About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Saturday, October 15, 2011

CHAMA KUTOA HUDUMA ZA USHAURI NASAHA KWA WANACHAMA WAKE KUTOKANA NA VIKOMBE KUDUNDA WILAYANI TUNDURU

Na, Augustino Chindiye Tunduru

CHAMA cha Wanaoishi na Virusi vinavyo sababisha Ukimwi na Ukimwi cha Tunduru Affected Society TAAs+ Tawi la Tunduru mkoani Ruvuma limeanza kutoa huduma ya Ushauri nasaha kwa Wateja wake zikiwa ni juhudi za taasisi yao kuwanusuru wanachama wake wasikate tamaa na kuwafanya wapoteze maisha haraka baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Chama hicho Issa Kadabadi na kuongea kuwa maamuzi hayo yamechukuliwa kufuatia kuwepo kwa wimbi kubwa la Waganga wa Tiba asili wanaotoa tiba mbadala ya VIKOMBE kwa Watu wanaoishi na VVU na UKIMWI hali ilipelekea baadhi ya wanachama wake kupoteza maisha.

Alisema hadi sasa Chama chake kimepoteza wanachama watano baada ya kuibuika kwa watoa vikombe hao ambao wengi wao wamekuwa wakiwadanganya kwa kuwazuia kuendelea kunywa dawa zao ambazo hutolewa Hospitali za ARVs hali iliyo usukuma uongozi wa Taasisi hiyo kuanzisha darasa hilo katika kitengo cha darasa la kutolea elimu ya ushauri nasaha kilichopo katika Hospitali ya serikali ya Wilaya ya Tunduru.

Akifafanua taarifa hiyo Kadabadi alisema kuwa masomo ambayo hutolewa kwa ushauri wenye ushuhuda wa wanachama 12 ambao walipelekwa katika Kikombe kinachotolewa kwa Bibi Hadija Alli Omari wa Kijiji cha Misechela Wilayani humo baada ya kugundulika kwa tiba hiyo mbadala maarufu kwa jina la KIKOMBE ambao mbali na Bibi huyo kuwaeleza wakapime baada ya wiki mbili watakutwa hawana maambukizi ya ugonjwa huo hatari lakini baada ya kupimwa walikutwa wakiwa hawajapona “ yaani kikombe kimedunda”    
       
Wakati hayo yakiendelea taarifa kutoka ofisi ya Chama kinachosimamia usajiri wa Waganga na Wataalamu wa Tiba asili (CHAWATIATA) na kudhibitishwa na Katibu wa Chama hicho wa Wilaya ya Tunduru Sofia Mpinga zinaonesha kuwa jumla ya Waganga 37 wamesajiriwa na Chama hicho kwa ajili ya kutoa Tiba mbadala ya kikombe Wilayani humo hali inayo onesha kuwa huduma zinazotolewa na maafisa tabibu katika Hospitali, Zahanati na Vituo vya afya wilayani humo wameonekana kuzidiwa nguvu na waganga hao.

Akizungumzia hali hiyo pamoja na kukiri kuwepo kwa changamoto kubwa ya mfumuko watoaji wa tiba mbadala za Vikombe  Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Dkt. Alex Kazula  alisema kuwa Wilaya yake inakabiliwa na tatizo kubwa la maambukizi mapya ya VVU na Ukimwi.

Dkt. Kazula aliendelea kufafanua kuwa Takwimu zinaonesha kuwa Wilaya yake inakabiliwa na maambukizi ya Ugonjwa huo kwa asilimia 4.1% kwa wakazi wote wanakadiliwa kuwa ni zaidi ya Wananchi 200,000 wanaoishi Wilayani humo.

Alisema pamoja na takwimu hizo, taarifa za wagonjwa wapya zinaonesha kuwa watu 226 wakiwemo wanawake 121 na wanaume 105 waligundulika mwaka 2010 ikiwa ni sawa na asilimia 3.7% ya  watu 6079 walijitokeza kupima Virusi vya ukimwi kwa hiari na kati yao wanaume walikuwa 2408 na wanawake 3671.

No comments:

Post a Comment