About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Friday, March 30, 2012

CCM SONGEA YAISHIKA PABAYA CHADEMA KAMPENI ZA UDIWANI MANISPAA YA SONGEA

Hamis Abdala Ally ambaye ni mmoja wa timu mahiri ya kampeni ya Chama cha Mapinduzi Manispaa ya Songea akizungumza kwenye mkutano huo wa kampeni wa kumnadi George Oddo kuwa diwani katika kata ya Lizaboni

Ibrahimu Ngaponda akiwahutubia wananchi wa Madizini kata ya Lizaboni kwa lengo la kuwahamamisha wananchi hao kumchagua George Oddo ili awe Diwani wa Kata ya Lizaboni

Add caption

Mgombea udiwani kupitia Ccm Kata ya Lizaboni George Oddo akiomba kura kwenye moja ya mikutano ya kampeni za udiwani

Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Manispaa ya Songea Zuberi Mtelela akiwahutubia wananchi wakati wa mkutano wa kampeni za kumnadi George Oddo jana

Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Diwani wa Vitimaalumu Manispaa ya Songea Genfrida Haule akiwaomba wananchi wamchague George Oddo kuwa diwani wa Kata ya Lizaboni



Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Matogoro Charles Mhagama akiwahutubia wananchi wa kata ya Lizaboni kwenye mkutano wa kampeni za Ccm

Meneja Kampeni wa Kata ya Lizaboni Kwinyelesa kulia akimnadi George Oddo kuwa diwani wa Kata hiyo ili aweze kushirikiana na wananchi wa kata hiyo kusukuma mbele gurudumu la maendeleo mbele
Na Stephano Mango, Songea
WANANCHI wa Kata ya Lizaboni Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wametakiwa kuwa makini katika kufanya maamuzi sahihi ya kumchagua Diwani wa Kata hiyo katika uchaguzi unatarajiwa kufanyika aprili mosi mwaka huu kwa kumchagua mgombea wa Chama cha Mapinduzi ili aweze kushirikiana na wananchi katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo
Wito huo umetolewa jana na Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Diwani wa Vitimaalum Manispaa ya Songea Genfrida Haule kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za udiwani kata ya Lizaboni uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Madizini
Haule alisema kuwa Chama cha Mapinduzi kina hazina kubwa ya makada ambao wanaweza kuipeperusha bendera ya chama katika uchaguzi huu wa udiwani lakini kutokana na busara za viongozi wa Ccm na matakwa ya wananchi tumemteua George Oddo aweze kuwatumikia wananchi wa kata hii
Alisema kuwa awali Kata hiyo ilikuwa ina matatizo mengi sana katika sekta ya Afya, elimu, barabara, maji na masoko lakini kutokana na sera nzuri za Ccm kwa kupitia aliyekuwa Diwani wa Kata hii marehemu Said Ali Manya Serikali ya inayoongozwa na Ccm ilikuwa sikivu na ndio maana mnaona maendeleo makubwa katika Kata ya Lizaboni
Alieleza zaidi kuwa kuna baadhi ya kero bado zipo kwenye kata hii hivyo ni vema mkamchagua diwani kupitia tiketi ya Ccm ili aweze kumalizia ahadi na kero ambazo marehemu ally Said Manya aliziorodhesha kwa kuweka mikakati ya utekelezaji ili kuleta mabadiliko zaidi ya kimaendeleo
Naye Hamis Abdala Ally ambaye ni mmoja wa timu mahiri ya kampeni ya Chama cha Mapinduzi alisema kuwa wananchi wanapaswa wazipuuze kelele za wapinzani ambao kwao kuona damu inamwagika katika Kata ya Lizaboni kwao ni ushindi
Ally alisema kuwa Chadema wamekosa sera na umakini katika kampeni zao kwa kushindwa kueleza mambo ambayo yataweza kuwasaidia wananchi badala yao wanaendekeza fujo na matusi huku wakishabikia kwa nguvu ukubwa uvunjifu wa amani katika kata hiyo
“ Nimesikitika sana kuona viongozi wa Chadema wanafurahia kuona kuna kijana amepigwa panga na kujeruhiwa vibaya na ajali ya kugongwa kwa mtoto juzi na kudai kuwa kwa kuwa damu imemwagika sasa ndio dalili ya ushindi kwao jambo ambalo linatia shaka wananchi na kudhani kuwa wao ndio waliopanga uvujaji damu huo” alisema Ally
Alieleza zaidi kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi imefanya mambo mengi toka upatikana uhuru wan chi hii kwa kuwawezesha wananchi kupata barabara safi, maji safi na salama, elimu, afya, masoko, na uwezeshaji wa mitaji ya kiuchumi kwa kuzungumza na taasisi za fedha kupunguza masharti katika mikopo yao kwa wananchi
Alifafanua kuwa kupatikana kwa vitu hivyo ndiko kunakosababisha wananchi wapate ustawi wao na kuchangia kuleta maendeleo kusudiwa kwani watakuwa wamekombolewa kwa kiasi kikubwa sana na kwamba mapungufu mengine yanafanyiwa kazi kwani yanafahamika waziwazi
Alisema kuwa kwa kuwa Serikali iliyopo madarakani ni ya Ccm na iliwekwa na wananchi hivyo kuwasikiliza Chadema kuwa wataleta maendeleo ni uongo mkubwa na kitendo cha kuwapigia kura aprili mosi mwaka huu ni kutupa kura zenu na mtasimamisha maendeleo kwa kipindi kirefu
Alifafanua kuwa nyinyi wenyewe wananchi ni mashahidi hakuna mwaka ambao wananchi wamelima mahindi mengi kama mwaka jana lakini Serikali imeyanunua yote na mengine yanaendelea kupelekwa kwenye hifadhi ya chakula sasa hao wanaosema mbolea imechakachuliwa na kusema Serikali imeshindwa kununua mahindi wanapata wapi ujasiri kama sio kuwadanganya wananchi?
“ Eti Zitto Kabwe anafika nyumbani kwa watu badala ya kuuliza wenyeji, yeye anakurupuka na kusema hapa kuna matatizo ya wizi wa mbolea, mafuta ya jenereta za umeme hivyo ichagueni Chadema ili idhibiti hilo, sasa kama wao wanafahamu kuna wizi kwanini wasiiambie Polisi ili mwizi akamatwe badala yake wanataka udiwani kwani Diwani ni Polisi? Watadhibiti kwa njia gani? Kama sio wao ndio wanaofanya mchezo huo mchafu?”
Alisema kuwa hali ya umeme ni ya uhakika kwasababu kulikuwa na tatizo la kiufundi lakini tayari Shirika la Tanesco limeshafanya kazi yake na umeme unapatikana ambapo wananchi wanaendelea na shughuli zao za kujiingizia kipato ili kuyafikia malengo ya maendeleo
Akizungumza kwenye mkutano huo Katibu wa Siasa na Uenezi wa Ccm Wilaya ya Songea Mjini Zuberi Mtelela alisema kuwa wananchi mpigieni kura Oddo George ili aweze akaungane na madiwani wenzake ili aweze kutimiza ahadi ambazo tuliziahidi wakati wa uchaguzi  mkuu wa mwaka 2010
Mtelela alisema kuwa mkiichagua Chadema licha ya kuwa mtakuwa mmepoteza kura zenu na kusimamisha maendeleo kwa miaka mitatu bali mtakuwa mmeongeza kikundi cha watu wenye fujo kinachoshabikia mambo mabaya kwa jamii ya Manispaa ya Songea
Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya Vijana Mkoa wa Ruvuma Mwajuma Rashid alisema kuwa Chadema wamejipanga kuleta vurugu siku ya uchaguzi na tayari wameanza kuwapiga na kuwatishia viongozi wa Ccm hivyo wananchi mkiwapa kura watu hao mtakuwa mnajenga kizazi cha vurugu na kukwamisha maendeleo yaliyopangwa katika kata ya Lizaboni
Rashid alisema kuwa sisi tumetulia lakini uvumilivu una mwisho wake na endapo mamlaka zinazo husika hazitadhibiti mwenendo huo ambao unahatarisha amani katika uchaguzi huo nasi tunaweza tukatumia nguvu zetu ili wapiga kura na wanachama wa Ccm wawe salama
Naye Mwenyekiti wa Ccm Manispaa ya Songea Hemed Dizumba alisema kuwa kazi kubwa inafanywa na wananchi wa Lizaboni ndio maana Chadema wana haha kwani tayari wenyewe wanajua kuwa ushindi kwao haupo
Dizumba alisema kuwa ushahidi upo wazi kutokana na maneno wanayowasema wenyewe kwasababu hizo mbwembwe walizonazo wameshagundua kuwa zinaletwa na washabiki wao kutoka Bombambili, Majengo, Mjini, Mfaranyaki, Misufini na Ruvuma lakini sisi tunazungumza na watu wa Lizaboni ambao ndio wapiga kura
Kwa upande wake mgombea udiwani kupitia Chama hicho Oddo George alisema kuwa uzuri wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi wananchi mmeuona hivyo hakuna sababu ya kuichagua Chadema katika uchaguzi huo
George alisema kuwa mipango ipo wazi kinachotakiwa ni wananchi kukubari april mosi mwaka huu kuwa inapaswa kuitekelezwa na Chama cha Mapinduzi kupitia Diwani wake ambaye ni mimi hivyo wananchi naomba kura zenu zote ili niweze kuibeba mikoba aliyoiacha marehemu Ally Said Manya mabaye alikuwa Diwani wa kata hii kupitia Ccm
Alisema kuwa kama kweli wananchi wa Kata ya Lizaboni mnaheshimu maendeleo mliosaidiana kuyaleta Kata ya Lizaboni na Marehemu Manya basi msipoteze kura zenu kwa kumchagua mgombea wa Chadema ambaye ameshaonyesha kuwa hana dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo watanzania
MWISHO

TIMU YA MLALE JKT YAMWAGIWA VIFAA VYA MICHEZO

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu
Na Augustino Chindiye, Songea

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ametoa vifaa vya Michezo kwa timu ya JKT MLALE ambayo ndio timu pekee ya Mkoa huo iliyotinga katika hatua ya Tisa Bora ya Ligi ya Taifa daraja la kwanza.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni Mipira 16, na viatu jozi 25 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 2.5, zikiwa ni juhudi za serikali ya Mkoa huo kukamirisha maandalizi ya timu hiyo itakayowakilisha Mkoa wa Ruvuma katika Ligi hiyo inayo tarajia kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi huu.

Akiongea katika makabidhiano ya msaada huo Mkuu wa mkoa Mwambungu pamoja na mambo mengine ali toa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kuunganisha nguvu zao na kuiunga mkono timu yao.

Alisema baada ya timu ya Majimaji kufanya vibaya katika ligi hiyo hivi sasa mkoa wake umeelekeza nguvu katika timu hiyo wakiwa na matumaini kuwa timu hiyo ita watoa kwa kuujengea heshima mkoa Mkoa wa Ruvuma

Nao viongozi wa timu ya JKT Mlale na Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoani hapa (FARU) Joseph Mapunda na mwakilishi wa Kikosi cha Mlale Isack Kusimbwa pamoja na neno la shukiurani kwa msaada huo walimuahidi Mkuu wa Mkoa kuwa watahakikisha timu hiyo inatinga ligi kuu.

Walisema msaada huo umefika wakati muafaka na wakaahidi kufikisha vifaa hivyo kwa walengwa pamoja na salamu zake kwa wachezaji wote na wakatumia nafasi hiyo kumkaribisha kiongozi huyo kushiriki katika michezo hiyo ili aweze kujionea kazi ya vijana wake.
Mwisho

Thursday, March 29, 2012

WAKULIMA WA KOROSHO TUNDURU BADO HAWAJALIPWA MADAI YAO LICHA YA SERIKALI KUTOA AGIZO

       Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Madaha
Na Augustino Chindiye, Tunduru

WAKATI kukiwa na maelekezo kutoka Serikani kuwa mabenki yatoe fedha zitakazotumika kuwalipa malipo ya pili, pamoja na kulipia korosho ilizo kopwa kutoka kwa wakulima wa zao hilo wakulima wa wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma malipo hayo bado hayajaanza  kutolewa.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Chama kikuu cha Ushirika wa wakulima wilayani Tunduru (TAMCU) Imani Kalembo alipotakiwa kuzungumzia utekelezaji wa agizo hilo kutoka serikalini.

Akifafanuaa taarifa hiyo Bw. Kalembo alisema kuwa malipo hayo yameendelea kukwama kutokana na majibu ya viongozi wa Benki ya NMB tawi la Tunduru waliodai kuwa bado hawajapokea maelekezo kutoka makao yao makuu juu ya kuanza kutoa fedha hizo zitakazotumika wakati wa malipo hayo.

Katika taarifa hiyo Kalembo alisema kuwa jumla ya tani 4800 zimekwama katika maghala na kusababisha malipo kwa wakulima wa Korosho wilayani humo kushindwa kutolewa ni sehemu ya tani 7000 zilizozalishwa Msimu wa mwaka 2011/2012.

Alisema katika msimu huu Wilaya hiyo ilibahatika kuuza katika mnada mmoja tu kati ya minada 9. ambapo iliuza tani kama 1100 na kwamba hayo ilitokana na wanunuzi wakubwa kukataa kununua korosho hizo kwa bei ya shilingi 1480 kwa kilo moja  waliyoitaka wakulima hao wakiwa wanashinikiza wanunue kwa chini ya shilingi 1400.

Kufuatia hali hiyo baadhi ya vyama vya msingi vya ushirika vya wakulima wa wilaya hiyo vimepata changamoto ya baadhi ya wakulima wake kuondoa korosho maghalani na kuanza kuuza korosho zao kwa walanguzi ambao hutumia kipimo halamu kiitwacho KANGOMBA yaani bakuli linalobeba kilo 2 linanunuliwa kwa shilingi 600.

Akizungumzia hali hiyo Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Madaha pamoja na kuipongeza serikali kwa kutoa tamko hilo alisema kuwa ofisi ya kwa kushirikiana na uongozi wa Mkoa huo zikiwa ni juhudi zaa kuhakikisha kuwa malipo hayo yatolewe kwa haraka.
Mwisho

MKURUGENZI WA WILAYA YA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA ATISHIWA KUUAWA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda
Na Stephano Mango, Songea
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linawasaka watu wasiofahamika wanaodaiwa kumtishia kumuua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Mussa Zungiza(56) ambaye inadaiwa kuwa alitumiwa ujumbe wa maandishi kwenye simu yake ya mkononi akitishiwa kuuawa  .
Akizungumza na www.stephanomango.blogspot.com  jana mchana ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Michael Kamhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea machi 25 mwaka huu majira ya saa za mchana huko katika wilaya ya Namtumbo .
Kamanda Kamhanda alieleza zaidi kuwa inadaiwa mnamo siku tofauti za mwezi machi mwaka huu huko katika wilaya ya Namtumbo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  ya wilaya hiyo Zungiza alipokea ujumbe wa maandishi kupitia kwenye simu yake ya mkononi akitishiwa kuuawa. 
Alibainisha zaidi kuwa kwenye simu hiyo ya mkononi ujumbe huo ulitoka  katika namba  mbalimbali za simu,ambapo ujumbe wa kwanza ulitumwa machi 14 mwaka huu  majira ya saa 1:46 asubuhi na ujumbe wa pili ulitumwa  mach 14 mwaka huu majira ya saa 4:08 usiku .
Alieleza zaidi kuwa ujumbe huo ulieleza kuwa siku yoyote Zungiza atauawa kwa njia ya aina yoyote na kutoeleza chanzo au sababu ya kutaka kumuuwa ,jambo ambalo lilimpa hofu kubwa juu ya maisha yake .
Kamanda Kamhanda alisema kuwa Mkurugenzi Mtendaji huyo Zungiza  baada ya kupokea ujumbe huo kupitia kwenye simu yake ya mkononi  hatua ya kwanza alichukua ya kuwasiliana na kamati ya ulinzi ya wilaya hiyo na kisha alitoa taarifa juu ya ujumbe huo aliotumiwa wa vitisho katika kituo cha polisi cha wilaya ya Namtumbo ambako lilifunguliwa jalada la uchunguzi .
Hata hivyo kamanda Kamhanda alisema kuwa jeshi la polisi mkoani Ruvuma  linaendelea na upelelezi zaidi wa kina kuhusiana na tukio hilo ili kuwabaini watu waliohusika kumwandikia ujumbe kupitia simu yake ya mkononi ambao ulimtishia kumuuwa Zungiza.
 MWISHO

AKAMATWA NA POLISI BAADA YA KUMZIKA MWANAE KICHANGA MAMA AKIWA HAI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda

NA GIDEON MWAKANOSYA ,SONGEA
JESHI la polisi mkoani Ruvuma limemtia mbaroni Anna Mhenga (25) mkazi wa Bombambili katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa tuhuma za kumtupa mtoto wake mwenye umri wa siku moja  kwenye eneo la msitu wa milima ya Chandamali ambako alichimba shimo na kumfukia .
Habari zilizopatikana jana mjini Songea ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael Kamhanda zilisema kuwa tukio hilo lilitokea machi 24 mwaka huu majira ya saa za mchana huko katika eneo la msitu wa Chandamali uliopo katika Manispaa ya Songea.
Kamanda Kamhanda alisema inadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio Anna alijifungua mtoto wa jinsia ya kike kisha aliondoka eneo la nyumbani kwake na alielekea kwenye eneo la msitu mkubwa wa miti wa Chandamali ambako aliamua kuchimba shimo na kukifukia kichanga alichotoka kujifungua .
Alifafanua kuwa inadaiwa kuwa Anna alijifungua mtoto huyo akiwa na ujauzito wa miezi 7 kisha alifikia uamuzi wa kumtupa mtoto wake kwa kumfukia  jambo ambalo liliwafanya majirani wamshitukie ambapo mmoja kati yao ambaye ndiye raia mwema alitoa taarifa katika kituo kikuu cha Polisi cha Songea.
Alieleza zaidi kuwa Polisi baada ya kupata taarifa ya tukio hilo walifanikiwa kumkamata Anna ambapo katika mahojiano ya awali mtuhumiwa alikataa kuhusika na tukio hilo na baada ya upelelezi zaidi wa Polisi alikiri kuwa ni kweli alikuwa na ujauzito .
Alifafanua zaidi kuwa machi 26 mwaka huu majira ya saa za asubuhi  mtuhumiwa Anna alipelekwa kwenye Hospitali ya Serikali ya mkoa Songea kupimwa ambako ilibainika kuwa mazingira yote yalionyesha kuwa mtuhumiwa alitokakujifungua .
Alieleza zaidi kuwa Polisi baadaye waliendelea kumhoji na alikubali kuwa ni kweli alijifungua mtoto wa jinsia ya kike ambaye alidai kuwa amemzika kwenye msitu mkubwa wa miti uliopo eneo la Chandamali .
Kamanda Kamhanda alibainisha zaidi kuwa inadaiwa mtuhumiwa baadaye aliwapeleka askari Polisi kwenye msitu wa Chandamali ambako aliwaonyesha mahali alipomfukia mtoto huyo ambapo walichukua jukumu la kufukua eneo hilo na kukuta maiti ya kichanga ikiwa ndani ya shimo.
Alisema kuwa maiti ya kichanga huyo baadaye ilichukuliwa na kupelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kilichopo katika hospitali ya Serikali ya mkoa Songea na Polisi bado inaendelea kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo .
MWISHO

Wednesday, March 28, 2012

DKT EMMANUEL NCHIMBI MBUNGE WA SONGEA MJINI NA WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO ATINGA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA LIZABONI MANISPAA YA SONGEA

 Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dkt Emmanuel Nchimbi akimnadi mgombea wa Udiwani wa Kata ya Lizaboni, Manispaa ya Songea kupitia CCM  George Oddo aliyesimama kushoto kwenye mkutano uliofanyika kwenye ofisi za CCM kata ya Lizaboni jana
 Mamia ya wananchi wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dkt Emmanuel Nchimbi akimnadi mgombea wa Udiwani wa Kata ya Lizaboni, Manispaa ya Songea kupitia CCM  George Oddo kwenye mkutano uliofanyika kwenye ofisi za CCM kata ya Lizaboni jana
Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dkt Emmanuel Nchimbi akimnadi mgombea wa Udiwani wa Kata ya Lizaboni, Manispaa ya Songea kupitia CCM  George Oddo kwenye mkutano uliofanyika kwenye ofisi za CCM kata ya Lizaboni jana

Monday, March 26, 2012

KONGANO BUNIFU ZINA MCHANGO KATIKA KUKUZA UCHUMI WA NCHI


 Aliyekuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa mafunzo ya Wawezeshaji Kongano Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya( MB) akimkabidhi Cheti cha kuhitimu mafunzo hayo mmiliki wa mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com ,Stephano Mango,wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume Sayansi na Teknolojia Dkt Dugushilu Mafunda. wa kwanza kutoka kulia ni Wawezeshaji wa mafunzo hayo Dkt Flower Msuya na Mhandisi Peter Chisano


Mgeni rasmi aliyefunga mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya (MB) akiwa kwenye picha ya pamoja naViongozi wa Tume ya Sayansi na Teknologia na washiriki wa mafunzo ya Wawezeshaji Kongano Tanzania yaliyofanyika Ukumbi wa The Beach Comber Hotel kuanzia Februari 27 hadi machi 1, 2012
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
HAKUNA ubishi kuwa umaskini nchini Tanzania umebaki kuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya nchini yetu ingawa pia Tanzania ina matajiri wakubwa wachache na maskini wengi.
Kwa mtazamo wangu mtu maskini ni yule asiye na uchaguzi kwenye chakula, hawezi kuyakataa magonjwa wala ujinga katika maisha yake kwani kwake kila kitu ni kigumu na amekuwa sugu katika hali hiyo
Umaskini nchini umeota mizizi wanaishi kwa kipato duni sana kwani wengi wanaishi chini ya dola moja ya marekani kwa siku, umaskini upo mijini na vijijini watu wanatia huruma ukiwaona kutokana na ugumu wa maisha kutokana na sababu mbalimbali
Ikiwemo ya viongozi wetu wengi wanashindwa  kutambua na kuifungua mifumo ya kiuchumi, kisiasa na hata kijamii ili kuwawezesha wananchi kwa wingi wao ili wawe washiriki na wadau muhimu katika kumiliki uchumi wao
Watanzania wengi kushindwa kuwa na maamuzi juu ya mustakabali wa Taifa lao leo na kesho kunaendelea  kuwafanya wageni kutumia vibaya rasilimali tulizojaliwa kuwa nazo
Ni wazi kuwa watanzania tuna rasilimali za kutosha ambazo zinaweza kutukwamua kwenye tope zito la umaskini lakini hatujaweza kuzitumia vizuri na mbaya zaidi tumewaachia wageni ndio wamiliki na kuzitumia kwa ujeuri rasilimali zetu kwa muavuli wa uwekezaji
Hali hiyo inatufanya tuendelee kuwa maskini wa kutupwa na kujenga utamaduni mpya wa utegemezi kwa mataifa ambayo tumewaachia wachume mali zetu na kukimbizia huko kwao
Taifa letu, leo limekuwa na watu tegemezi kuanzia ngazi ya mtu binafsi, kaya, jamii, na hata Taifa, swali la kujiuliza sasa ni je tu wategemezi kwa kiasi gani na je, miaka 50 ijayo tunataka tuwe na Taifa la aina gani?
Utegemezi sio jambo zuri kwani unapunguza uhuru wetu, unatukosesha thamani, tunakosa sauti ya kimaamuzi na unatufanya tuwe wadogo mbele ya wahisani au wafadhiri tunaowategemea
Katika makala haya, nakusudia kujadili jambo chanya la kongano bunifu kama ishara ya kufanya mageuzi ya kiuchumi na kuondoa dhana ya utegemezi kama Taifa na jamii kiujumla kwani katika nchi nyingine jambo hili limesaidia kuinua na kuimarisha uchumi wao
Kongano bunifu zipo nyingi nchini ambazo ili ziweze kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika ngazi ya kijamii hadi kitaifa zinahitaji kuunganika ili ziwe na nguvu ya pamoja katika soko la bidhaa kwa kushirikiana na  sekta binafsi, serikali na wanataaluma katika kongano mahsusi kwenye maeneo mbali mbali hapa nchini kwetu.
Katika nchi nyingi ushirikiano huu umekuwa kichocheo kikubwa cha  ubunifu  ambao husaidia katika kutoa bidhaa zenye viwango na sifa zinazoweza kuhimili ushindani ndani na nje ya nchi kwa malengo kusudiwa
Kongano bunifu zina uwezo mkubwa wa kupunguza umaskini na kutoa nafasi nyingi za kazi kwa jamii pia vilevile Kongano hizi huleta mahusiano ya karibu sana kati ya wanachama wa kongano na wadau wengine wa maendeleo kama vile  wanataaluma, sekta binafsi na serikali.
Wengi wanaweza kushangaa neno kongano bunifu kwani inawezekana halijazoeleka masikioni mwa watu wengi, ili niweze kuwatendea haki wasomaji na wananchi nieleze kidogo maana ya neno hilo
Kongano bunifu ni muunganiko wa shughuli za aina moja za wajasiliamali wenye malengo sawa na wanaofanya kazi katika eneo/ wilaya, mkoa na Taifa moja katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika shughuli yao
Mfano ni wachongaji vinyago, wahunzi, wakulima wa uyoga, mwani, alizeti, mahindi, maharage, ufuta mpunga, wavuvi, wafugaji kuku, watengenezaji batiki, wasindikaji wa mazao, wafugaji wa wanyama mbalimbali, wavuvi na vikundi vya wajasiliamali kama hao
Wajasiliamali wanaojishughulisha na ufugaji wa kuku katika wilaya nzima wanaweza wakatengeneza jukwaa lao(kongano bunifu) litakalokuwa linajadili namna bora ya kuimarisha ufugaji wa kuku ,soko, mitaji, changamoto nyingine zinazowakabili katika kufikia hali stahiki, hiyo ndiyo maana ya kongano bunifu
Kwa kutambua umuhimu wa kongano bunifu katika kuleta uchumi imara wa jamii na Taifa, kuanzia februari 27 hadi machi 1, mwaka huu wa 2012 Tume ya Sayansi na Teknolojia nchini iliweza kutoa mafunzo kwa wawezeshaji kongano katika ukumbi wa The beach Comber, jijini Dar es Salaam
Washiriki wa mafunzo hayo walitoka Tanzania bara na Visiwani ambapo jumla ya washiriki 46 kutoka kwenye kongano 26 nchini walifanikiwa kupata mafunzo hayo muhimu yenye lengo la kukuza kukuza uwezo wao katika kuhamasisha na kuanzisha ushirikiano kati ya sekta binafsi, serikali na wanataaluma katika kongano mahsusi kwenye maeneo mbali mbali hapa nchini kwetu.
Ili washiriki waweze kupata ujuzi wa kuweza kuimarisha kongano ambazo ziko katika mazingira wanakofanyia kazi ili kukuza mkakati wa kuongeza Ubunifu na Ushindani wa  sekta binafsi kupitia kongano bunifu kwa lengo la kuchochea maendeleo ya kiuchumi nchini
Wawezeshaji wa mafunzo hayo walikuwa watanzania ambao ndio wamekuwa wawezeshaji katika nchi za Nigeria, Msumbiji, Ghana, Senegal, Tanzania na Kenya ambao ni Dkt Flower Msuya, Sostenes Sambua na Peter Chisano
Washiriki wa mafunzo hayo waliweza kutoa elimu stahiki ya kuimarisha kongano bunifu katika katika maeneo ambayo washiriki wanatoka ili ziweze kuwa na nguvu moja katika kufanya wazalishaji watengeneze bidhaa bora zenye kukidhi ushindani katika masoko ya ndani na nje.
Kutokana na hilo na kila mmoja akatimiza wajibu wake tuna kila sababu ya kuongoza bara zima la Afrika katika kuonyesha umuhimu wa Kongano bunifu jinsi zilivyoweza kusaidia katika kuongeza pato la taifa, ajira na maendeleo ya jamii , uchumi, ubunifu na Ushindani wa Taifa katika masoko ya nje
Ni vema sasa nchi ikaanza kuendeleza dhana ya kongano bunifu kama njia ya kufikia maendeleo ya kiuchumi nchini kwa kushirikisha wajasiliamali kutumia vema fursa zilizopo za maliasili zetu ili ziwe nguzo kubwa katika kufikia lengo stahiki
Kuanza upya kimtazamo ni fursa ya kubadilika na kuchukua mambo mazuri mapya ambayo kutoka kwa wengine au pale yanapopatikana hata ndani yetu kutasababisha kutuondoa kwenye utegemezi wa kiuchumi na kuondokana na umasikini uliokithili nchini
Kesho ya Tanzania hatuwezi kuongelea bila leo na kila tunachopanda leo ndicho tunachovuna kesho, hivyo msingi wa leo tuliujenga jana uwe mbovu au mzuri pia kwa sababu leo ipo kwa sababu ya kesho ipo na jana ilikuwepo basi leo tunapaswa kubadilika ili tuijenge vyema kesho yenye neema
Leo tukianza upya basi kesho tutazaliwa upya na tukizaliwa upya ndipo hapo tunapopaswa kuwa , hivyo kujifunza na kuanza upya ni ujasiri na ni njia ya kuleta mabadiliko katika dunia ya leo bila kujali gharama za kufanya hivyo
Tuanze upya kwa kuwa wajasiriamali mahiri chini ya kongano bunifu kwani ujasiriamali ni ile hali, uwezo na mkakati au mchakato wa kubuni, kuanzisha, kuendesha na kumudu shughuli halali ya maendeleo ya kiuchumi
Tunahitaji ujasiliamali wa kujiamini, kuthubutu, kubuni na kuendeleza zao tokeo la ubunifu huo kwa kuleta faida chanya katika maisha yake, jamii na Taifa kiujumla kwani ujasiliamali ni nguzo muhimu kwa uchumi wa kisasa wa karne ya 21
Dhana ya ujasiliamali inatimia endapo hali ya kugundua au kubuni biashara mpya au kuiendeleza ile ya zamani kwa ajili ya kuwekeza na kutoa huduma stahiki kwa jamii pana, hivyo tuamue sasa kuwa katika hali hiyo katika jukwaa la dunia ili kuzifaidi fursa za uchumi za ndani na nje ya nchi
Uchumi wa dunia umebadilika, uchumi wa soko katika utandawazi ndio unashikilia mfumo wa kiuchumi wa dunia ili kuharakisha maendeleo kwa kutoa ajira mbadala kwa kujiajili, kujitegemea na kujenga uwezo wa kujiamini katika maisha na biashara kubwa dhana ya ujasiliamali chini ya kongano bunifu inahitajika
Wahenga walisema huwezi kuzuia sikio lako kusikia lakini unaweza kuzuia mdomo wako usiseme, nami kwa hakika nasema nauzuia mkono wangu usiandike zaidi lakini siwezi kukuzuia msomaji kuendelea kusoma
Mwandishi wa Makala
Anapatikana 0715-335051
www.stephanomango.blogspot.com
 

Sunday, March 25, 2012

HIVI NDIVYO CCM ILIVYOFUNIKA JANA KWENYE MKUTANO WA UDIWANI KATA YA LIZABONI MANSPAA YA SONGEA


Mwenyekiti wa CCM Manispaa ya Songea Hemed Dizumba akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Polisi Kata ya Lizaboni wakati wa kampeni za kumnadi mgombea wa kiti cha udiwani kata ya Lizaboni kupitia chama hicho George Oddo


Mgombea Udiwani Kata ya Lizaboni Manispaa ya Songea kupitia tiketi ya Ccm George Oddo akiomba kura kwa wananchi jana wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya mtaa wa Polisi kwenye kata hiyo


Kama kawaida Ccm bila burudani haiendi, hawa ni baadhi ya kinadada wanenguaji kwenye kampeni hizo

Wananchi waliojitokeza jana kusikiliza mkutano wa Ccm uliofanyika kwenye viwanja vya mtaa wa Polisi Kata ya Lizaboni, katikati anaonekana mgombea akiomba kura kwa wananchi

Saturday, March 24, 2012

VIONGOZI WA MKOA WA MTWARA NA RUVUMA WAASWA KULITA MKONGA WA TAIFA

       Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu
Na Agustino Chindiye,Tunduru
VIONGOZI wa Mikoa ya Ruvuma Mtwara na maeneo yanayopitiwa na Mkongo wa Taifa nchini wameombwa  kuulinda na kuhakikisha kuwa Mkongo wa Taifa haukatwi wala kuhujumiwa kwa njia yoyote ile.

Ombi  hilo  limetolewa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa ambaye anaendelea na ziara ya kukagua Mkongo wa Taifa katika Mikoa ya kusini.

Pamoja na maagizo hayo pia Profesa Mbarawa alitoa elimu juu ya faida za Mawasiliano ya Mkongo wa taifa  kwa viongozi wa Ngazi za Vijiji, Wilaya na hata kwa wananchi wachache kila alipokutana nao kikubwa akihimiza ulinzi wake na kueleza kuwa nyaya zilizo wekwa katika Mkongo huo hazina soko popote Duniani na kwamba atakaye fanya uharibifu wowote atawasababishia wenzake kukosa mawasiliano tu.

Aidha katika hotuba hiyo kwa viongozi hao alisema kuwa mawasiliano kupitia Mkongo wa Taifa yataiwezesha Tanzania kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo katika sekta za Biashara, Uzalishaji mali, Elimu na Afya, pamoja na Ulinzi.

Akizungumzia matatizo ya mawasiliano ya simu za Mkononi yaliyoanza kujitokeza katika siku za Karibuni Prof. Mbarawa alikiri kuwa hali hiyo inatokana na mitambo ya kampuni za simu zilizowekeaz nchini kuwa hivi sasa zimeanza kuelemewa na wingi wa huduma na wateja.

Akifafanua taarifa hiyo Profesa Mbarawa alibainisha kero na matatizo ya simu za Mkononi kutounganishwa vizuri pale mtumiaji anapopiga ama kukoroma, kampuni za Simu kupiga matangazo ya biashara kwanza kabla ya  kumuunganisha mtumiaji anapotaka kuongea na mwingine ama mitambo kutofanya kazi ambayo yamekua yakilalamikiwa na wananchi

Ziara hiyo ya kiukaguzi zaidi, Waziri Mbarawa akipita katika vituo na njia ambazo Mkongo wa Taifa umelazwa kuunganisha mawasiliano kati ya Mkoa na Mkoa ikiwa ni awamu ya kwanza, kabla ya awamu nyingine ambapo wilaya zote pia zitaunganishwa.

Naye Mbunge wa jimbo la Tunduru Kusini ambaye alikuwa mwenyeji wake Abdalah Mtutura alisema kuwa alilazimika kumpeleka Waziri huyo katika Tarafa ya Nalasi ali akajionee maelfu ya wananchi wanaoishi huko huku wakiwa hawana huduma za mawasiliano wala hawasikilizi Radio yoyote ya Tanzania huku ahadi iliyotolewa na Rais kuwa wangejengewa vituo vya kuwawezesha kupata mawasiliano hayo ikiwa haija tekelezwa.

Awali akimsomea taarifa ya maendeleo ya Wilaya hiyo Mkuu wa Wilaya ya Tunduru  Juma Madaha alibainisha kuwa mbali na kuwepo kwa utitiri wa makampuni ya simu ya Ttcl.Vodacom, Tigo, Zantel na Airtel lakini huduma hiyo imekuwa ikipatikana kwa uhakika katika makao makuu ya Wilaya na Vijiji vichache.

Alisema Wilaya hiyo ina ukubwa wa eneo la kilometa za mraba 18,778 ikiwa na tarafa 7. kata 35 na Vijiji 148 na kwamba ipo umbali wa Kilometa 1264 kutoka jijini Dar es Salaam kupiti makao makuu ya Mkoa wa Ruvuma Mjini Songea na Kilometa 800 kutoka Dar es Salaam kupitia Masasi Mkoani Mtwara na Mikoa wa Lindi nakuongoza kuwa hali hiyo inapaswa kuangaliwa na serikali katika uimarishaji wa miuondo mbinu yake.
Mwisho


Thursday, March 22, 2012

DARAJA LASABABISHA KAPTENI KOMBA ASHINDWE KUWAPA POLE WAHANGA

Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi Kapteni John Komba

Na Gideon Mwakanosya, Nyasa
MBUNGE  wa Jimbo La Mbinga Magharibi Kapteni mstaafu John Komba ameshindwa kuendelea na ziara yake ya siku mbili ya kwenda kuwapa pole ndugu wa watu wanao daiwa kuwa wamekufa maji na wengine kujeruhiwa vibaya baada ya gari waliyo kuwa wakisafiria kutoka Mbinga mjini kwenda kijiji cha Ngumbo kusombwa na maji wakati likiwa linavuka daraja la mto mnywamaji na kusababisha watu wanne kufa maji na majeruhi wawili kufuatia daraja la mto mbuchi kutitia na kusababisha kushindwa kupita magari
Hata hivyo Kapteni Komba alifanikiwa kufika nyumbani kwa marehemu Mwalimu Lucas Godon Mbunda wa kijiji cha Mkili ambako familia ya marehemu pamoja na ndugu na jamaa walikuwa wakiendelea kuomboleza msiba na aliwapa pole na kutoa rambirambi na alitoa ahadi ya kuwalipia ada watoto wawili wa marehemu Mbunda wanaosoma katika shule ya sekondari ya bweni ya Chipole inayomilikiwa na Kanisa la Katoliki  iliyopo wilaya ya Songea vijijini na shule ya sekondari ya Bweni ya Beroya iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Kapteni Komba alifafanua zaidi kuwa analazimika kuchukua jukumu hilo la kuwalipia ada ya mwaka mmoja watoto wa marehemu Mbunda ambao wameachwa wakati mgumu kwani marehemu Mbunda kabla ya kukutwa na umauti alikuwa anatoka Mbinga ambako alikwenda kuhakiki taarifa za akaunti yake ya Benki ya NMB na kuchukua mshahara wake wa mwezi uliopita jambo ambalo limeonesha wazi kuwa watoto hao wanahitaji msaada zaidi wa kulipiwa ada ili waendelee na masomo ambapo fedha zinahitajika Shilingi laki nane kila mmoja .
Kapteni Komba ambaye aliongozana na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Mbinga wakiwemo Katibu wa CCM wa wilaya hiyo Anastasia Amasi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga Oddo Mwisho aliendelea na ziara yake hadi katika kijiji cha Kihagara ambako alishindwa kuendelea na safari yake baada ya daraja la mto mbuchi kutitia kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha magari kushindwa kupita kwenye daraja hilo.
Wakiwa kwenye eneo la daraja la mto Mbuchi Diwani wa kata ya kihagara (CHADEMA)  Steven Pata alimweleza Mbunge Kapteni Komba  kuwa machi 14 mwaka huu  wakati maafa makubwa yaliyotokea ya vifo vya watu wanne kufa maji na watu wengie kujieruhiwa wakati gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji pia mvua hizo zilisababisha daraja la mto Mbuchi kutitia hivyo aliiomba Serikali ione umuhimu wa kuchukua hatua za haraka za kulitengeneza daraja hilo amabako ni kiungo kikubwa kutoka Liuli na kihagara  na pamoja na wanachi wa kutoka kata za Lihundi, Lundu, Mbaha na Lituhi .
Kwa upande wake Meneja wa wakala wa barabara (TANROADS) mkoani Ruvuma Mhandisi Abrahamu Kissimbo alisema kuwa kikosi cha wataalamu wake kimeshafanya tathimini ya uharibifu wa miundombinu uliotokea katika daraja la Mbuchi na kwamba ameahidi kuwa ndani ya wiki mmoja mara tu baada ya kufika vipuli vinavyo hitajika kwenye daraja hilo ujenzi huo utakuwa umekamilika na amepiga marufuku pikipiki na magari kupita kwenye daraja hilo na watakao kamatwa watachukuliwa hatua.
Machi 14 mwaka huu majira ya saaa nane usiku gari aina ya Landlover wanteni yenye namba za usajili T 492 AWY ambalo lilikuwa klikitoka Mbinga kwenda Ngumbo huku likiwa limesheheni abiria pamoja na mizigo lililokuwa likiendeshwa na Bosco Hyera lilisombwa na maji wakati linavuka kwenye daraja la mto Mnywamaji na kusababisha watu wanne kufa maji na watu wengine wawili kujeruhiwa vibaya.
 Mwisho

Wednesday, March 21, 2012

KIKONGWE CHA MIAKA 75 CHASOMBWA NA MAJI NA KUFARIKI DUNIA

Na Steven Augustino,Tunduru

BIBI kizee wa Miaka 75 amefariki dunia baada ya kusombwa na maji yaliyo furika katika Mto uliopo katika Kitongoji cha Mchololo katika kijiji cha Tulieni Wilayani Tunduru.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa Bibi huyo aliyefahamika kwa jina la Laina Abdurahamani alikuwa na mkasa wakati akijaribu kuvuka mto huo wakati akitokea shambani kwake.

Taarifa hiyo iliendelea kufafanua kuwa akiwa katika harakati hizo ghafla mkondo wa maji makali yalimchukua na kuondoka.

Walisema baada ya tukio hilo wasamalia wema walipiga kelele za kuomba msaada na kwamba hadi wanafika waogeleaji katika eneo hilo walimkuta bibi huyo akiwa amekwisha fariki dunia na kufanikiwa kuuokoa mwili wake.

Mganga aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu Laina Dkt. Goerge Malawi alisema kuwa chanzo cha kifo hicho kilitokana na marehemu kunywa maji mengi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma  Michael Kamuhanda amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na akatumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kuacha tabia za kuishi kwa mazoea na akahimiza kudumisha utamaduni wa kuvushana.

Hili ni tukio la pili kusababisha kifo likifuatiwa na tukio la hivi karibuni ambapo hivi karibuni Mkazi waKijiji cha Kangomba said Abubakari (43)  alilipotiwa kufariki dunia baada ya kupigwa na radi huku kukiwa na taarifa za  946  vyoo 35 vimebomolewa kutokana na mvua
hizo.

Mwisho

Sunday, March 18, 2012

WANNE WAKAZI WA DAR WAKAMATWA SONGEA NA MENO YA TEMBO

     Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda

NA DUSTAN  NDUNGURU,SONGEA.

WATU wanne wakazi wa jijini Dar es salaam wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kukamatwa na nyara za serikali(meno ya tembo) zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni sita.

Akiongea na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoani hapa Maiko Kamuhanda alisema watu hao walikamatwa katika kijiji cha Suluti kwenye maeneo ya mashamba ya NAFCO wilayani Namtumbo aprili 15 mwaka huu majira ya saa 2.30 asubuhi.

Kamuhanda alisema watu hao walikamatwa na askari wa doria baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema wa kijiji cha Suluti.

Aliwataja majangili yaliyokamatwa kuwa ni John Andrew(30) ambaye ni dereva wa gari,Hemed Geofrey(30),Idd Manase(32) na Modesta Eliakim(25) wote wakazi wa Dar es salaam.

Kamuhanda alifafanua kuwa majangili hayo yalikamatwa yakiwa na vipande 30 vya meno ya tembo ambayo walikuwa wamepakia katika gari ambayo ilikuwa imebandikwa namba bandia DFP 7208 aina ya TOYOTA Landcruiser.

Alisema kwenye kadi ya gari hilo inaonyesha namba T.125 ATD Toyota Landcruiser mali ya Morrice Christopher Meenda na kwamba meno hayo ya tembo walikuwa wakiyapeleka Dar es salaam.

Kamanda huyo wa polisi aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana na polisi kwa kutoa taarifa mbalimbali na kwamba mpango uliopo ni kwa jeshi hilo kuendelea kukabiliana na majangili hayo.

Hata hivyo alisema polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

                MWISHO.

NYUMBA 946 ZALIPOTIWA KUBOMOKA WILAYANI TUNDURU

                   Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Madaha

Na Steven Augustino,Tunduru

NYUMBA  946 zimeripotiwa kubomoka kutokana na  mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mfululizo Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma na kuwaacha wakazi wake wakiwa hawana makazi.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Tunduru, Afisa Tarafa wa tarafa ya Matemanga  Ally Hatibu na kuongeza kuwa pia mvua hizo zimebomoa vyoo 35 na kusomba mazao katika mashamba ya wakulima 56 na kwama hivi sasa wananchi hao wanahifadhiwa na Ndugu, jamaa na marafiki katika maeneo yao.

Hatibu aliendelea kueleza kuwa pamoja na matukio hayo pia. Mvua hizo zimeharibu vibaya  miundombinu ya barabara, Madaraja  yanayounganisha kati ya Wilaya hiyo na makao makuu ya Mkoa huo barabara za kwenda vijijini.

Akifafanua taarifa hiyo  Hatibu alisema kuwa Tarafa ya Milingoti ndiyo iliyo athirika zaidi kutokana na kubomokewa na nyumba 716 huku takwimu zikionesha kuwa tarafa ya Lukumbule ikifuatia kwa kuwa na nyumba 230 zilizo bomoka kufuatia mvua hizo.

Aidha takwimu za maafa hayo zinaonesha kuwa Kata ya Nakayaya ndiyo inayo ongoza kutokana na kubomokewa na Nyumba 122, Kata ya Milingoti 99, Masonya 88, Nanjoka 57,Mchangani 54 huku kata ya majengo ikishika nafasi ya mwisho kutokana na kubomokewa na nyumba 46.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo daraja lililobomoka ni la mto Masonya liliteteleka kutokana na mto huo kujaa pamoja na madaraja ya mito Nasanga na Msinjewe pamoja na mto Mkandu barabra iendayo katika vijiji vya tarafa za Lukumbule, Nalasi na Mchoteka na kusababisha usumbufu
kwa wanananchi kutokana na baadhi ya magari kusitisha safari za kwenda na kuingia mjini Tunduru huku kukiwa na wimbi la ongezeko la nauli kwa magari yanayokubali kufanya safari hizo kwa kubahatisha.

Hatibu aliendelea kubainisha kuwa miongoni mwa usumbufu unaowapata madereva wanaofanya safari katika maeneo hayo  ni pamoja na kutozwa fedha na wananchi walio panga miti katika maeeenero yaliyo haribika na kuwatoza kati ya Shilingi 5000 na Tsh.2000 kwa kila gali linapo vuka kuelekea upande wa pili.

Alisema kufuatia hali hiyokamati ya Ulinzi na usalama ililazimika kuwatembelea wahanga na kuwapa pole kwa mkasa huo pamoja na kujionea uharibifu wa madaraja hayo na kupeleka taarifa za maafa hayo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ili kuangalia uwezekano wa wahanga hao kupatiwa msaada Serikalini.

Kuhusu uharibifu wa miundombinu ya Barabara na madaraja hayo, Hatibu alisema kuwa tayari Meneja wa Wakara wa Barabara Mkoa wa Ruvuma (TANROAD`s) amekwisha tuma wataalamu Wilayani humo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa barabara zote zinafunguka na shughuli kuendelea kama kawaida.

Mwisho

Saturday, March 17, 2012

RAIS KIKWETE, VIJANA MITAANI WANAKUULIZA HIVI............................?



                    Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete

Na Stephano Mango, Songea

RAIS Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, naomba leo nitumie nafasi hii kuzungumza nawe juu ya mambo machache ambayo nimekuwa nikisikia vijana wanayazunguza na kutamani kuyafikisha kwako juu ya serikali yako na namna wanavyokutazama katika nafasi yako juu ya mustakabali wa maisha yao chini ya jua hili.

Hivyo ninaomba ufahamu kuwa vijana wengi wana mengi ya kusema nawe kama ilivyo kwa watanzania wengi, tatizo kubwa ni namna ya kufikisha kauli yao hiyo kwako. Hivyo mimi naomba nibebe wajibu huo wa kuwa kipaza sauti cha vijana kwa kufikisha kauli yao kwako.

Awali ya yote napenda kukupa pole kutokana na majukumu mengi ya kuwatumikia watanzania, majukumu uliyokabidhiwa na wananchi kupitia sanduku la kura mnano tarehe 14.12.2005 ambayo mpaka leo bado unayo.
Mheshimiwa Rais, kwa muda mrefu sasa vijana wa kitanzania wamekuwa wakilalamika juu ya mazingira magumu yanayowakabili katika harakati zao za kimaisha. Hii inatokana na jinsi hali ilivyobadilika tofauti na matarajio waliyokuwa nayo juu yako kabla na baada ya kuchaguliwa kwako kuwa rais wa awamu ya nne wa Tanzania.
Hivyo wamekuwa wakijiuliza kama ni kweli kuwa ile kauli ya “Maisha bora kwa kila Mtanzania” na ile ya “Tanzania yenye neema yawezekana” inawahusu wao au ni kwa wale wachache tu walio katika mazingira ya kujichukulia Chao Mapema.
Ninakumbuka wakati unapiga kampeni na kuomba kura kwa watanzania mwaka 2005 na mwaka 2010 ulikuwa na kauli mbiu nzuri juu ya vijana kuwa utawawezesha Vijana kujiajiri
Mheshimiwa Rais, wakati uliporudi jijini Dar es salaam baada ya kuteuliwa Mjini Dodoma kuwa mgombea wa CCM katika uchaguzi mkuu wa 2005, ulipata mapokezi makubwa sana ambapo pamoja na mambo mengine ulikutana na kilio cha vijana juu ya matatizo mbalimbali yanayowakabili.
Hivyo walipoongea nawe katika Ukumbi wa Diamond Jubilei ulisema kuwa umesikia kilio chao na hivyo uliahidi kujitahidi kutafuta namna ya kuwasaidia vijana hao kutoka katika hali ngumu ya maisha inayowakabili.
Hata hivyo hali imekuwa ni tofauti na matarajio yao tangu serikali yako iingie madarakani. Swali la vijana ni je ulikuwa unawalaghai au kuna vitu ulivyokutana navyo ikulu vikakwamisha dhamira yako njema uliyokuwa nayo dhidi yao?
Swali hili limekuwa likiulizwa kwani mambo yanayoendelea kwa vijana baada ya kuingia madarakani serikali yako yamewakatisha tamaa na wengi wamekuwa wakijuta kwani hawakutarajia kuona hayo hasa kwa kuzingatia kuwa eti (ulikuwa mshikaji wao) katika hali ngumu ya maisha.
Vijana wamekuwa wakiuliza kuwa je zile ajira milioni moja ulizoahidi kila mwaka bado zipo au zinachukuliwa na wawekezaji wa nje au ni kwa vijana wapi, na kwa wale uliowaahidi kuwawezesha kujiajiri ni hao serikali yao iliyoamua kuwafukuza mjini kwa kuwa wanachafua miji kwa kutembeza bidhaa mikononi na kuuza mitumba katika maeneo ambayo mnadai si maeneo si rasmi?
Je ni wapi mlipowatengea vijana hao penye nafasi na miundo mbinu bora na wakakataa kwenda? au ndio Machinga Complex yenye kiza kinene?
Mheshimiwa Rais, hivi karibuni nilikuwa jijini Dar es salaam, ambapo kwa bahati nzuri nilipata nafasi ya kuzunguka katika maeneo mengi ya jiji hilo, kwa sehemu kuwa vijana waliokuwa wakifanya biashara zao za kuuza mitumba na bidhaa nyingine (maarufu kama wamachinga), wameondolewa na kupelekwa katika maeneo yasiyo na biashara wala miundo mbinu,
Matokeo yake wengi wamekata mitaji yao kiasi cha baadhi yao kuamua kujiua baada ya kubomolewa kwa vibanda vyao bila kujua kama huko walipokuwa wanapelekwa ni sehemu sahihi au la, pia zoezi hilo limehamia pia kwa wapiga debe na makondakta wasio na shughuli maalum katika vituo mbalimbali vya daladala.
Hata hivyo licha ya hatua hiyo kuchukuliwa kwa ajili ya vijana hao ambao nao ni wahitaji na wamekuwa wakitegemea kupata riziki kupitia maeneo hayo, bado hakuna hatua mbadala zimechukuliwa katika kuwasaidia wahusika hao ili wasiende kufanya zile biashara za kutegemea mtaji wa nguvu zao (wizi, ujambazi, umalaya na ukahaba).
Zoezi hili si la jijini Dar es salaam tu, bali ni katika maeneo yote ya nchi yetu. Kwa sehemu kubwa inaonekana kuwa tumehamisha tatizo kutoka sehemu moja na kulipeleka sehemu nyingine, kwani hakuna mbinu mbadala za kuwasaidia hao tuliowaondoa mjini.
Mheshimiwa Rais, pamoja na kauli nzuri za viongozi wetu juu ya kuwataka vijana kurudi vijijini kwa ajili ya kujiingiza katika kilimo kwanza na ufugaji lakini ukipita katika maeneo mengi ya vijijini utakutana na hali mbaya ya maisha ya huko na wala hakuna miundo mbinu mizuri wala pembejeo kwa wale wote wanaoamua kujikita katika sekta hizo muhimu.
Na kwa wale wachache wanaojifanyia shughuli hizo, bado hawapati soko wala mazao yao hayanunuliwi kwa wakati na kama wanauza mazao yao basi ni kwa wafanyabiashara ambao wananunua mazao hayo kwa bei ya chini na hivyo kuwa ni hasara kwao,nani atawasaidia hao katika mikakati yao ya kujikwamua kiuchumi?.
Vijana wanauliza, mbona wao hata kama wamejiunga katika vikundi vya watu wasiopungua hamsini hawawezi kupata mikopo ili nao wafanye biashara zitakazowanyanyua kiuchumi na hivyo kuitwa wajasiriamali wa ndani? Kwani kila wakifanya hivyo hawafanikiwi, kwa hili unasemaje mheshimiwa rais?

Mheshimiwa Rais, vitendo vya unyanyasaji na kuwaua vijana na wachimbaji wadogo vinavyofanywa na wachimbaji wakubwa ambao wengi si raia katika maeneo mbalimbali ya migodi ya madini yetu ni sehemu ya kilio cha kila mara huku serikali yako ikifumbia macho bila kutoa walao kauli ya kukemea matendo hayo ni sehemu ya swali ambalo vijana wamekuwa wakiuliza.
Wao wana nafasi na kauli gani katika kujinufaisha na ujtajiri huo ambao ni sehemu ya neema kubwa Mwenyezi Mungu aliyoitunukia Tanzania na sasa inachukuliwa na wageni kama mali isiyo na wenyewe? Ni vema ukawajibu vijana hata hili.
Kuna vikundi mbalimbali vya vijana katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu wanaoishi na VVU, lakini pamoja na wao kukaa kama familia, bado hawapati misaada itakayowawezesha walao kuwa na miradi ya kuwapatia mapato ili waweze kujikimu kimaisha
Kwani iwapo vijana hawa wasipopata misaada ni hatari sana kwa maisha ya watanzania wengine kwani wanaweza kuamua kusambaza VVU kwa makusudi bila kujulikana licha ya kuwa wamekuwa wazi kuwa wanaishi na VVU.
Kwasababu ,wengi wao wamekuwa wakitongozwa na wanaume/wanawake wengine kwa kuwa hawajionyeshi na kwa kweli wengi wao ni wazuri wa sura na miili na afya zao ni nzuri na wala huwezi kuwatilia shaka kama hutaelezwa kuwa wanaishi na VVU. Hili pia ni swali la vijana kwako.
Mheshimiwa Rais, nina mengi ya kuzungumza nawe kwa niaba ya vijana wa Tanzania, hata hivyo naomba uniruhusu niseme kuwa umefika wakati wa kuwasiliza vijana, kwani kilio kikubwa cha vijana ni kutokusikilizwa.
Hivyo ninakuomba sana ujitahidi pamoja na ratiba yako kutingwa na shughuli nyingi za nchi, utenge walao siku moja ili ukae na vijana wa Tanzania uwasikilize kwani nina imani kuwa wana mambo mengi ya kusema nawe.
Ninayasema haya kwa kuwa mpaka sasa hakuna waziri yeyote wa Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana au hata manaibu mawaziri wao, aliyewahi kupanga na kukaa na vijana na kuwasikiliza katika kilio chao.
Fahamu kuwa kwa sehemu kubwa inawezekana kuwa mengi huyafahamu na wala hujayasikia yote, lakini ukipata nafasi ya kuwasikiliza vijana utafahamu hayo na mengi zaidi ambayo ulikuwa hujayasikia.

Mheshimiwa Rais, nimalizie kwa kusema kuwa, vijana wanahitaji kusikia jambo jipya, wengi wanatamani kupata nabii mpya wa kuwaokoa na wala habari za kisiasa si za lazima kwao kwani wengi wana maisha magumu, hawajui watakula nini kesho na wala maisha yao watayaboresha vipi.
Hivyo unaombwa kubeba wajibu huo kwa nguvu mpya ili vijana wakiri kuwa sasa wameuona ukombozi ulio tayari kwao. Ni matarajio ya vijana kusikia kitu juu ya hayo na mengine mengi ambayo hayajaandikwa hapa ili waweze kujua kuwa wewe ni mkombozi wao au wasubiri mwingine.
Mwandishi wa Makala
Anapatikana 0715-335051
www.stephanomango.blogspot.com

Friday, March 16, 2012

WANNE WAHOFIWA KUFA MAJI KUTOKANA NA GARI KUSOMBWA NA MAJI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda

NA DUSTAN  NDUNGURU  SONGEA.

WATU wanne wanahofiwa kufa maji na wengine watatu kunusurika katika wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma baada ya gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji kwenye mto Mnywamaji kijiji cha Ngumbo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo limetokea machi 14 mwaka huu majira ya usiku katika kijiji cha Ngumbo.

Kamuhanda alisema kuwa gari lenye namba za usajili T492 AWY Landrover 110 lililokuwa likisafiri kutoka Mbinga mjini kuelekea katika kijiji hicho lilisombwa na maji wakati lilipokuwa likivuka katika daraja la mto Mywamaji ndani likiwa na watu saba.

Alifafanua kuwa kujaa kwa maji hayo kulifuatia mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha na kwamba maji hayo yalikuwa yameambatana na mawe jambo ambalo lilisababisha gari hilo kusukumwa.

Kamuhanda aliwataja wanaohofiwa kufa maji kuwa ni Lukas Mbunda(59) ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nkili,Maiko Due(39) mkazi wa Mbinga mjini na Evangelista Mzili(37) mkazi wa kijiji cha Unango.

Alimtaja mtu wa nne ambaye mwili wake umepatikana ni Aidan Mahundi(19) ambaye ni fundi magari mkazi wa kijiji cha Paradiso na kwamba watu watatu walionusurika ni Mathias Mbunda,Rose Mpombo ambao wamelazwa katika kituo cha afya Nkili na dereva wa gari hilo John Hyera ambaye alitoweka mara baada ya tukio hilo.

Hata hivyo jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

             MWISHO.