About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Friday, December 9, 2011

REGIA MTEMA ATEMA CHECHE KWENYE MKUTANO WA HADHARA MJINI SONGEA

Mbunge wa Viti Maalum Chadema Regia Mtema akiwahutubia mamia ya wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma kwenye Viwanja vya Soko la Samaki la Zamani Mfaranyaki ambapo aliwataka wananchi kutambua umuhimu wa kudai Katiba Mpya kwa maendeleo ya Watanzania wote badala ya kuendelea kukabali ubakaji wa demokrasia unaoendelea kufanywa na Serikali katika harakati za mchakato wa kuandaa Mswada wa mabadiliko ya Katiba mpya 2011 uliosainiwa na Rais Kikwete hivi karibuni

Mtema alisema kuwa Katiba iliyopo imechoka na ndio imelifikisha Taifa hapa lilipo na kusababisha upatikanaji wa viongozi wabovu wenye kila aina ya uchafu ambao wamekuwa wakiwadharau wananchi wazi wazi na kuwatengenezea mazingira ya kuendelea kuwa maskini huku wao wakiishi peponi kwa kutumia kodi za wananchi

Alisema amewashangaa wabunge wa CCM kwa kitendo chao cha kuipuuza Katiba ambayo waliapa kuilinda kwa kuwanyima haki wananchi ya kujadili na kutoa maoni yao kuhusu Katiba Mpya ambayo inahitajika kwa ajili ya watanzania wote na sio ya Rais Kikwete na Chama chake

Amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wabunge wa Chadema kwa kuidai katiba mpya toka wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2011 hadi sasa wanapopinga sheria ya mabadiliko ya Katiba Mpya  yenye vipengele katili iliyopitishwa na Rais Kikwete hivi karibuni kwani vinamapungufu mengi ambayo yasiporekebishwa basi Katiba ijayo itakuwa mbovu kuliko iliopo sasa

Alisema kuwa Taifa linadai kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru ambao haueleweki katika vichwa vya watu na hauna mantiki yoyote kwani uhuru unaodaiwa wa miaka 50 ya Tanzania haupo kwasababu Tanganyika ilipata Uhuru Disemba 9,1961 ambapo Tanzania haikuwepo,sasa huo uhuru unaodaiwa upo wapi

Aliendelea kusema kuwa maadhimisho hayo yameghalimu mabilioni ya Shilingi kutokana na kodi za wananchi ambao wanaishi kwenye lindi la umaskini huku wakidhurumiwa haki zao na Serikali na kwamba amewataka wananchi kuipuuza Serikali ya CCM kwani ndio inayowamaliza watanzania kila siku

Alieleza kuwa Serikali inafanya sherehe hizo za uhuru hewa huku watanzania wanakufa kwa kukosa dawa katika vituo vya afya,wengine wanakufa kwa kukosa chakula,wengine kwa kupigwa mabumu na risasi na Serikali kwa lengo la kuwanyima haki muhimu za binadamu ikiwemo kujieleza,kupata malipo yao kutoka na kazi zao, kutaka maeneo ya kufanyia shughuli zao na mambo mengine kadha wa kadha


                Mamia ya wananchi wakisikiliza mkutano huo
 Wananchi wakiwa wamekaa juu ya kijiwe cha CCM huku wakiwa wamechoka wakisikiliza mapungufu ya Sheria ya kuandaa mchakato Katiba Mpya iliyosainiwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete kutoka kwa Mbunge Regia Mtema hayupo pichani
 Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma ,Diwani wa Kata ya Mjini na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa CCM Joseph Fuime (kulia) akiwa na Katibu wa Chadema Jimbo la Kawe Powel Mfinanga (kushoto)wakimsikiliza Mbunge Regia Mtema hayupo pichani
 Viongozi wa Chadema wakionyesha ishara ya kuichinja CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014 na uchaguzi Mkuu mwaka 2015,wa kwanza kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Songea na Diwani wa Kata ya Majengo Idd Abdalal,Katibu wa Chadema Mkoa wa Ruvuma Dorphin Ghazia,Katibu wa Jimbo la Kawe Powel Mfinanga,Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma na Diwani wa Kata ya Mjini na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa CCM Joseph Fuime,
 Mbunge wa Viti Maalum Chadema Regia Mtema akiendelea kutema cheche mjini Songea

 Katibu wa Jimbo la Kawe Powel Mfinanga akizungumza na mamia ya wananchi wa Songea katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho ambapo aliwataka wananchi kukiamini chama cha CHADEMA kwani ndio chama mbadala kitakachoweza kuwavusha wananchi toka hapa walipo kwenda mbali zaidi katika masuala ya jamii,miundombinu,afya,elimu,maji kwa kuzitumia vizuri rasilimali za taifa kwa maendeleo ya wote

Alisema CCM kwa kushirikiana na Rais Kikwete wameshindwa kuwafikisha watanzania kule waliko waahidi mara baada ya kushika dola mwaka 2005 na mwaka 2010 kwani akili zao zimefika mwisho wa kufikili na zimeganda na ndio maana hata wenyewe wametambua hilo kwa kuiga sera za CHADEMA na kushindwa kuzitekeleza kutokana na kuganda kwa akili zao

Alisema CCM haistahili kuendelea kuitawala Tanzania kutokana na kuwapeleka watanzania motoni kutokana na kusababisha gharama za maisha kupanda,thamani ya shilingi kushuka,kutokuwepo kwa elimu bora,miundombinu bora,huduma bora za maji,afya na mambo mengine

Alieleza zaidi kuwa Rais Kikwete amekuwa bingwa wa kutengeneza kashfa akiwa madaraka kwani yeye amekuwa Rais wa kwanza kupigwa mawe akiwa Mbeya,wa kwanza kudondoka jukwaani,wa kwanza kuwadanganya wananchi,wa kwanza kuvutwa mguu akiwa jukwaani na mtoto,wa kwanza kutukanwa na Uingereza,wa kwanza gari zake kuchakachuliwa mafuta,wa kwanza kukabidhi cheki ikiwa na maneno tofauti na talakimu,Rais wa kwanza kukabidhi gari kwenye halmashauri isiyostahili,wa kwanza kutoa ahadi nchi nzima akiwa kwenye Kampeni,wa kwanza kutumia fedha nyingi za Serikali kwa kusafiri nje,kufanya sherehe nyingi kwa kudi za watanzania,wa kwanza kusaini miswada ya gharama za uchaguzi na wa mabadiliko ya katiba mpya huku akijua mapungufu yaliyoko,wa kwanza kuwamwagia maji ya upupu wazee wa jumuiya ya Afrika Mashariki na wa kwanza kutoa matamko mengi yasiyo na utekelezaji,wa kwaza kwa kucheza kiduku kwa mbwembwe kwenye sherehe mbalimbali za Kitaifa na kijamii

"Rais ambaye kila kukicha anatengeneza rekodi mbaya za utendaji kama anavyofanya Kikwete astahili kuwa kiongozi hata wa familia yake kwani watoto wakishafahamu uwezo mdogo wa baba yao wa kiuongozi kamwe hawatamuheshimu,Urais ni taasisi nyeti kitaifa hivyo kuendelea kuwachagua watu walioganda akili watateketeza vizazi viliopo na vijavyo"alisema Mfinanga

Alisema kuwa Serikali ya Kikwete imedhihirisha kuganda kwa akili kwani kila mpango wanaoubuni ukiwemo wa ujenzi wa Sekondari za kata,kilimo kwanza imeferi licha ya kutumia fedha nyingi za wananchi na nguvu kazi,hivyo watanzania wanatakiwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano ya CHADEMA ili kujiandaa kuchukua nchi kwenye chaguzi zijazo


Katibu wa Jimbo la Kawe Powel Mfinanga akiendelea kuwashushia NONDO wananchi ili waweze kuanza harakati za kuiondoa CCM madarakani katika chaguzi zijazo kwa kutumia nguvu ya umma kwa ustawi wa Taifa la Tanzania ambalo limesimama kiuchumi,kiutamaduni,kijamii,kielimu,kiafya na huduma zingine muhimu

No comments:

Post a Comment