About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Saturday, October 15, 2011

WAKILI AITAKA MAHAKAMA IWAPIME AKILI WASHTAKIWA WA KESI ZA MAUAJI

Na Augustino Chindiye, Tunduru
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma imewaamuru watuhumiwa Wawili wa makosa ya mauaji ya kukusudia kwenda kufanyiwa uchunguzi wa akili katika Hospitali maalumu ya Mirembe inayotibu wagonjwa wa akili nchini.

Amri hiyo imetolewa na Jaji wa Mahakama kuu kanda ya Songea Mkoani Ruvuma Hamisa Kalombola katika vikao vya kusikiliza kesi za mauaji zinazoendelea katika Mahakama kuu Wilayani Tunduru baada ya kuridhishwa na hoja zilizotolewa na upande wa Utetezi unao ongozwa na Wakili wa Kujitegemea Sebastia Waryuba.

Walio amriwa kupelekwa Mirembe kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa akili zao ndipo kesi zao zije kuendelea katika vikao vijavyo ni  Susani Kapinga anaye kabiliwa na kesi ya mauaji namba 10/2011 ya kumuua Mtoto wake wa Miaka 10 marehemu Jafeti Njovu katika tukio lilitokea kijiji cha Kumbara Wilayani Namtumbo April 27 2010.

Mtuhumiwa mwingine aliyeamriwa kwande kupimwa akili kupitia kifungu namba 220 (1) cha mwenendo wa Mashtaka kinacho iruhusu mahakama hiyo kutoa amri ya watuhumiwa wanaodhaniwa kuwa ni Wagonjwa wa akili ni Salum Furahisha Masame anayekabiriwa na kesi ya mauji ya kukusudia Namba 4/2011 ya kuwaua Baba yake mzazi Marehemu Furahisha Masame na  Mama yake wa kambo marehemu Asumini Mohamed katika tukio lilitokea May 22/2010 katika kijiji cha Muhuwesi Wilayani Tunduru.

Awali wakisomewa mashitaka hayo mbele ya Jaji Kalombola watuhumiwa hao kwa nyakati tofauti walikubali kufanya makosa hayo hali ambayo ilisababisha upande wa Utetezi unao ongozwa na Wakili Waryuba kujenga hoja ya wateja wake kupelekwa kupimwa akili akidai kuwa kitendo cha kukubali kwao kiurahisi wakati wakiwa wanafahamu kuwa adhabu ya makosa waliyo kubali ni kifungo cha maisha au kunyongwa hadi wafe kinamtia mashaka kuwa huenda wateja hao walifanya makosa hayo bila kujifahamu au ni wagonjwa wa akili.

Wakati wakili Wariyuba akijenga hoja ya wateja wake kwenda kufanyiwa uchunguzi wa akili katika Hospitali ya Mirembe iliyopo katika Manispaa ya Dodoma, upande wa Jamhuri wenye jukumu zito la kuthibitisha bila kutia mashaka juu ya tuhuma zinazo wakabili watuhumiwa hao unao ongozwa na Mwanasheria Msomi wa Serikali Hamimu Nkoleye ulionekana kukubali amri hiyo kwa shingo upande hasa kwa kesi inayomkabili mtuhumiwa Masame.

Katika ujenzi wa hoja za kisheria pamoja na mambo mengine, Nkoleye alikataa kuridhia kitendo cha Wakili wa Utetezi kutumia kifungu hicho dhidi ya mtuhumiwa Masame kwenda kufanyiwa uchunguzi huo kwa kudai kuwa wakili Waryuba anapingana na kifungu Namba 220 (1)  kwani kauli za mteja ambaye pamoja na kukubali mbele ya Jaji pia hapo awali alikubali kutekeleza mauaji hayo kituo cha Polisi na mbele ya mlinzi wa amani.

Alisema katika Maelezo hayo mtuhumiwa huyo anayetetewa na Waryuba alidai kuwa alichukua uamuzi huo wa kuwaua kwa kuwapondaponda na mwichi wa kutwangia baada ya kumshuhudia Marehemu baba yake huyo akiponda raha na kimada wakati mama yake mzazi anapata shida kiasi cha kukosa fedha za kujikimu na chakula.

“ Ingawa kifungu namba 220 (1) kinairuhusu Mahakama kutoa amri ya mtuhumiwa kwenda kupimwa akili, upande wa mashtaka uliiomba mahakama isitoe amri hiyo kwa Mtuhumiwa mauaji Namba 4/2011  Salum Masame kwani kitendo hicho kitachelewesha kesi hiyo bila sababu za msingi” alisema Nkoleye .

Akitoa amri hiyo Jaji Kalombola alisema kuwa pamoja na Mahakama kuzingatia hoja zote zilizotolewa na upande wa Utetezi na Jamhuri alidai kuwa ingawa kifungu namba 220 (1) kilichotumika na upande wa Utetezi kinatoa uhuru kwa mahakama kuridhia kutoa amri hiyo au kutotoa lakini kutokana na uhuru huo, mahakama imeona ni busara kutoa amri hiyo ili haki iweze kutendeka.

Jaji Kalombola anaendele kusikiliza kesi Nne (4) zinazoendelea katika Mahakama kuu Wilayani Tunduru ambapo kati yake kesi mbili ni za mauaji ya kukusudia zinatokea Wilayani Namtumbo na kesi Mbili ni matukio yaliyo tokea Wilayani Tunduru. 

No comments:

Post a Comment