Na Steven Augustino,Songea.
WAANDISHI wa habari nchini wameaaswa kufanya kazi zao kwa kufuata misingi ya taaluma ya habari ili kulinda amani ya taifa letu.
Hayo yalisemwa na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambugu wakati alipokuwa akifungua mkutano maalumu wa Wadau wa habari mkoani Ruvuma uliofanyika kwenye ukumbi wa chama cha walimu mjini Songea.
Mwambungu alisema waandishi wa habari ni kioo cha jamii hivyo hawana budi kufanya kazi zao kwa moyo wenye uzalendo na sio kuandika habari zenye kuchochea maovu.
“Ndugu zangu waadishi tusimame katika maadili, mtihani uliopo ni namna ya kuzingatia maadili yanayoambatana na taaluma yenu hivyo fanyeni kazi kwa uaminifu”,alisema Mwambungu
Alisema kwa ujumla vyombo vyote vya habari vinaongozwa na kanuni zilizowekwa, lengo lake la kwanza ni kuhakikisha umma unapata habari zilizo sahihi hivyo msipotoshe umma mkasababisha mahafa makubwa
Kadhalika alieleza kuwa ni vyema waandishi wajitambue kuwa wao ni nani katika jamii hivyo ni vyema wajiwekee utaratibu mzuri wa kufanya kazi katika taaluma yao ili wasiweze kuingiliwa na watu wengine.
Alifafanua kuwa kuna watu wamekuwa wakiingilia taaluma hiyo ni vyema wachukuliwe hatua zinazostahili pale wanapobainika kuvamia tasnia hiyo kwa nia mbaya ya kuchafua sifa ya wanahabari.
Vilevile alisema kuwa habari zinazoandikwa zizingatie utamaduni wa kujenga taifa iliziweze kulinda amani, kukosoa maovu katika jamii na kuepusha kuchochea chuki na uhasama miongoni mwa watanzania na akaongeza kuwa endapo hatutazingatia haya gharama yake baadaye ni kubwa.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani Ruvuma Bw. Andrew Kuchonjoma aliwataka waandishi wa habari kuacha malumbano yasiyo ya lazima miongoni mwao.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment