Na Stephano Mango ,Songea
Martina Nombo (27) mkazi wa kijiji cha Lulambo Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma amejifungua Mtoto wa kike ambaye anadaiwa kuwa na vichwa viwili ameomba msaada kwa watu wenye uwezo wamsaidie wakiwemo wataalam wa upasuaji wa Kichwa wamsaidie kuhokoa maisha ya Mwanaye.
Akizungumza na mtandao huu wa www.stephanomango.blogspot.com katika wodi namba tano ambapo amelazwa na Mwanaye huyo hospitali ya Mkoa wa Ruvuma jana mara baada ya kupata rufaa kutoka hospitali ya Mbuyula iliyopo Wilaya ya Mbinga
Mama wa Mtoto huyo amesema, alijifungua salama kwa njia ya kawaida mapema 9 juni mwaka huu katika hospitali ya Mbuyula ambapo mara baada ya kukabidhiwa mwanaye na wauguzi aligundua kuwepo kwa tatizo hilo na aliwaarifu nao walimweleza kuwa aendelee kuwa na subira.
Amesema, tangu alipojifungua katika hospitali ya Mbuyula kichwa cha mtoto waki kilizidi kukua na kutengeneza kitu kama uvimbe ambapo mtoto aliendelea kutibiwa hospitalini hapo hadi madaktari walipompatia rufaa ya kumwamishia katika hospitali ya mkoa jana kwa ajili ya matibabu zaidi.
Kwa upande Daktari Bingwa wa upasuaji wa hospitali hiyo Hassan Lumbe amesema, picha ya X-ray imeonyesha kuwa ndani ya kichwa kuna shimo ambalo linasababisha ubongo utoke na kuingia kwenye uvimbe ,pia mifupa ya kichwa aijajiunga vizuri.
Amesema,upasuaji wa mtoto huyo katika hospitali hiyo hauwezi kufanyika kutokana na kutokuwa na vifaa na utaalamu walionao hawakidhi viwango vya kutoa tiba kwa mtoto huyo hivyo wanamrufaa kwenda muhimbili .
Amesema,kesi kama hizo ni chache kuripotiwa katika Hospital hiyo na kwamba wao walimpokea baada ya kupewa rufaa toka katika hospitali aliyozaliwa ya Mbinga nao wanatarajia kumpatia rufaa kwenda hospitali ya taifa ya Mhubili kwani wamefanya vipimo na vimeonyesha kuwa opelesheni hiyo haiwezi kufanywa hapo na wanachofanya ni kuandaa rufaa pamoja na fedha kidogo ya kumsaidia kumsafirisha Mama huyo na Mwanaye.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment