About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Wednesday, February 29, 2012

WAHUKUMIWA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA MIAKA 11 JERA

Na, Augustino Chindiye Tunduru

MAHAKAMA ya hakimu mkazi mfawidhi wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma imewahukumu watu wawili kutumikia kifungo cha miaka 11 jela baada ya
kupatikana na hatia katika matukio tofauti ya wizi.

Akitoa hukumu hizo kwa nyakati tofauti Hakimu wa Mahakama hiyo Geofrey Mhioni alisema kuwa anatoa adhabu hiyo baada ya Mahakama hiyo kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa walalamikaji.

Waliohukumiwa kutumikia adhabu hiyo ni Michael Lukas (31) aliyehukumiwa kutumikia  kifungo cha miaka 5 jela baada ya kupatikana na hatia katika  Shauli la Jinai Namba 119/2011 la tuhuma za wizi wa kuaminiwa kinyume na kifungu namba 273 (B) cha sheria.

Katika shauri hilo Lukas alikuwa anatuhumiwa kuiba Pikipiki yenye namba za usajiri T175 BQU mali ya Said Yasini ambaye alimuazima kwa madai ya kutaka kumpeleka mkewe katika hospitali ya Misheni ya
Mbesa kwa ajili ya kupatiwa matibabu na kwenda kuiuza kwa Shilingi 800.000 katika kijiji cha Londo Mkoani Lindi.

Akifafanua hukumu hiyo Mhini alisema kuwa katika kuonesha nia mbaya mtuhumiwa huyo pia alishirikiana na Mtu aliye muuzia na kufaniliwa kubadilishwa namba za usajiri wa pikipiki hiyo kuwa nmaba
T434 BEE .

Katika tukio la pili aliyehukumiwa na mahakama hiyo ni Salm haji (29) aliye kuwa anakabiliwa na shauli la Jinai namba 153/201 na kupatinana na  hatia katika makosa ya Kuvunja nyumba kinyume na Sheria namba 294
(2)cha kanuni ya adhabu  sura ya 16.ambapo alikiri kosa hili alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 6 jela na kosa la wizi kinyume na kifungu namba 265  pamoja na kifungu cha 258 cha kanuni ya adhabu kosa ambalo alihukumiwa kifungo cha miaka 5 jela na kuelezwa kuwa
adhabu zote zinaenda kwa pamoja.

Awali akiwasomea mashauri hayo Mwendesha mashtaka mkaguzi msaidizi wa Polisi ASP Alfred Kasolo alisema kuwa Mtuhumiwa Lukasi alifanya kosa
hilo Septemba 12/2011 huku mtuhumiwa wa shauli la jinai namba 153 /2011
Haji yeye alitenda kosa hilo Nov 12 2011 ambapo alivunja na kuiba
mali yenye thamani ya Shilingi 126,0000 katika nyumba ya  George
Komba.

Mbali na kutokuwa na kumbukumbu za  makosa ya nyuma kwa watuhumiwa hao
baada ya mahakama kuwatia hatiani ASP Kasolo aliiomba mahakama hiyo
kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia za
aina hiyo.

Wakitoa utetezi wao kabla ya kupewa kwa adhabu hiyo watuhumiwa hao kwa
nyakati tofauti Haji aliiomba mahakama hiyo impatia adhabu ndogo
kutokana na afya yake kusumbuliwa na kifua kikuu, huku mtuhumiwa Lukas
akiomba aonewe huruma kutokana na kusumbuliwa na vidonda vya tumbo.

Mwisho

Monday, February 27, 2012

MAFUNZO YA WAWEZESHAJI WA UJASIRIAMALI KANDA YAANZA KATIKA UKUMBI WA THE BEACH COMBER HOTEL JIJINI DAR ES SALAAM YAANZA ASUBUHI HII

 Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commission For Science And Technology DKT, Dugushilu Mafunda akiwakaribisha washiriki kutoka Tanzania Bara na Tanzania Visiwani katika ukumbi wa mafunzo wa The Beach Comber Hotel
 Mwasisi wa Kongano la Ujasiriamali Tanzania Profesa Burton Mwamila akimkaribisha mgeni rasmi ili aweze kufungua mafunzo hayo ya siku nne ambayo yanaanza Februari 27 hadi machi 1 mwaka huu
                        Washiriki wa mafunzo hayo wakiendelea na darasa


Washiriki wa Mafunzo ya Cluster Facilitator wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo

Sunday, February 26, 2012

CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA WA WAKULIMA WILAYA YA TUNDURU KIMEELEMEWA NA MZIGO WA MADENI

Na,Steven Augustino Tunduru

WAKATI Makampuni ya Wanunuzi wa Korosho Nchini wakiendele kutunishiana misuli na Serikali Chama Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Wilaya ya Tunduru (TAMCU) kimekiri kuelemewa na mzigo wa Madeni ya Wakulima yaliyotokana na Chama hicho kununua Korosho za Wakulima wa
zao hilo.

Hayo yameeelezwa na Meneja wa Chama hicho Imani Kalembo wakati akitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Madaha wakati wa kikao cha pamoja na Wadau wa Kilimo na viongozi wa Vyama vya Siasa .

Katika taarifa yake, Meneja huyo alifafanua kuwa hadi sasa chama hicho kupitia vyama vikuu vya Ushirika vya wakulima wa zao hilo kinadaiwa Jumla ya Shilingi Bilioni 2,441,870,350 .

Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa fedha hizo zimetokana na chama hicho kununua jumla ya Kilo 6,976,821 ambazo Chama hicho kupitia vyama vya msingi vimeweza kuzilipia kwa asilimia 70% pekee .

Alisema sambamba na Deni hilo pia Tamcu bado inakabiriwa na deni la Shilingi Milioni.608,260,000 zilizo tokana na Mkopo wa  kilo 506,855 za Korosho za zilizo kopeshwa na wakulima kwa vyama vya Msingi .

Kalembo aliendelea kueleza kuwa wakati hayo yakiendelea Chama hicho pia  kinakabiliwa na changamoto ya Chama kushindwa kununua jumla
ya kilo 86,324 zenye thamani ya Shilingi Milioni 17,264,800 ambazo bado zipo mikononi mwa wakulima wa zao hilo hali inayo endelea
kuwakatisha tamaa ya kuendelea na kilimo hicho.

Akizungumzia hali uzalishaji wa zao hilo katika Msinu wa mavuno wa
mwaka 2011/2012,Kalembo alisema kuwa Takwimu za manunuzi na Korosho
zilizopo mikononi mwa wakulima zinazonesha kuwa Jumla ya Kilo 7,570,000
zilizalimwa katika kipindi hicho.

Akizungumzia madhara yaliyo sababishwa na mgomo wa  Makampuni ya Wanunuzi zao hili Mkuu wa Wilaya hiyo Juma Madaha aliwataka wakulima kupitia wadau hao kuwa na uvumilivu wakati Serikali ikitafuta
suluhisho la kudumu la soko la mazao hayo.

Mwisho

MADEREVA YEBOYEBO WAMTEMEA NYONGO RC MWAMBUNGU RUVUMA

                              MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU
Na Kassian Nyandindi, Songea

MADEREVA wanaoendesha pikipiki maarufu kwa jina la 'yeboyebo' katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, wamemlalamikia mkuu wa mkoa huo Said Mwambungu wakisema kuwa chanzo cha machafuko na mauaji ya raia wawili waliopigwa risasi na askari polisi, yametokana na jeshi hilo kupuuza taarifa za uhalifu zilizokuwa zikitolewa na wakazi wa manispaa hiyo.

Malalamiko hayo yalitolewa na madereva hao kutokana na vifo vingi vinavyojitokeza katika manispaa hiyo wengi wanaouawa ni wao, walipokuwa wakizungumza katika kikao kilichoitishwa na mkuu wa mkoa huo kwa lengo la kujenga ushirikiano baina ya serikali na madereva hao ili machafuko yaliyotokea hivi karibuni yasiweze kuendelea.

Akichangia hoja katika kikao hicho mmoja kati ya madereva hao  Bonventura Njogopa, alisema kuwa mara nyingi askari polisi wapelelezi wamekuwa wakikaa vijiweni katika maeneo ya mjini na kuwafuatilia madereva hao kwa madai kwamba wanajihusisha na vitendo vya ujambazi wakati sio kweli badala yake walimweleza Bw. Mwambungu kuwa askari hao ni vyema muda mwingi wawe wanazunguka pembezoni mwa mji ambako mara nyingi wamekuwa wakijificha majambazi.

"Mheshimiwa mkuu wa mkoa askari wako wapelelezi wanatuambia sisi ndio chanzo cha kuwepo kwa majambazi, hii si kweli sisi ni raia wema tunachohitaji waache kukaa muda mwingi vijiweni hapa mjini badala yake wawe wanazunguka na sehemu zingine katika mji wetu wa songea ambako ndiko wahalifu wengi wanajificha", alisema Njogopa.

Naye Ali Omary alisema kwa muda mrefu polisi wamekuwa wakiwataka wao kama madereva wa pikipiki ambao huzunguka katika maeneo mbalimbali, kujenga ushirikiano na jeshi hilo kwa kutoa taarifa kwa njia ya simu au vinginevyo pale wanapobaini kuna dalili za uhalifu mahali fulani, lakini pamoja na wao kujitahidi kufanya mawasiliano na askari hao wamekuwa wakipuuzwa.

"Tunaiomba serikali yako hususani hawa polisi wakamate majambazi, lakini pia waache habari za kutuumiza sisi madereva wa pikipiki kwa kutupiga ovyo", alisema.

Pia walimweleza mkuu huyo wa mkoa kwamba askari wa usalama barabarani na polisi wa kawaida wote kwa pamoja wamekuwa wakijihusisha na ukamataji wa pikipiki jambo ambalo linawafanya washindwe kutambua nani hasa anapaswa kukagua vyombo hivyo vya moto.

Walielekeza malalamiko yao kwa mkuu wa usalama barabarani (RTO) mkoani Ruvuma  Sebastian Mtaki wakisema kuwa wanapotoa taarifa kwake, juu ya vitendo hivyo vinavyofanywa na askari wake hupuuzwa na hakuna hatua zinazochukuliwa.

"Utakuta pikipiki inakamatwa na kupelekwa kituoni, unapotakiwa kwenda kulipa faini ya makosa yako tunaambia tumfuate askari fulani kwenye baa fulani, je mkuu huu ndio utendaji halali wa kazi au ni ofisi zao binafsi", walihoji.

Kwa upande wake akijibu hoja hizo mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mwambungu alisema kimsingi atafuatilia malalamiko yao na kuyafanyia kazi haraka na kwamba aliwataka kuheshimu sheria na taratibu zilizowekwa ili kuepuka uwezekano wa uvunjifu wa amani kama ilivyojitokeza siku mbili zilizopita.

Hata hivyo aliongeza kuwa ofisi yake imekwisha unda tume ya watu nane ambayo itachunguza machafuko na mauaji ya raia yaliyojitokeza mjini Songea na kutoa majibu kwake kwa kippindi cha siku saba zijazo.

MWISHO.

Saturday, February 25, 2012

WAANDISHI WA HABARI MKOA WA RUVUMA KUENDELEA NA MAFUNZO YA UANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI

 Mwezeshaji wa Mafunzo ya uandishi wa habari za uchunguzi Fili Karashani
 Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Ruvuma Andrew Kuchonjoma akifuatilia mafunzo hayo ya siku tano yaliyoanza Februari 22 na kumalizika februari 27, yaliyofadhiriwa na Muungano wa Vyama vya Waandishi wa Habari Mikoani(UTPC) na kuhudhuria na waandishi 22
 Kutoka kushoto ni Alpius Mchucha (Habari leo), Christian Sikapundwa (Mhariri Tujifunze) Cresencia Kapinga (Majira) Joyce Joliga ( Mwananchi) Judith Lugome (Tujifunze)
 Christian Sikapundwa (Mhariri Tujifunze) Cresencia Kapinga (Majira)
 Joyce Joliga ( Mwananchi) Judith Lugome (Tujifunze)
 Kutoka kushoto Kassian Nyandindi (Majira) Thomas Lipuka (Jambo Leo) Ngaiyona Nkondora (Radio Free/Star Tv, Ngerangera
 Ngaiyona Nkondora (Radio Free/Star Tv na Jofrey Nilai (Radio Maria)
 Thomas Lipuka akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo
Kutoka kushoto ni Gerson Msigwa(TBC) Julius Konala (Tanzania Daima) Ngerangera Senior, Muhidin Amri (Majira) Jackline Claver (Radio Maria)

Thursday, February 23, 2012

ASKARI WANNE WAHOJIWA KWA KUSABABISHA MAUAJI YA WATU WATATU

 KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUVUMA MICHAEL KAMUHANDA
 ASKARI WAKITULIZA GHASIA JANA
Mmoja wa marehemu aliyeuawa kwa kupigwa risasi na Polisi

Na, Stephano Mango ,Songea

VURUGU zilizojitokeza wakati wa maandano ya amani ya wananchi wenye hasira kali katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma zimesababisha hasara kubwa ya mali zenye thamani ambayo haikufahamika mara moja na kwamba katika sakata hilo Askari  Polisi wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuwapiga risasi za moto watu wawili ambao wamefariki kwenye maandamano hayo

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda alisema kuwa hali ya mji kwa sasa hivi ni tulivu na hatua mbalimbali za kiusalama zinaendelea kuimarishwa ili wananchi waendelee na shughuli zao za kila siku

Kamuhanda alisema kuwa kwenye vurugu hizo watu 54 walikamatwa na wamefikishwa Mahakamani kujibu tuhuma za kufanya maandamano bila kibali na kusababisha uvunjifu wa amani katika maeneo mbalimbali ya mji wa Songea na vitongoji vyake

Alisema kuwa Askari Polisi waliohusika na kupiga risasi raia kwa sasa wanahojiwa na Jeshi hilo ili kupata uhalali wa kutumia risasi za moto katika tukio la maandamano yaliyofanyika jana na kwamba ikidhibitika kuwa walifanya uzembe watachukuliwa hatua za kisheria

Alieleza zaidi kuwa wananchi wakiwa kwenye maandamano hayo walivamia Ofisi za Chama cha Mapinduzi Manispaa ya Songea  na Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Vijijini walipiga mawe milango na kisha kuchoma bendera na kuleta hasara za mali nyingine za chama hicho, walivamia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Songea na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,walivamia  Ikulu ndogo walipiga mawe, walivamia Kituo cha Polisi na kupiga mawe na kuharibu baadhi ya magari ya wananchi

Alieleza kuwa waandamanaji walirusha mawe hovyo na kuwajeruhi wananchi wenzao, kufunga barabara kwa kutumia mawe makubwa, magogo na kuchoma mataili moto ili gari zinazoingia na kutoka nje ya mji zisiweze kuendelea na safari zake pia waandamanaji walivamia gari la Polisi na kuanza kurusha mawe na kusababisha Askari waanze kujihami kwa kurusha mabomu ya machozi

Alifafanua kuwa fujo hizo zinadaiwa kuwa zimetokana kwa sababu wananchi wamekuwa wakilalamikia matukio mfululizo wa mauaji mbalimbali likiwemo la mwendesha Pikipiki aliyeuawa februari 22 mwaka huu majira ya 2 asubuhi huko katika eneo la mto Matarawe, kuwa Jeshi la Polisi halichukui hatua ya kuwadhibiti wauaji hao

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Thomas Oley Sabaya alisema kuwa baada ya kutokea matukio hayo ameitisha viongozi wa Serikali za mitaa ya yote na kuwapa maagizo kuwa kuanzia sasa ulinzi shirikishi unatakiwa kuanza kwa kasi zaidi na kwamba kama kunawatu wanajihusisha na mambo ya uhalifu wajisalimishe haraka kwenye vyombo vya dola badala kusubiri wakamatwe

Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu amelaani kitendo kilichotokea juzi ambacho amesema sio cha kawaida hivyo kufuatia tukio hilo ameunda tume huru ya watu nane ambayo itafanya kazi ya siku saba ya kuchunguza kwa kina juu ya hali iliyojitokeza juzi mjini Songea na ripoti inapaswa kuwasilishwa arahamisi ijayo asubuhi ofisini kwake na kwamba hiyo tume inahusisha vyombo vyote vya dola

Baadhi ya wananchi wameiomba Serikali ichukue hatua za haraka kudhitibi hali iliyojitokeza juzi ambapo watu wawili waliuawa kwa kupigwa risasi na Polisi wakati wa wenye hasira kali walipokuwa wakipita mitaani kufanya vurugu huku wakidai kuwa Jeshi la Polisi limeshindwa kufanya kazi na mwingine kufa baada ya kutumbukia kwenye shimo na Pikipiki wakati wa vurugu hizo

 Wananchi hao ambao ni wakazi wa maeneo ya Mfaranyaki, Majengo, Bombambili na Mjini ambao wameomba majina yao yahifadhiwe walisema kuwa hali iliyojitokeza juzi haikuwa ya kawaida hivyo ni vyema Serikali ikatafuta njia muafaka ya kudhibiti chanzo cha vurugu badala ya kujishughulisha na kuzuia maandamano ya amani ya wananchi na kwamba thamani yake haikuweza kufahamika mara moja

MWISHO

MTOTO MCHANGA AOKOTWA NA MSAMALIA MWEMA AKILIA MSITUNI

Na,Steven Augustino,Tunduru

MTOTO mchanga anayekadiliwa kuwa na umri wa wiki moja au mbili kameokotwa baada ya kutelekezwa na mama yake mzazi na kukomea kusiko julikana

Taarifa kutoka kwa msamalia mwema aliyemuokota kichanga hicho Halima
Chalamanda alisema kuwa kabla ya tukio hilo alisikia Sauti ikitokea
katika vichaka vya Msitu uliokuwa kambi iliyofungwa ya Jeshi la Wananchi wa JWTZ wakati akielekea Shambani katika kijiji cha Namsalau.

Alisema kuwa baada ya kusikiliza kwa makini aligundua kuwa sauti ya kitoto
hicho ikitokea vichakani  hali iliyo msukuma kuingia katika msitu huo na kumkuta akiwa peke yake na kuamua kumchukua.

Chalamanda aliendelea kufafanua kuwa baada ya kumuokota mtoto huyo alichukua uamuzi wa kumpeleka katika Kituo kikuu cha Polisi kilichopo Mjini hapa na baadae akaelekezwa kumpeleka katika Hospitali ya Serikali ya Wilaya hiyo kwa ajili ya uchunguzi.

Akizungumzia hali ya  Mtoto huyo, Mganga wa Hospitali ya Serikali ya Wilaya hiyo Dkt. Goerge Chiwangu alisema kuwa hali ya mtoto huyo ilikuwa ni dhaifu sana lakini baada ya Msamalia huyo ambaye pia
analea Mtoto mchanga kumsaidia kwa kumnyonyesha Maziwa na kupatiwa hudumu za matibabu hali yake imeendelea kuimarika.

Alisema baada ya uchunguzi pia maafisa tabibu waligundua kuwepo kwa vidonda sehemu mbalimbali za mwili wake vilivyo sababishwa na  kukaa polini kwa muda mrefu hali iliyo wafanya wadudu kuanza kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake.

Dkt. Chiwangu alieendelea kueleza kuwa kutokana na mtoto huyo kukosa mtu ayemtambua ofisi yake kwa kusaidiana na idara ya Ustawi wa Jamii
Wilayani humo wanampango wa kumpeleka katika Kituo cha Kulelea Watoto
Yatima kilichopo katika Hospitali ya Missioni ya Mbesa ili alelewe
huko na Watoto wengine.

Wakiongea kwa nyakati tofauti Afisa ustawi wa jamii wa Wilaya hiyo
Alto Philipo na Mlezi wa Watoto yatima Katika Kituo cha Mbesa Mchungaji Ignas Nchimbi walisema kuwa hilo ni tukio la kwanza la mama kutupa mtoto mchanga Wilayani humo toka Kituo cha kulelea Watoto yatima kifunguliwe mwaka 1960.

Akizungumzia hali ya Watoto wanao lelewa katika kitu hicho Mchungaji Nchimbi alisema kuwa kituo hicho chenye Watoto 27, kichanga hicho kitakuwa cha 28 na kwamba hali ya kituo ni nzuri.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda mbali na kuthibitisha kuwepo kwa tukio hilo amesema kuwa jeshi hilo linaendelea na uchunguzi na kwamba sheria itafuta mkondo wake endapo mtuhumiwa atabainika.

Mwisho

Wednesday, February 22, 2012

SONGEA YAGEUKA UWANJA WA MAPAMBANO KATI YA POLISI NA WANANCHI


MADEREVA PIKIPIKI WAKIWA WAMEFUNGA BARABARA YA SONGEA KWEWNDA TUNDURU KARIBU NA MLANGO WA KUINGILIA OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUVUMA

Polisi wakiwatawanya na kuwakamata baadhi ya waandamanaji hao katika manispaa ya Songea baada ya wakazi wa manispaa hiyo wengi wao wakiwa madereva wa pikipiki kuandamana hadi ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma kupinga mauaji ya watu yanayoendelea kwa kasi mjini humo ambao hadi sasa jeshi la polisi halijafanikiwa kuwakamata wauaji.
 Polisi wakiwa katika mishemishe za kutuliza fujo na kujeruhi raia


Mama ambaye hakufahamika jina lake mara moja akiwa anaokotaa vipande vya taa ya gari yake baada ya kujeruhiwa katika vurugu hizo

Na Stephano Mango,Songea.

WATU watatu wamefariki dunia na idadi kubwa ya watu wanadaiwa kujeruhiwa kutokana na hali tete iliyozuka katika mji wa Songea mkoani Ruvuma, baada ya mamia ya wananchi na madereva wa pikipiki maarufu kwa jina la yeboyebo, kuandamana kuelekea kituo kikuu cha polisi na ofisi ya mkuu wa mkoa huo, wakipinga mauaji ya raia ambayo yameshamiri katika mji huo.
Kufuatia maandamano hayo kushika kasi katika mji huo, jeshi la polisi lililazimika kuingilia kati kwa kuanza kupiga mabomu ya machozi na risasi za moto hewani ikiwa ni lengo la kuwatawanya raia hao wasiendelee kuleta vurugu.  
Wakati mabomu na risasi hizo zikipigwa, ghasia za hapa na pale zilianza kujitokeza baadhi ya wananchi wakirusha mawe kuelekea kituo kikuu cha polisi na wengine wakipaza sauti wakielekeza lawama kwa jeshi hilo kwamba limeshindwa kudhibiti mauaji hayo.
Vurugu hizo zimesababisha ofisi za serikali na taasisi binafsi mkoani Ruvuma kufungwa kwa muda yakiwemo maduka na huduma za kifedha katika mabenki zimesimama kwa muda.
Huduma za usafiri katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani nazo zimesimama huku madereva wa mabasi na abiria wakikimbia kujificha kwa lengo la kuepukana na mabomu ya machozi na risasi za moto zilizokuwa zikipigwa hewani.
Pia huduma za matibabu katika hospitali ya mkoa huo nazo zimesimama kwa muda baada ya walinzi wa hospitali hiyo kufunga lango kuu kutokana na raia wengi walikuwa wakikimbilia huko wakiepukana na mabomu yaliyokuwa yakipigwa hewani.
Matukio ya mauaji katika mji wa songea yalianza kujitokeza mapema mwezi Novemba mwaka jana yakiendelea hadi sasa, ambapo kila baada ya siku kadhaa watu walikuwa wanauawa katika mazingira ya kutatanisha huku miili ya marehemu ikikutwa imejeruhiwa vibaya.
Watu tisa wameuawa katika mji huo tokea matukio ya mauaji yaanze kujitokeza katika mji wa Songea huku miili mingine ikiokotwa bila kuwa na sehemu za siri na kwamba watuhumiwa wanne wanaodaiwa kuhusika na mauaji hayo wanashikiliwa na polisi.
Watuhumiwa wanaoshikiliwa na jeshi la polisi ni Johari Kassim (16), Onesmo Hinju (14), Samason Haule (22) na Mussa Fuala (20) wote wakazi wa mtaa wa Lizaboni mjini Songea.
Pamoja na mambo mengine mpaka habari hizi zinaingia mitamboni Kamanda wa polisi mkoani Ruvuma hawakuweza kupatikana kuzungumzia sakata hilo huku simu zake zikiwa zimefungwa na askari polisi mjini hapa wakiendelea kupiga mabomu ya machozi, kwa lengo la kutawanya watu.
Uchunguzi uliofanywa na mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com umebaini kuwa vurugu hizo zimetokana na  wananchi hao kutokuwa na imani kwa Jeshi hilo kwa madai kwamba  halifanyi kazi yake ipasavyo katika kusaka majambazi na watu wengine wanaojihusisha na vitendo hivyo viovu badala yake nguvu kubwa wanaitumia katika kusaka na kukamata pikipiki zinazodaiwa kuwa na makosa
Vurugu hizo zilitokea jana baada ya wananchi hao wenye hasira kali kuona mauaji hayo yakizidi kuendelea siku hadi siku jambo ambalo liliwafanya waanze kufanya maandamano yenye lengo la kuilalamikia serikali kutokana na siku hiyo ya tukio kuokota mwili wa mtu mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni muendesha pikipiki akiwa ameuwawa na watu wasiofahamika hali iliyowafanya wananchi hao walifuatilie gari la Polisi ambalo lilifika kuchukua mwili wa marehemu huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika wakati wakiiupeleka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mkoa Songea ambako vurugu hizo zilianzia
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com  baadhi ya wananchi Mkoani humo wamedai kwamba tangu matukio haya yaanze kutokea Jeshi hilo halijachukua hatua ya kupita kila kata  kwa lengo la kutoa Elimu kwa wananchi hususani kwenye maeneo ambayo yamekumbwa na mkasa huo na kuongea na wananchi wake.
Akizungumza kwa njia ya simu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu alisema kuwa kitendo cha wananchi kuleta vurugu sio cha kushabikia hivyo aliwataka wananchi  kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo katika kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo hivyo viovu kwa kuwa watu hao wanaishi katika jamii na kudai kwamba Jeshi peke yake bila ya kupata ushirikiano toka kwa raia wema haliwezi kufanya kazi yake ipasavyo.

Monday, February 20, 2012

MCHIMBAJI WA MADINI YA VITO AFARIKI BAADA YA KUDONDOKEWA NA KIFUSI

Na, Augustino Chindiye Tunduru
MCHIMBAJI wa madini ya Vito katika eneo la machimbo yaliyopo Namba 8 katika Mto Muhuwesi Wilayani Tunduru Kessi  Mtolela ( Mpogolo)amefariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi cha udongo.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa marehemu aliangukiwa na kifusi hicho wakati akifuatilia madini hayo katika eneo hilo baada ya kuvutiwa na udongo ulio onekana kuingia kwa ndani ya kifusi hicho.

Walisema akiwa katika harakati hizo ghafla udongo uliokuwa juu yake ulikatika na kumuangukia kwa kumfunika mwili mzima na kupoteza maisha yake papo hapo.

Mganga kutoka katika Hospitali ya Serikali ya Wilaya ya Tunduru
Dkt.Jeshi Daraja aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu Mpogoro alisema kuwa kifo hicho kilitokana na mkandamizo mkubwa na udongo huo na kukosa hewa kwa muda mrefu.

Akizingumzia tukio hilo afisa madini makazi wa Wilaya hiyo
Fredriki Mwanjisi mbali na kukiri kuwepo kwake aliwatahadharisha
wachimbaji hao wadogo wadogo kufanya kazi zao kwa uangalifu ili
kujikinga na matukio ya aina hiyo ambayo yamekuwa yakisababisha vifo na vilema vya maisha.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael kamuhanda
alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi wa kifo hicho.

Mwisho

Sunday, February 19, 2012

MKUU WA MASOKO MANISPAA YA SONGEA SALUM HOMERA AONYA MWENENDO WA NCHI

MKUU WA MASOKO HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA SALUM HOMERA
Na Stephano Mango,Songea
SERIKALI imetakiwa kuona umuhimu wa kurudisha Azimio la Arusha ili kuweza kuwajengea watanzania pamoja na viongozi maadili ya uzalendo katika kuijenga Tanzania miaka 50 ya uhuru ijayo
Wito huo umetolewa jana na Mkuu wa Masoko wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Salum Homera ofisini kwake alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa
Homera alisema kuwa viongozi wengi wa sasa hawana maadili ya uongozi na wamekosa uzalendo wa kulitumikia taifa kwa moyo wote jambo ambalo linasababisha viongozi hao kushindwa kuwajibika ipasavyo katika ofisi za umma na mara nyingine kukumbwa na kashfa ya rushwa na ufisadi
Alisema kuwa kurudishwa kwa azimio la Arusha kutawafanya viongozi kufanya kazi kwa kufuata maadili na uzalendo wan chi kwa kuzitunza na kuzitumia rasilimali za nchi vizuri kwa faida ya watanzania wote na kuwasaidia watanzania kuwa na maendeleo mazuri
Alisema watanzania watakapo kuwa na maendeleo mazuri wataipenda nchi yao na viongozi wao kwani kwa pamoja watasaidiana kuijenga Tanzania yenye afya kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo
Alifafanua kuwa kila siku Serikali imekuwa ikishuka heshima yake kama mhimili muhimu wa uongozi kwa ujenzi wan chi makini kutokana na kukiukwa kwa misingi imara ya Azimio la Arusha na kwamba kutokurirudisha kutaendelea kushusha heshima ya Serikali na viongozi wake
Alisema kuwa kwa hali ya nchi ya sasa, ni muhimu vijana wanaomaliza kidato cha nne wakaenda kupata mafunzo mbalimbali ya ukakamavu na ya uzalendo kwa nchi yao katika Jeshi la Kujenga Taifa JKT, jambo ambalo litapunguza migomo katika vyuo vikuu kwa sababu watakuwa wamepata mafunzo ya uzalendo na hivyo kuwafanya kuwa na utaifa mbele badala ya kuwa na maslahi binafsi
Alisema kuwa kwa kufanya hivyo watanzania watakapo kuwa kwenye maeneo yao ya kazi watazingatia utaifa kwani hata wafanyabiashara watashindwa kujipangia wao bei za bidhaa kiholela na kuwafanya watanzania wanyonge wapate tabu katika maisha au kuiraumu Serikali kuwa imeshindwa kuzuia mfumuko wa bei holela
Alieleza zaidi kuwa uchakachuaji wa fedha nyingi za umma katika miradi ya wananchi kunatokana na wasimamizi wa fedha hizo kutokuwa na uzalendo stahiki wa kuijenga nchi yao hivyo kwa kupitia JKT hali hiyo inaweza ikapungua na hatimaye kwisha kabisa ustawi wa nchi yetu
MWISHO
 

KAPTENI KOMBA NA FALSAFA YA PALIPO NA MAJI YA UZIMA NAPAJUA KWA WAKOVU WA NYASA

 
 Rais Jakaya Kikwete akiwa na Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi Kapteni John Komba alipotembelea jimbo hilo
Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi,Kapteni John Komba akifungua Zahanati ya Tumbi, wa kwanza kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Mbinga Anastia Amasy

Na Stephano Mango,Nyasa
KILA Kiongozi katika jamii anayo majukumu yake ya msingi ambayo anapaswa  kuyatekeleza katika jamii husika kwa muda muafaka ambapo kwa upande wa vyama vya siasa wapo wale wa nyadhifa za uwakilishi ambao ni Madiwani, Wabunge, na Rais ambapo uwepo wao hutokana na Wananchi kuwachagua kupitia masanduku ya kura
Wawakilishi hao wana majukumu mengi ambayo kimsingi yameainishwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na ilani za uchaguzi za vyama vyao ambapo wakati wa kampeni walizinadi ilani hizo kwa nguvu kubwa.
Ambazo kimsingi zinapaswa kutekelezwa kwa viwango vilivyoahidiwa wakati wa kuomba ridhaa ya uwakilishi dhidi ya wananchi kwenye vyombo vya maamuzi.
Kwa sababu dhamana ya viongozi katika nchi mbalimbali duniani ni kuharakisha maendeleo katika jamii kwa kushirikiana na wananchi husika kwa lengo la kutatua kero zao kwa wakati ili kufikia malengo yanayokusudiwa na jamii husika.
Ni dhahiri kuwa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuna baadhi ya Wabunge wamefanya na wanaendelea kufanya juhudi kubwa ya kuhakikisha na wengine wamekuwa wakijikita na shughuli zao katika miji mikubwa na kusahau wapiga kura wao.
Wapo wabunge wengine wanafuatilia, na kusimamia utekelezaji wa ilani ya chama chao ambayo wao waliinadi kikamilifu kwa wapiga kura wakati wa Kampeni Mwaka 2010 lakini wengine toka wamepata ridhaa ya uwakilishi wamekuwa bize na mambo yao
Miongoni mwa Majimbo ya uchaguzi Nchini ambayo wapiga kura walipewa ahadi nyingi za kuletewa ustawi katika sekta za barabara, afya, elimu, mawasiliano, na uwezeshwaji kiuchumi ni Jimbo la Mbinga Magharibi ambalo ni miongoni mwa Majimbo saba ya Uchaguzi yaliyopo Mkoani Ruvuma.
Jimbo hilo ambalo limetangazwa hivi karibuni kuwa Wilaya ya Nyasa linawakilishwa na Mbunge Kapteni Mstaafu John Damian Komba ambaye wapiga kura wake wanamuita Mbunge wa Muyaya.
Hivi karibuni niliambatana na Mbunge Kapteni John Komba kutembelea Jimbo hilo ambalo kwa sasa lina jumla ya kata 15 ambazo ni Lundo, Luhangarasi, Liundi, Liparamba, Mtipwili, Lipingo, Lituhi, Mbambabay, Kilosa, Liuli, Kingilikiti, Chiwanda, Ngumbo, Tingi na Kihagara.
Ziara hiyo ya Kapteni Komba ilianzia kwenye Kata ya Lituhi ambapo alifungua Mashindano ya soka kombe la Kapteni Komba, mashindano ambayo yamefadhiriwa nay eye mwenyewe kwa gharama ya shilingi milioni 5
Ambazo zimegawanyika katika manunuzi ya jezi za timu 11 ambazo zinashiriki mashindano hayo, jezi seti tatu za waamuzi, mipira 2 ya mashindano, miamba ya chuma kwa ajili ya magoli, gharama za kutengeneza kombe
Katika mashindano hayo ambayo mshindi wa kwanza atapata zawadi ya shilingi 150,000/= na kombe, wa pili shilingi 100,000/=, wa tatu shilingi 50,000/= ambapo kwa timu 7 zilizobaki watapata kifuta jasho cha shilingi 20,000/= kwa kila timu
Pia alitembelea kata ya Ngumbo na kutoa msaada wa vitanda, mito, shuka, chandarua na magodoro  wenye thamani ya shilingi 3 milioni kwenye kituo cha Afya Mkili na Zahanati ya Kijiji cha Mbuli ili kuondokana na tatizo la wagonjwa kulala chini kwa kutumia mikeka
Akitoa misaada hiyo kwenye viwanja vya Kituo cha Afya Mkili Komba alisema kuwa kwa muda mrefu nilikuwa nafahamu kero ya wananchi wa maeneo hayo kuwa ni afya, maji, barabara, elimu na mawasiliano lakini kwa miaka mitano iliyopita nilichagua kushughulikia suala la elimu ,mawasiliano na barabara ambapo kwa sasa nashughulikia afya na maji
“Natambua matatizo yaliyopo kwenye sekta ya afya katika Jimbo la Mbinga Maghalibi hivyo kwa kuanzia natoa msaada wa shuka 24, magodoro 14, vyandarua 14, mito 14, vitanda 14 kwa ajili ya kituo cha afya cha Mkili na pia Vitanda 6, shuka 12, magodoro 6, Vyandalua 6, mito 6, na mzani wa kupimia watoto na wajawazito 1 kwenye Zahanati ya Kijiji cha Mbuli”alisema Komba
Komba alisema kuwa vituo vya afya na Zahanati karibu zote katika Wilaya hiyo hazina wataalamu,Vifaa Tiba na usafiri wa wagonjwa lakini tatizo hilo limeanza kushughulikiwa kwa kasi kubwa na nguvu zaidi kwa kuanzia kutoa vitu hivyo
Alisema kuwa natambua kuwa wananchi wamelalamikia kwa muda mrefu matatizo hayo hasa ya ukosefu wa vitanda na shuka kwani wanapotakiwa kulazwa hulazimika kutafuta mikeka na vitenge kwa ajili ya kujifunika wakati wa kulala huku wakipata mwanga wa vibatali kutokana na kukosa umeme
Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo Emmanuel Nchimbi akipokea msaada huo alisema kuwa kwa muda mrefu kituo hicho kilikuwa kinakabiliwa na matatizo hayo hivyo kwa msaada huo wananchi wanaopata huduma za matibabu watakuwa wameondokana na matatizo yaliyokuwa sugu katika kituo hicho
Naye Mganga wa Kituo hicho cha Afya Thomas Magulilo alieleza kuwa kituo chake cha afya kwa sasa kinakabiliwa na tatizo la watumishi wa kada ya afya,usafiri kwa wagonjwa na ukosefu wa maji kwani wagonjwa wamekuwa wakichota maji Ziwa nyasa na kuyatumia kwa kunywa,kuoga na shughuli zingine na kusababisha kuongezeka kwa magonjwa ya matumbo
Magulilo alisema kuwa kituo hicho kinahudumia wagonjwa kutoka Vijiji vya Yola,Luhundi,Ndonga na Mkili na wengine kutoka maeneo jilani hivyo kituo kimekuwa kikitoa huduma kwa wagonjwa wengi kuliko uwezo wake kwani vifaa tiba vipo vichache,wataalamu wa kada ya afya wapo wachache na kusababisha huduma inayotolewa kuwa duni
Alisema kuwa magonjwa sugu yanayosumbua wananchi wa maeneo hayo kuwa ni Malaria,upungufu wa damu,Minyoo,magonjwa yatokanayo na hali ya hewa, kuhala na kutapika pamoja na ugonjwa hatari wa ukimwi
Akiwa Kata ya Mbaha Mbunge huyo aliwapa pole wahanga wa kimbunga kwa kuwapa msaada wa bati 500 zenye thamani ya shilingi 7.5 milioni kwa waathirika 30 wa kata ya Mbaha ambao nyumba zao ziliezuliwa na mvua iliyoambatana na upepo mkali mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka huu na kusababisha harasa mbalimbali za mali
Diwani wa Kata ya Mbaha Stewat Nombo alimshukuru Mbunge huyo kwa msaada wake alio utoa kwa wananchi walio athirika na mvua hizo na kusema pia waathirika walipokea msaada wa maguni ya mahindi kutoka serikali ya wilaya ya mbinga. mbazo wanataka Mbunge wao kupitia serikali na wahisani wazitafutie ufumbuzi ili nao waweze kujivunia maendeleo yao.
Nombo amewaomba watu wengine wenye mapenzi mema kuwa tayari katika kuwasaidia watu mbalimbali wanao patwa na matatizo au majanga  pindi yanapo jitokeza kwa kuwa kuna baadhi ya kaya hukosa chakula na makazi ya kuishi
 
Wakazi wa Jimbo hilo kama  walivyo wapiga kura wa majimbo mengine nchini, wanamatumaini ya utatuzi wa kero zao kutoka kwa Mbunge wao kufuatia kuwepo kwa baadhi ya mafanikio kwenye sekta mbalimbali kutokana na juhudi anazozifanya.
Licha ya matumaini waliyonayo na maendeleo yaliyokwisha patikana baaadhi ya wananchi wamepaza sauti zao kuhusu baadhi ya kero zinazowasumbua a
Mkazi wa Kata ya Lituhi Chogo Wachogo anasema kuwa maji yapo ya kutosha kwenye kata yao ila tatizo linalowasumbua ni miundo mbinu ya kusambazia mtandao wa maji hayo.
Wachogo alisema pia barabara zinapitika vizuri kwa wakati wote tofauti na miaka ya nyuma, hata hivyo amemwomba Mbunge wao ashughulikie suala Usafiri wa uhakika ili wanunuzi wa Samaki na dagaa kutoka Ziwa Nyasa waweze kupata usafiri wa uhakika wa bidhaa zao kuelekea katika masoko.
Kwa upande wa mawasiliano Katibu wa CCM Wilaya ya Mbinga Anastasia Amasy anasema katika kata nyingi za Jimbo hilo kuna  mawasiliano ya simu ila katika kata  za Chiwanda, Ngumbo ambazo zipo kwenye mchakato wa kujenga minara katika maeneo hayo na ujenzi unaendelea ili wananchi wapate mawasiliano ya uhakika.
Amasy anasema kupatikana kwa wilaya mpya ya Nyasa kutatatua kero nyingi za wananchi katika sekta zote na kusema kuwa wananchi hao wanapaswa kufanya kazi zao kwa bidii kwa lengo la kuijenga wilaya hiyo mpya katika nyanja zote muhimu
Wakati wakilalamikia kero hizo kwa upande wao, wakazi wa Jimbo hilo wamepongeza juhudi zinazofanywa na Mbunge huyo za kupambana kwa dhati dhidi ya masuala yanayoonekana kuwa ni kikwazo kwao na kuelezea jinsi sekta za Barabara, Afya, Maji, Elimu, Mawasiliano zilivyopiga hatua kwa kiwango kikubwa.
Kwa nyakati tofauti walisema kuwa toka Dunia iumbwe hawajawahai kumpata Mbunge anayewajali na kuwathamini kwa kusaidiana naye kuleta maendeleo kwa wananchi ambaye kwa muda wote anakuwa jimboni na wananchi wake ama kweli Kapteni Komba anapaswa kuwa "Mbunge wa Muyaya" yaani Mbunge wa milele
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Kanali Mstaafu Edmund Mjengwa alisema Kapteni Komba amejitahidi sana kutatua kero za wananchi wake hivyo anapaswa kupongezwa sana kwa juhudi zake alizozionyesha katika kipindi cha uwakilishi wake wa miaka sita hii
Mjengwa alisema katika kipindi hicho Kapteni komba amefanikiwa kuwaletea wilaya mpya ya Nyasa ambayo ndio itakayokuwa nguzo muhimu katika kuimarisha sekta za uchumi, mawasiliano, barabara, elimu, afya na maisha bora kwa wananchi wa wilaya hiyo ambao shughuli zao kubwa ni kilimo cha kahawa, mihogo, mahindi, ulezi na uvuzi wa samaki na dagaa kutoka ziwa nyasa
Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi wa jimbo hilo la Mbinga Magharibi waipokee kwa shangwe wilaya hiyo mpya ambayo inafaida kubwa sana kwao na kuwataka waongeze bidii katika kilimo,uvuvi na kutenga maeneo ya uwekezaji na uzalishaji mali ili waweze kufaidi matunda ya wilaya yao mpya
Hata hivyo akijibu kero zilizoainishwa na wapiga kura wake kwenye Mkutano wa Kata ya Kilosa, Mbunge wa jimbo hilo Kapteni Komba amesema katika kipindi cha miaka mitano ya uwakilishi wake nimejitahidi kutekeleza ahadi muhimu nilizowaahidi ambazo zilikuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo na kero kubwa kwa wakazi wa Jimbo hilo.
Anasema wananchi wa jimbo hilo walimchagua na kumpa dhamana ya kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wakijua kuwa yalipo maji ya uzima napajua, hivyo pamoja na kuwaletea huduma muhimu kama Maji, Barabara, Afya, Elimu, Kufufua mazao ya biashara kama Kahawa, Korosho na kuwatafutia masoko ya uhakika,nilijitahidi kutekeleza ahadi zangu kwa 90% kwa kipindi changu cha miaka mitano iliyopita 2005/2010 
Kwa upande wa mawasiliano ya simu na miundombinu ya maji barabara kwa baadhi ya maeneo amewaomba wapiga kura wake wavute subira kwani tayari utekelezaji wake upo kwenye mchakato ingawa amesema upatikanaji wa Wilaya mpya ya Nyasa ambayo imetangazwa rasmi utachochea kasi ya maendeleo katika jimbo lake
Komba anasema amejitahidi sana kutatua kero za wananchi wake katika kipicha cha uwakilishi wake na anaishukuru serikali ya awamu ya nne kwa kusikiliza kilio chake cha kupatiwa wilaya hiyo mpya kwani sasa maendeleo ya wanambinga magharibi yatakuwa makubwa kwani nao watafaidika na bajeti ya Serikali kama wilaya zingine
Aidha amewaomba wapiga kura wake wawe na ushirikiano stahiki katika kutatua kero zilizopo ili kuweza kufikia lengo la maisha bora kwa kila mtanzania ingawa amewata kuipokea Wilaya yao Mpya ya Nyasa ambayo makao makuu wanatarajiwa yawe Mbambabay.
“Naomba wapiga kura wangu watambue kuwa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita nguvu nyingi nilielekeza kwenye ujenzi wa shule za msingi na sekondari, pamoja na miundo mbinu ya barabara, maji na mawasiliano na mwaka huu namalizia ahadi zangu muhimu katika sekta ya afya ili niweze kufanya tathimini ya miaka saba ya uwakilishi wangu” alisema Komba.
Hata hivyo anasema mafanikio ya mwanasiasa yoyote yule ni kutekeleza ahadi alizo ziahidi kwa wananchi wake kwa wakati stahiki, hivyo ahadi zote alizozitoa ametekeleza kwa ukamilifu kwa sababu yeye sie Mbunge wa uwongo bali wa kweli kwa hiyo hapendi wananchi wake walalamike kwa sababu yeye hakuomba ubunge wa malalamiko bali ni wa utekelezaji kwa yale aliyoyaahidi na kwasababu yalipo maji ya uzima napajua mie kazi yangu nikuyashusha kwa wapiga kura wangu ili waweze kufaidi matunda ya uhuru wa Tanganyika 
Mwandishi wa Makala haya
Anapatikana 0755 33 5051

Saturday, February 18, 2012

SERIKALI YATAKIWA KUDHIBITI UBABAISHAJI WA MAKAMPUNI YA SIMU

Na Augustino Chindiye, Tunduru

SERIKALI kupitia mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imeombwa kuyachukulia hatua za kisheria makampuni yanayotoa huduma za mawasiliano nchini yanayo wayumbisha wateja wake kwa kudai imewawekea fedha kwenye akaunti maalum wakati inawadanganya.

Ombi hilo limetolewa jana na wateja wa makampuni hayo kwa nyakati tofauti kufuatia kuwepo kwa wimbi kubwa la watumiaji wa mitandao hapa nchini kukumbwa na kiwewe cha kila mtumiaji wa mtandao wa simu za mikoni kujikuta wakiwa wameingiziwa kitita cha fedha wanazoshindwa kuzihamisha na kuzitumia.

Fedha hizo zinazodaiwa kumwangwa katika Simu hizo ili zikae hewani na watu wanaodhani kuwa ni “Mafisadi” zimeingizwa kwa watumiaji wa mitandao yote nchini na kuzificha katika akaunti iliyopewa jina la future banking MBanking ambapo kila mtumiaji wa Simu ameingiziwa
Shilingi 800,000 /= kwa kila mtandao wa simu anaoutumia.

Hamis Seleman alisema kuwa pamoja na fedha hizo kinachowachanganya watumiaji wa mitandao hiyo mbali na fedha hizo kuonekana kuingizwa katika Simu zao ni fedha hizo
kutowezekana kwa kutolewa kwa njia yoyote kutokana na kuwekwa namba ya siri ( PIN )  hali iliyosababisha mlundikano wa watu kutoa vijijini kuja mijini ili kuona uwezekano wa kutoa fedha hizo ili wazitumie.

Seleman alisema kuwa kwa mujibu wa maelekezo watumiaji waliovumbua fedha hizo ziliko
fichwa, mtumiaji wa simu ya mtandao wowote anatakiwa kubonyeza alama ya *150*55# na kubonyeza alama ya Ok ili kuituma katika mtandao anaoutumia atapata ujumbe unao mwelekeza kuwa kuingia katika akaunti hiyo na kadili utakavyo endelea utapata ujumbe unao kueleza kuwa umeingiziwa kiasi hicho.

Wakati hayo yakiendelea baadhi ya makampuni ya simu hapa nchini yamekuwa yakituma ujumbe unao watahadharisha wateja wake kuwa hayata husika na utapeli wowote wa kifedha utakaofanyika kutoka na wateja wao kutumiwa Meseji hali inayoonesha kuwa huenda wamiliki wa mitandao hiyo wamezidiwa nguvu na watu hao wanaoingilia mitandao ya simu zao.

Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya Mawakala wa M-pesa, Airtel money na Tigo pesa walikiri kupata usumbufu mkubwa kutoka kwa wateja hao ambao kila mtumiaji wa simu kwa muda sasa wamekuwa wakienda kuomba kutolewa fedha hizo.

Mwisho.

Friday, February 17, 2012

MAKUMBUSHO NI KIINI CHA MAENDELEO NA USTAWI WA WATANZANIA

 Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Songea yanavyoonekana
                                          Fratel John Kassembo
Na Stephano Mango,Songea
WATANZANIA tunapaswa kufahamu umuhimu wa Makumbusho ili tujenge utamaduni wa kuyatembelea mara kwa mara tuone na kujifunza mambo ya kale ili kuona jamii zao zilivyokuwa zinaishi kwa muingiliano wenye kujenga jamii imara
Makumbusho ni sehemu ambayo watu wanaweza kujifunza namna ya uhifadhi bora wa mazingira kwa kuangalia watu wa kale walivyoweza kunufaika na mazingira yaliyowazunguka na mali asili zilizokuwepo kwa kupata dawa za miti shamba,chakula na vitoweo
Kupitia Makumbusho wananchi wanaweza kujifunza wajibu wao kwa nchi yao na jamii nzima inayowazunguka kwa kuangalia Mashujaa wa kale waliojitoa kwa moyo kupigana kwa ajili ya uhuru wan chi,ulinzi na usalama wa mali zao
Uwepo wa Makumbusho ni jambo la kujivunia kwani yanaweza kutumika kujenga amani katika jamii ya watu wanaoishi kama ndugu na marafiki kwa kuangalia maisha ya watu wa kale walivyoishi kwa kushirikiana katika mambo yaliyokuwa yanawahusu wao na jamaa zao
Pia ni sehemu ambayo huwakutanisha watu wa mataifa mbalimbali wanaokuja kuzitembelea na kujifunza historian a tamaduni zetu hivyo kuifanya dunia kuwa mahali padogo kwani vitu wanavyojifunza hupelekwa nchi za mbali na kujulikana kwa watu wa mataifa mbalimbali
Nakufanya kuwa kiungo cha mabadiliko na maendeleo ya Taifa kwani kupitia Makumbusho watu wanaweza kujifunza umuhimu wa mabadiliko na umuhimu wa kila mmoja kujiletea maendeleo kwa kuangalia namna mwanadamu alivyopitia hatua mbalimbali za mabadiliko mpaka kufikia hatua tuliyopo hivi sasa
Kukuza amani na kuchangia kwa ufanisi zaidi katika kujenga amani Dunia,  Makumbusho yanaweza kuandaa midahalo, kuonesha filamu, jitihada za utafiti, matembezi, mikutano ya amani na maonyesho ya utalii
Ni sehemu ambayo huvuta watalii,hukuza sayansi,hushangaza/kustaajabisha,kuelimisha,kuburudisha na hutia chachu ya uwajibikaji kwani ndani yake yana kumbukumbu zilizohifadhiwa hivyo makumbusho ni historia inayoishi
Akizungumzia umuhimu wa Makumbusho ,Mwezeshaji na mtoa mada wa mambo ya uongozi, dini, vijana, falsafa, ujasiriamali na amali za maisha John Kasembo alisema kuwa kumbukumbu ni wasaa wa kutafakari sisi wenyewe maisha yetu hivyo tunapaswa kuweka juhudi za kutunza makumbusho zetu
Kasembo alisema kuwa suala la kutunza Makumbusho ni tete kulibinafsisha kwani linabeba utamaduni na utambulisho wa Taifa au jamii husika, hivyo zinawezwa kutunzwa na mtu binafsi kwa maendeleo yake, taasisi au Taifa
Alisema kuwa mchango wa Tanzania kwenye tamaduni za nchi za Ulaya haupo  na haujulikani , ingawa kila siku tunaendelea kutothamini utamaduni wetu kwa kuendelea kuiga tamaduni za nje bila sababu za msingi
Alieleza kuwa utamaduni wa Tanzania unastahili kukuzwa,kutangazwa na kusimamia ili nasi tuweze kuchangia utamaduni wetu kwenye mataifa mengine na ustaarabu wa ulimwengu, hivyo utambulisho binafsi na wa pamoja, kati ya kumbukumbu na historia
Alieleza zaidi kuwa Makumbusho ni benki ya kumbukumbu licha ya kuwa sehemu ya kuelimisha na kuburudisha, pia makumbusho ni kumbukumbu ya fikra,  kazi,maisha,mtazamo wa matukio na watu
“Waafrika wengi hatuna utamaduni na hatujalelewa, uvivu, malezi, elimu, ndio gharama za kutunza kumbukumbu binafsi na ndilo hata tatizo linaloikumba Taifa, jambo ambalo linapaswa kurekebishwa”alisema Kasembo
Alieleza kuwa wadau wa utamaduni na wataalamu wa makumbusho wanahitajika kukutana na watu ili kuweza kuelezea maana na kutetea nafasi ya makumbusho kwasababu makumbusho zipo kwenye moyo wa mfumo, taasisi zinazohudumia na kuendeleza jamii
Alieleza kuwa ni njia muhimu ya kubadilishana utamaduni,kutajirishana tamaduni, kustaajabia tamaduni na maendeleo ya maelewano ya pamoja, ushirikiano na amani kati ya watu kwani yana kumbukumbu muhimu kwa jamii na zaidi ni chachu ya maendeleo ya jamii
Alifafanua kuwa akumbusho yanakusanya vitu vyenye umuhimu wa kisayansi,kijamii na kihistoria ili kutunza, kusoma, kutafsiri mambo mbalimbali ili kizazi kijacho kiweze kutukumbuka kwa kulinganisha yaliyopita nay a wakati huo
Ni ukweli uliodhahiri kuwa kumbukumbu ni muhimu isivyodhanika kwa maendeleo na ustawi wa utunzaji wa taifa, taasisi au mtu binafsi, hivyo zinapaswa zitunzwe,zikuzwe,zistawishwe,zielezwe na ziandikiwe maelezo
Uaminifu katika utunzaji ni muhimu kwani kuna hatari kubwa ya kuweka kumbukumbu ambazo zimebeba uongo ndani yake na nje zimevishwa sura ya ukweli kwasababu tunaandaa siku mbaya kwa kizazi chetu kijacho
Historia ni mwalimu mzuri kwa sababu ili uweze kutafsiri na kuyaelewa yanayotokea sasa na kuyaelewa yatakayotokea kesho, tuna lazima ya kuangalia na kutafsiri kilichotokea jana
Watanzania tunayo fursa nzuri ya kuutafakari na kuutathimini utamaduni wetu na hivyo kujitahidi kuutunza, kuulinda, kuuboresha, kuukuza na kuusambaza kwasababu nchi isiyo kuwa na utamaduni ina kosa mizizi ya kusimamia
Utamaduni ni roho ya Taifa na tunu yetu tuutunze ili tuweze kujivunia na kuchangia kwenye ustaarabu wa ulimwengu katika muunganiko wa tamaduni na ustaarabu wa dunia
Hatuwezi kuukimbia udhaifu wetu, lakini tunaweza kupigana nao na tukidhamiria vya kutosha tunaweza kushinda ambapo wakati stahiki ni sasa hapa tulipo kwa sababu uimara wa utamaduni wa kizazi cha sasa na kijacho upo mikononi mwetu
Leo, sisi ni vyombo vya uamuzi wa kutengeneza Taifa lenye afya njema kiutamaduni,mira na desturi kwa kutunza yale yafaayo na kuyarekebisha au kuyaondoa yale yasiyofaa kwa faida yetu nay a vizazi vijavyo
Mtazamo wangu na wako ndio unaotengeneza uhai wa utamaduni na taifa letu, hivyo tuamue kuwa chombo cha mabadiliko kwa kuwaelimisha na kuwahamasisha umuhimu wa utamaduni na makumbusho kwani utambulisho una uwezo mkubwa wa kuakisi maendeleo kusudiwa
Mwandishi wa Makala
Anapatikana 0715-335051

Thursday, February 16, 2012

MASHINDANO YA KAPTENI CUP YANAYOSHIRIKISHA TIMU 10 YAFUNGULIWA LITUHI

 Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi Kapteni John Komba akifungua Mashindano hayo
            Timu hizo kabla hazijaanza mashindano zikisalimiana
 Mechi kati ya Police Fc na Shujaa Fc ikiendelea ambapo mpaka mpira unamalizika Police Fc 1 na Shujaa Fc 0
 Baadhi ya mashabiki wakiangalia mechi kati ya Police Fc na Shujaa Fc
Na Stephano Mango, Nyasa
MASHINDANO ya mpira wa miguu yaliyoandaliwa na  Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi Wilaya mpya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma Kapteni John Komba na kushirikisha timu 10 kutoka kata ya Lituhi yamefunguliwa rasmi
Akifungua mashindano hayo mwandaaji wa Mashindano hayo Mbunge Kapteni John Komba alisema kuwa mchezo wa soka unapendwa na watu wengi na unapochezwa huleta furaha kwa wachezaji na mashabiki
Komba alisema kuwa mara nyingi vijana wa kata ya Lituhi walikuwa wanaomba nianzishe mashindano ya soka ili waweze kufurahi na kukuza vipaji vyao
“Nilikubali maombi yao na kuanzisha mashindano haya yanayoshirikisha timu 10 kutoka ndani ya kata ambayo nimeyazindua ili vijana wapate burudani, wajenge afya zao na kubadilishana mawazo namna ya kuwa vijana wenye mawazo chanya ya kujenga nchi yao”alisema Komba
Alieleza kuwa vijana hao kwa kuhitaji mashindano hayo kumeonyesha kuwa hawapendi kupoteza muda wa kuzurula, kutenda vitendo viovu hasa muda wa jioni baada ya kutoka katika shughuli za kilimo au ujasiliamali
Alisema kuwa msindi wa kwanza katika mashindano hayo atapata zawadi ya kombe na fedha shiingi 150,000, msindi wa pili shilingi 100,000 msindi wa tatu 50,000 ambapo timu zilizobaki ambazo zimeshiriki zitapata zawadi ya shilingi 20,000 kila timu
Alifafanua kuwa ili mashindano hayo yawe ya kisasa zaidi nimetengeneza nguzo za magoli (miamba) nimetoa jezi 3 za waamuzi kwa maana ya muamuzi wa ndani na wawili wa pembeni, pia nimetoa jezi 10 kwa timu zilizoshiriki zote na kwamba gharama zake kwa jumla ni shilingi milioni 3
Awali  Mratibu wa mashindano hayo Mosi Zamtanga alisema kuwa kabla ya mshindano hayo timu shiriki zilipitia michakato mbalimbali ambapo kwa zile ambazo zilikidhi vigezo vilivyoweka ndizo zilizo sajiliwa kushiriki mashindano
Zamtanga alizitaja timu zinazoshiriki mashindano hayo kuwa ni Nkaya Boys, Lituhi Sekondari, Mzalendo, Shujaa, Dodoma, Ngingama, Njomole, Majeshi, Police na Astone Villa
Mwisho

MWANASHERIA MBOGORO NA MTAZAMO MBADALA WA KAULI MBIU YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANGANYIKA

 Mwanasheria Edson Mbogoro akifafanua jambo wakati wa mdahalo huo
 Mwanasheria Edson Mbogoro akiwa kwenye moja ya mikutano ya kuimarisha chama cha Chadema mjini Songea
Baadhi ya wananchi waliohudhulia mdahalo huo kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bombambili Jimbo Kuu la Songea hivi karibuni

Na Stephano Mango,Songea
SIAMINI kama kuna Mtanzania ambaye hajawahi kuisikia mahali popote kauli mbiu ya sherehe ya  miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika iliyokuwa inatangazwa kwa nguvu kubwa na Serikali ya kuwa Tumethubutu,tumeweza na tunazidi kusonga mbele.
Mwanasheria na Wakili wa Kujitegemea Edson Mbogoro ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) ameamua kutoa maoni yake juu ya kauli mbiu hiyo ili kuweza kuona kama inaakisi uhalisia wa mambo kwa kipindi hicho cha miaka 50 toka tupate uhuru.
Akizungumza hivi karibuni kwenye mdahalo wa kauli mbiu ya miaka 50 ya uhuru uliofanyika kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bombambili mjini hapa ,Mbogoro akiwasilisha mada kwenye mdahalo huo  alisema kuwa ukitafakari kwa umakini maneno yanayounda kauli mbiu ya miaka 50 ya uhuru na kuoanisha na uhalisia wa mambo toka tupate uhuru  utabaini kuwa kauli mbiu hiyo imetiwa chumvi.
“Maoni yangu sio msahafu yanaweza yakakosolewa au kupingwa kwa nguvu ya hoja kwani nayatoa kama mchokonozi kwa ajili ya kuibua mjadala wenye afya zaidi kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu”alisema Mbogoro.
Alisema kuwa uhuru katika ngazi ya mtu binafsi humaanisha uwezo wa kujiamulia mambo yako mwenyewe ambapo katika ngazi ya Taifa au Nchi humaanisha kujitawala,yaani kuondokana na hali ya kuwa chini ya himaya ya kigeni ambayo hushikilia na kuamua mustakabali wa kila jambo kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni nakadharika.
Uhuru humaanisha kujinasua toka kwenye minyororo ya kupuuzwa kifikra ambapo jamii huzaliwa upya na kujenga matumaini mapya ndio maana katika hotuba aliyoitoa siku ya uhuru hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliainisha maadui wakuu watatu ambao ni umaskini,ujinga na maradhi na kusema kuwa adui mkubwa kuliko wote ni umaskini.
Ninamnukuu Mwl Nyerere “…….Tukiweza kumshinda adui umaskini tutakuwa tumeweza kupata silaha itakayotuwezesha kuushinda ujinga na maradhi…namuomba kila raia wa Tanganyika aape kiapo cha kuwa adui wa umaskini, amshambulie adui huyo popote atakapoonekana”.
Mwalimu Nyerere alitutahadharisha kuwa katika kupigana vita dhidi ya maadui hao, hatuna wajomba wa kupigana badala yetu, kwamba tunaweza kupata misaada ya wafadhiri kutoka nje lakini jukumu la kujiletea maendeleo ni letu wenyewe kwanza.
Mbogoro alieleza kuwa Serikali ya uhuru ilijiwekea malengo hayo matatu, ni jambo la dhahiri kuwa tuliposherekea miaka 50 ya uhuru moja ya maswali ambayo tulipaswa kujiuliza ni kiasi gani tumeweza kuupiga vita umaskini .
Alisema kuwa wakati huo tatizo kubwa ni kwamba Mwalimu hakukabidhiwa na wakoloni nchi kama tunavyoiona leo bali alikabidhiwa makabila 120 yenye viongozi wa kimila yaani Machifu, utaifa haukuwepo ambapo kazi kubwa ni kuyaunganisha makabila hayo na kuwa taifa moja lenye umoja na mshikamano
Alifafanua kuwa Mwalimu Nyerere alifuta mfumo wa uchifu uliokuwepo akaunda Wizara ya sanaa ya taifa na vijana ili kumwezesha mtu mweusi kujitambua na kuthamini utu wake na utamaduni wake na kwa mvuto wa Mwalimu ulisaidia kuwaunganisha watanganyika ambapo mbio za mwenge zilihamasisha hisia za uzalendo na utaifa na lugha ya Kiswahili ilisaidia kuwaunganisha watanganyika.
Alieleza kuwa neno kuthubutu kwa mujibu wa kamusi ya standard Swahili/English iliyochapwa na chuo kikuu cha Oxford toleo la 1995, linamaana ya ujasiri wa kuamua na kutenda jambo gumu ambalo ni la hatari, ambalo mafanikio yake hayatabiri, kwa kukubali kupata uhuru, hakuna shaka kuwa tulithubutu kwa vile ulikuwa uamuzi mgumu unaotupelekea ambako hatuna uzoefu nako, kusikotabirika.
Alisema kuwa, mara baada ya kupata uhuru chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere Serikali iliweza kuwa na mipango mizuri na ambayo ilitekelezeka kama vile ujenzi wa viwanda vya kukoboa na kusindika mazao ya biashara kama vile, korosho, kahawa, kutengeneza nguo, viwanda vya kutengenezea zana za kilimo, viwanda vya kusindika chakula na vingine vingi.
Alieleza zaidi kuwa ujenzi wa mashirika imara ya uchukuzi na usafirishaji wa anga, nchi kavu na majini na mashirika ya ugavi na kwamba asilimia ya 90 ya watanzania walikuwa wanajua kusoma na kuandika na kwamba wakati Serikali ya awamu ya kwanza inaondoka madarakani ilikuwa imeshaweka msingi wa mapinduzi ya viwanda na teknologia ambapo kilichotakiwa ni marekebisho ya uendeshaji kwa ajili ya kuleta ufanisi zaidi.
Alisema kuwa wakati huo tulithubutu kuweka misingi mizuri ya maendeleo, swali la kujiuliza je tumeweza?, katika kujibu swali hilo viongozi wa Serikali wanatumia takwimu kuonyesha kiwango cha mafanikio kama vile idadi ya watu, upatikanaji wa maji,  afya,  miundombinu, vyuo vikuu, shule za msingi na sekondari toka wakati tunapata uhuru hadi sasa na vitu vingine.
Alisema kuwa kwa mtu wa kawaida ambaye anaheshi mu ukweli hawezi kujisifia hatua ya maendeleo tuliyoipiga kwani hailingani kabisa na umri wetu wa nusu karne kama Taifa, kwani tungeweza kufanya mara 50 zaidi ya hapa tulipo, hivyo hatujaweza bali tumeshindwa.
Alisema kuwa tunatakiwa kujilinganisha na nchi kama Malaysi, Indonesia, Singapore, Thailand, Veirtnam na nyingene ambazo tulipata nazo uhuru katika kipindi  kinachokaribiana zikiwa na hali duni kama tulivyokuwa nayo sisi wakati tunapata uhuru.
Alisema kuwa, mazuri yote ya awamu ya kwanza yameyeyushwa na awamu zilizofuata, kwani Mwalimu Nyerere aliacha viwanda 12 vya nguo vinavyofanya kazi lakini leo vimebaki vitatu ambavyo vinasuasua, aliacha mashirika ya umma 380 ambayo mengi yamebinafsishwa.
Alifafanua kuwa viwanda vya kuyeyusha chuma na kutengeneza vipuri na zana mbalimbali vya  Mang’ua na Kilimanjaro, Tanzania Scania Assembly Plan, Kibaha Mgololo kilichopo Mufindi, vimeuzwa kwa bei chee, tumerudi kwenye utegemezi hata kwenye kijiti cha kuchokonolea mabaki ya vyakula kwenye meno ni made in china.
Alieleza kuwa leo tunasubiri wafadhili hata kwa ajili ya kutujengea matundu ya vyoo vya watoto wetu mashuleni, ujinga umeongezeka kwa maana asilimia 90 ya watu wanaojua kusoma na kuandika alioiacha hayati Mwalimu Nyerere imepungua hadi kati ya asilimia 65 na 70.
Alieleza zaidi kuwa hatuna umeme wa uhakika baada ya miaka 50 ya kujitawala, ni asilimia 3 tu ya kilimo chetu ndio kinatumia trekta, asilimia 26 wanyama kazi na asilimia inayobaki bado ni jembe la mkono.
Alisema kuwa Tanzania ni nchi maskini ikiwa katikati ya utajiri kwa asilimia 18 ya maji baridi dunia yafaayo kwa kunywa na umwagiliaji yako Tanzania, nchi ya tatu barani Afrika  kwa uzalishaji  dhahabu nyingi baada ya Afrika Kusini na Ghana.
Alifafanua kuwa Tanzania ni nchi ya barani Afrika kwa kuwa na Ng’ombe wengi baada ya Ethiopia, pia inazalisha madini yenye thamani kubwa aina ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania pekee lakini ni nchi inayoongoza kwa kupokea misaada mingi barani Afrika kuliko nchi yoyote ile
Alisema kuwa ni nchi ya tatu Duniani kwa kupokea misaada mingi baada ya Afghanistan na Iraq, misaada Tanzania imeongezeka toka dola za kimarekani 39.19 mwaka 1961 hadi dola za kimarekani bilioni 2.89 mwaka 2009 lakini misaada hiyo imekuwa kama ndoo ya maji inayovuja kwani imeshindwa kutukwamua.
Alisema ukosefu wa falsafa ya kuiongoza nchi kumepelekea utafunaji wa wazi wa rasilimali za taifa kwani ufisadi umetamalaki kwenye ofisi za umma,mikataba mibovu na kuwafanya wawekezaji kuja nchini kuchuma rasilimali zetu zote na kuwaacha watanzania wakiwa maskini.
“Uongozi wa umma umekuwa dili kwa baadhi ya watu kujineemesha mchana kweupe na kuwafanya watanzania wengi kubaki maskini na kusababisha maadui watatu waliotangazwa wakati tunapata uhuru, umaskini, ujinga na maradhi kushindwa kutokomezwa”alisema Mbogoro.
Alisema kuwa katika mazingira hayo hatuna sababu ya kusema kuwa tumeweza bali tumeshindwa bila kulekebisha matatizo ya msingi yanayotukabili kama Taifa kusonga mbele ni kujidanganya na kwamba kauli mbiu sahihi ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru ilipaswa kuwa Tumethubutu, Tumeshindwa, Tumekwama, Tunahitaji kujikwamua.
Alimalizia kwa kusema kuwa, nimejaribu kuonyesha tulikotoka na tulipo na si zaidi kuhusu tunakokwenda kwa sababu ni kiza kinene, hivyo kama taifa tunahitaji kujitazama upya kwenye kioo cha ukweli na tukubali vile kinavyotuonyesha kisha tujadiliane vya kutosha ili tujinasue na kusonga mbele.
Mwandishi wa Makala
Anapatikana 0715-335051
www.stephanomango.blogspot.com