About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Saturday, October 15, 2011

DKT MPONDA AWAHIMIZA WANANCHI KUZINGATIA USAFI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NCHINI

Thomas Lipuka Songea
WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hadji Mponda  katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani mwaka huu Mkoani Ruvuma,ikiwa pia siku ya uzinduzi wa sherehe za miaka 50 ya uhuru kauli mbiu ya siku hiyo ya Mazingira ilikuwa tusimamie na kudumisha muungano ,tuhifadhi Mazingira.
Ambapo kauli mbiu halisi ya miaka 50 ya Uhuru ni kwamba Tumedhubutu,Tumeweza na Tunasonga mbele.
Katika siku hiyo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii aliwakumbusha watu wa Mkoa wa Ruvuma na nchi nzima kuwa Wizara ya Afya imechukua juhudi kadhaa katika kufikia lengo la kuwa na hali bora ya Afya na usafi wa Mazingira nchini.
Dk.Mponda alizitaja baadhi ya hatua hizo ni pamoja na uandaaji wa sera ya usafi na Afya kwa Mazingira,ambayo alisema ipo katika hatua za mwisho za ukamilikaji.
 Hatua nyingine ni uandaaji wa sheria ya Afya ya Jamii ya mwaka 2009 na Sheria ya usajili wa Afya kwa Mazingira ya mwaka 2007 ambazo zinakazia usafi na Afya ya Mazingira nchini kote.
Alisema mpango mkakati wa Afya na usafi wa Mazingira wa mwaka 2008-2017 utatiliwa mkazo mikoa yote ikiwa ni pamoja na kuratibu zoezi la mashindano ya Afya na usafi wa Mazingira yanayoshirikisha Halmashauri zote nchini.
 Dk Mponda aliongeza kusema kwamba Halmashauri zimefanikiwa kujenga uwezo kote nchini kupitia mbinu shirikishi zinazohimiza na kuhamasisha mabadiliko ya tabia ili kuinua usafi nchini.
 Amesema ushirikishwaji wa jamii ni mbinu kuu katika kuhimiza usafi wa mbinu ya Afya ya Mazingira pia urejeshwaji wa mafunzo ya wasaidizi wa Afya ya mazingira ni muhimu ili kujenga uwezo wa Vijiji na Kata katika kusimamia usafi wa Afya na Mazingira ngazi ya Kijiji na Kata.
 Dk.Mponda amesisitiza kuwa mashindano ya usafi na Afya ya Mazingira katika Halmashauri hapa nchini yameongeza chachu ya ushirikishi wa sekta binafsi katika kutoa huduma za usafi pia kuongezeka kwa ukusanyaji taka ngumu na jamii kushiriki kwa kiasi kikubwa katika shughuli za utunzaji wa usafi wa Afya ya Mazingira na kuchangia huduma hiyo hatimaye kupunguza magonjwa ya mlipuko.
Halmashauri nchini zimepata changamoto katika bajeti zake ambazo kuna ongezeko la fedha ili kwenda sambamba na utoaji wa huduma ya kutunza usafi na Afya ya Mazingira katika maadhimisho hayo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mheshimiwa Dkt Haji Mponda alizipongeza Halmashauri kwa ongezeko la bajeti ya usafi wa Mazingira katika mipango yao,uimarishaji wa huduma za uzoaji wa taka ngumu na maji taka.
Dkt Mponda alizisifu baadhi ya Halmashaurti ambazo zinaimarisha na ukarabati machinjio ili kuleta afya na usafi wa mazingira katika utoaji wa huduma hizo za machinjio hatimaye kuepuka magonjwa yasiyo na mpango.
Akizungumzia masuala ya Masoko ili kuleta usafi wa Mazingira na Afya kwa walaji Dkt Mponda alisisitiza ujenzi wa Masoko mapya,vyakula viwe katika hali ya usafi na haiba kwa mlaji,pia kuwepo kwa vyoo katika Masoko hayo ambavyo ni bora na safi wakati wote.
Dkt Mponda alisisitiza Halmashauri zote kujali na kuongeza ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua ili kuepuka mkusanyiko wa taka wakati wa mvua,kwani miundombinu dhaifu haiwezi kudhibiti taka ngumu na maji taka.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii alisema zipo changamoto za mipango dhaifu na bajeti ndogo ya usafi wa Mazingira uhaba wa vitendea kazi,wataalamu wa Afya kasi ndogo ya mabadiliko ya jamii katika kulinda usafi na Afya kasi ndogo ya mabadiliko ya jamii katika kulinda usafi  na Afya ya mazingira pamoja na tabia ya jamii katika kulinda,kuboresha mazingira mambo ambayo yanafanyiwa kazi na Serikali pia jamii ipate elimu na kubadilisha tabia ya kupenda usafi na kuchukia uchafu.

No comments:

Post a Comment