Na Gideon Mwakanosya, Songea
WATU watatu wamefikishwa Mahakamani kwa kosa la kula njama na kutenda kosa la jinai la kufanya udanganyifu na kujipatia mkopo wa fedha toka katika Benki ya NMB tawi la Songea Mkoani Ruvuma .
Wakisomewa shitaka hilo jana na Hakimu mkazi Mfawidhi Mwandamizi Baptisti Mhelela amesema,washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo kati ya oktoba 22 mwaka 2008 na desemba 5 mwaka 2010 .
Amesema,katika kosa la pili mshitakiwa namba moja Cosmas Haule (35) anashitakiwa peke yake kwa kujipatia mkopo wa fedha shilingi milioni arobaini kwa udanganyifu kati ya kipindi hicho hicho cha oktoba 22 mwaka 2008 na 5 desemba 2010 na aliposomewa kosa alikana.
Amesema,mshitakiwa Cosmas yupo nje kwa dhamana na ametoa hati ya nyumba na dhamana ya mali isiyo hamishika yenye thamani ya shilingi milioni kumi pamoja na dhamana ya milioni 15 kesi hiyo inatarajiwa kutajwa septemba 30 mwaka huu,upelelezi bado haujakamilika.
Katika kosa la tatu,Mshitakiwa namba tatu Asha Banda (35) anashitakiwa kwa kosa la kujifanya mmiliki wa nyumba namba 22 kitalu L L Mateka B wakati ilikuwa siyo jambo la kweli na kubadili jina kuwa anaitwa Consolata Alphonce Soko .
Inadaiwa kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo kati ya tarehe hizo hizo oktoba 22 ,2008 na 5 desemba 2010 katika benki ya NMB tawi la Songea.
Mshitakiwa amekana shitaka na yupo nje kwa dhamana ya shilingi milioni tano ,na mshitakiwa namba 2 Onesmo Soko naye yupo nje kwa dhamana ya milioni tano.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment