WILAYANI TUNDURU YATUMIKA KUKUSANYA FEDHA YA KUBORESHA MIUNDOMBINU KATIKA SHULE ZILIZOPO MJINI HUMO

Na Steven Augustino,Tunduru

MAHAFARI ya kuwaaga wanafunzi wanaomaliza kidato cha Nne katika Shule za Sekondari za Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma yametumika kufanya harambee za kuchangisha fedha kutoka kwa wazazi na walezi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hizo ili ziweze kusaidia utengenezaji wa miundombinu mbalimbali .

Hali hiyo imetokana na Shule nyingi za Sekondari katika Wilaya hiyo kukabiliwa na uhaba mkubwa wa vifaa mbalimbali pamoja na kutokuwepo kwa miundombinu ya maji, uchakavu wa vyumba vya madarasa pamoja na upungufu wa thamani yakiwemo madawati, meza na viti vya kukalia wanafunzi.

Akizungumzia hali hiyo katika mahafari yaliyofanyika katika Shule za Sekondari za Masonya na Mataka afisa elimu wa Shule za Sekondari wa Wilaya ya Tunduru Mwl. Ally Mtamila alisema kuwa mpango huo umebuniwa kufuatia tabia za ukaidi na ugumu wa kuchangia maendeleo kupitia michango ambayo imekuwa ikiombwa na Shule kutoka kwa wazazi na walezi hao.    

Alisema baada ya kupatikana kwa fedha hizo zitasaidia kuanzia kutatua matatizo yanayozikabiri yakiwemo ya kujenga, kufanya ukarabati au kufanya malipo ya kuanzia kutengenezea vitanda kwa shule za Hostel au kununulia mbao ambazo zitatumika kutengenezea meza na madawati zikiwa ni juhudi za kupunguza adha mbali mbali zinazo ikabili idara hiyo wakati huohuo pia idara hiyo ikijitahidi kuomba uwezeshwaji kutoka halmashauri ya Wilaya hiyo.

Akizungumzia michango ya Shilingi 456,440 iliyopatikana kupitia harambe hiyo iliyofanyika katika Shule  za Sekondari zilizopo mjini Tunduru ambazo ni Frenkweston, Mataka na Masonya wakati wa mahafari hayo,  Mtamila alisema kuwa huo ni mwanzo mzuri na kwamba endapo utamaduni huo utaendelezwa kuna uwezekano wa Wilaya hiyo kupiga hatua kubwa za kimaendeleo katika nyanja hiyo  ya elemu.

 Aidha Mwl. Mtamila aliendelea kueleza kuwa idara yake yenye shule 19 inakabiriwa na upungufu wa walimu 130 kati ya mahitaji ya walimu 289  wengi wao wakiwa ni walimu wa masomo ya Sayansi hali inayotishia wanafunzi hao kufanya vibaya katika mitihani ya masomo hayo ambapo jumla ya wanafunzi 1200 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari mwaka huu.

Akiongea kwa nyakati tofauti wakati wa kufunga mahafari hayo  pamoja na mambo mengine Mwl. Ally  Mtamila aliwakumbusha wazazi na walezi wa wanafunzi waliomaliza darasa la saba kufanya maandalizi ili watoto wote watakao chaguliwa wajiunge kwa wakati na kuanza masomo ya sekondari.

Kuhusu wahitimu wa kidato cha Nne Mtamila aliwataka kufanya maandalizi mazuri ili waweze kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya taifa ili waweze kuendelea na masoma ya juu na kwamba wasikubali kudanganyika na maisha ya uraiani ambayo mwisho wake unaweza kufupisha maisha yao.

Awali wakisoma risala katika shule hizo kwa niaba ya wanafunzi wanaoagwa,Omari Jeuri wa Masonya Sekondari na Ayubu Adhuman wa Mataka sekondari walisema kuwa kukosekana kwa huduma ya maji katika shule zao kunatishia kulipuka kwa homa za matumbo ukiwemo ugunjwa wa kipindupindu.

Wakizungumzia madhara ya ukosefu wa Miundombinu ukosefu wa Walimu wa masomo ya sayansi, meza na viti vinavyo zikabili shule zao wakuu wa shule za Masonya Mwl. Mohamedi Ngaunje na Mkuu wa Shule ya sekondari ya Mataka Mwl. Johnes Liombo walidai kuwa endapo matatizo hayo yataachiliwa yaendelee kuna hatari ya idadi kubwa ya wanafunzi kuendelea kufanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya taifa na kuiweka Wilaya yao katika alama mbaya kila mwaka.

Mwisho.     

No comments:

Post a Comment